Simon Sirro: Tunamhitaji Gwajima, alizungumza maneno ya kichochezi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi hilo linamuhitaji Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa kuwa kuna mkanda wameupata unaosemekana ni wake ambao unazungumza maneno ya kichochezi.

Kamanda Sirro alisema: “Tumepata clip (mkanda) inayosemekama ni ya kwake. Tunamtaka athibitishe kama hayo maneno ni ya kwake. Na kama ni yeye ameyasema, anaelewa nini kuhusu kile alichokizungumza kwa sababu hayo maneno ni kichochezi. Tupo kwenye uchunguzi mama yangu.”

Jana, polisi jana walipiga kambi kwa saa saba kwenye geti la nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wakitaka kumkamata bila ya mafanikio.

Polisi hao walikuwa kama wageni wa askofu huyo wakisubiri wafunguliwe geti, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:10 jioni walipoamua kuondoka wakitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye namba za kiraia, ambalo kwa muda wote huo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa geti hilo.
 
Hebu tujadili,maana kwa muktadha ulivyo na jinsi ninavyowasikia wachangiaji wa kigoda,wanamkosoa rais Moja kwa moja
 
Tunajua watendaji wote serikali wanatamani sana kufanya kazi kumfurahisha mkuu. Lakini wajikumbishe kuwa wakubwa nao huwa hawapendi sana kuona watu wanajipendekeza kupita kiasi
 
Kamanda SIRRO naye aangalie anataka kuanza sifa za KOVA, sio kila jambo ni la kuita kuhoji
Mkuu haya mambo we acha tu,
Wakubwa wakisema jamba hata kama hujisikii utajamba tu

Mradi tu uchafue hali ya hewa
 
Back
Top Bottom