Simchukii mtu, Lakini kwa utaratibu huu tutafika?

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
906
Leo, pamoja na kwamba ningependa kusema sana, sisemi. Ila naomba tuangalie hizi picha mbili, halafu kwa kutumia akili ya kawaida kabisa tuone kama vipaumbele vya serikali vinalenga kumsaidia nani!

Napenda nisieleweke vingine. Swala la ulinzi na usalama nalo linapaswa kupewa kipaumbele. Lakini tunamlinda nani kama tunazuia kibaka mmoja huku kuna kinamama kumi na watoto wao wako hatarini kufa?

Kwa nionavyo mimi ingekuwa heri kama tungenunua walau ambulance kadhaa ili kuwawahisha hao kinamama huko kusikokuwa na vitanda wala madawa. Ingesaidia japo wasafiri comfortably kwenda huko wasikojua hatima yao. Angalau.

Kwa hali hii tutafika?

wajawazito.jpg

polisi.jpg
 
Daaaaaah kweli inauma sana, hizo ndinga ukichukua 30 unajenga jumba jingine na vitanda vya maana
 
Fedha za safari za Vasco katika kipindi chake zingetosha kuweka vifaa vya kisasa na dawa za kutosha kwenye hospitali zetu. Pia zingeweza kugharamia ujenzi wa barabara mbadala na kupunguza foleni Dar es Salaam.

Kimsingi vipaumbele kwa viongozi wetu ni maisha yao binafsi, familia na rafiki zao.
 
Ukiwa mjinga ni mjinga tu sasa,kila siku ni hii picha tu

Mpendwa Mtia nia,

Nilikuwa nasema tu kuwa vipaumbele vya serikali vinanipa maswali kuhusu malengo na dhamira. Picha ni zile zile. Za kila siku tu. Lakini wewe unaonaje? Mnafaa kweli kuendelea kupewa dola kwa maamuzi ya aina hiyo?

Kabla hujajibu, nakushauri uliangalie hilo katika sura hizi:

1. Una mkeo mjamzito, umembeba kwenye basikeli, halafu ukiwa unakaribia mjini unakutana na msururu wa magari hayo ta polisi yanatoka bandarini! wewe unadhani ungejisikiaje? ungekuwa proud kuwa una serikali?

2. Wewe ndiyo una mimba ya miezi tisa, umefanikiwa kukimbizwa hospitali halafu unafika huko unakuta hakuna hata pa kupumzika. Madaktari hawatoshi, na usafi wa hospitali unatia shaka. Kabla hata hua-adopt mazingira mapya ya kulala chini, kuumwa na mbu nakukanyaga mikojo yenye umri wa miezi kadhaa chooni, mara hao madaktari wachache nao wamegoma! unaposhangaa unaambiwa, "wanapataga shida sana hao kusoma, hata hivyo wana madai ya muda kweli kweli" Niambie wewe ungefikiriaje? serikali yako ni sikivu? inajali? ungeendelea kubakia hospitali au ungeondoka? ungekwenda wapi?....binafsi siombei katika muda kama huo hali ya leba ikukamate! Halafu unasikia kwenye taarifa ya habari kuwa serikali imeagiza landcruiser kama mia hivi na magari ya washawasha kama 700 kwa ajili ya polisi!

Baada ya kulitafakari mpaka hapo, unaweza kujibu tena!
 
Wanaume inabidi wafanye mgomo wa kuwatia wake zao mimba kwa kuwa hali ni mbaya kihivyo na serikali ndo hivyo tena. Hii huenda ikapunguza tatizo!!!!!
 
Wanaume inabidi wafanye mgomo wa kuwatia wake zao mimba kwa kuwa hali ni mbaya kihivyo na serikali ndo hivyo tena. Hii huenda ikapunguza tatizo!!!!!

Huo mgomo utakuwa batili,sawa na maandamano bila kibali cha polisi wa bongo...
 
Fedha za safari za Vasco katika kipindi chake zingetosha kuweka vifaa vya kisasa na dawa za kutosha kwenye hospitali zetu. Pia zingeweza kugharamia ujenzi wa barabara mbadala na kupunguza foleni Dar es Salaam.

Kimsingi vipaumbele kwa viongozi wetu ni maisha yao binafsi, familia na rafiki zao.

Siyo safari tu, kuna mambo mengi sana yasiyo ya msingi yanafanyika. Kwa mfano, kuna haja gani kuandaa maadhimisho ya siku ya maji, wakati tunajua hatujafanya lolote kupunguza kero hiyo? Na kama tungeamua kutumia fedha hizo kwa mambo ya kijamii, je tungechimba visima vingapi?....Yaani badala ya kufanya shughuli, mbona ingekuwa much better kama tungeamua kugharimia mojawapo kati ya mambo yanayotusumbua?..sasa piga hesabu mambo ya aina hiyo yako mangapi uniambie, tungesaidia kiasi gani kupunguza kero za wananchi wetu?
 
kawaulize libya na somalia au kenya watakwambia kipi ni cha kwanza na kii ni cha pili,
 
Huo mgomo utakuwa batili,sawa na maandamano bila kibali cha polisi wa bongo...
Mgomo huo utasababisha wanawake wakawashitaki wanaume Polisi kuwa wamegoma. Alafu Polisi watawakamata wanaume wote waliogoma na kuwasweka mahabusu. Wakifikishwa mahakamani watajitetea kuwa wanawake wanahongwa kanga na tsheti na chama fulani ambacho ndicho chanzo cha matatizo yaliyopelekea mgomo huo. Wanawawake watajitetea kua tatizo ni wanaume ambao wamekuwa hawaoni mbali na wamekuwa wakikichagua chama cha mafisadi ambacho sasa kukisababisha matatizo. Wanaume wanaleta mgomo kwa kutowajibika kwao kukiondoa madarakani chama cha mafisadi. Hakimu ataamuru kuwa kesi iondolewe mahakamani na kila mwanaume akaelewane na mkewe kuwa huu ni wakati muafaka wa kukiondoa chama cha mafisadi madarakani la sivyo athari kwafamilia izidi kuwa kubwa!!!
 
Ni bora mara100000% wazae wakiwa katika hali hiyo kuriko kuzalia kwenye nyumba kubwa wakati mabomu ya alshababu yanatua juu ya miili yao na watoto wao.

Najua haujawai kuona au ni miemuko ya siasa uchwara za leo tulizonazo vijana wengi lakini nenda siria/burundi uwaulize wakina mama wanaozalia njiani na barabarani watakupa jibu sahihi,na utakuwa mwisho wako wa kuleta hiki ki uzi chako humu.
 
Elly B

Wananchi wanawapenda mno CCM acha wakione cha moto mie siilaumu serikali maana ni hao hao akina Mama na kura zao nyingi kwa CCM na hawaambiliki . Acha wakione .
 
Last edited by a moderator:
Ni bora mara100000% wazae wakiwa katika hali hiyo kuriko kuzalia kwenye nyumba kubwa wakati mabomu ya alshababu yanatua juu ya miili yao na watoto wao.

Najua haujawai kuona au ni miemuko ya siasa uchwara za leo tulizonazo vijana wengi lakini nenda siria/burundi uwaulize wakina mama wanaozalia njiani na barabarani watakupa jibu sahihi,na utakuwa mwisho wako wa kuleta hiki ki uzi chako humu.

Sasa magari ya washawasha yanaweza kuzuia Alshababu?nauliza tu
 
Mgomo huo utasababisha wanawake wakawashitaki wanaume Polisi kuwa wamegoma. Alafu Polisi watawakamata wanaume wote waliogoma na kuwasweka mahabusu. Wakifikishwa mahakamani watajitetea kuwa wanawake wanahongwa kanga na tsheti na chama fulani ambacho ndicho chanzo cha matatizo yaliyopelekea mgomo huo. Wanawawake watajitetea kua tatizo ni wanaume ambao wamekuwa hawaoni mbali na wamekuwa wakikichagua chama cha mafisadi ambacho sasa kukisababisha matatizo. Wanaume wanaleta mgomo kwa kutowajibika kwao kukiondoa madarakani chama cha mafisadi. Hakimu ataamuru kuwa kesi iondolewe mahakamani na kila mwanaume akaelewane na mkewe kuwa huu ni wakati muafaka wa kukiondoa chama cha mafisadi madarakani la sivyo athari kwafamilia izidi kuwa kubwa!!!

Umeeleza vizuri...

Ila swali ni je,unaimani na hao polisi?

Baadhi yao usishangae wakaishia kushikwa ugoni na wake wa hao mahabusu waliogoma kuwatimizia haki wake zao....
 
Ni bora mara100000% wazae wakiwa katika hali hiyo kuriko kuzalia kwenye nyumba kubwa wakati mabomu ya alshababu yanatua juu ya miili yao na watoto wao.

Najua haujawai kuona au ni miemuko ya siasa uchwara za leo tulizonazo vijana wengi lakini nenda siria/burundi uwaulize wakina mama wanaozalia njiani na barabarani watakupa jibu sahihi,na utakuwa mwisho wako wa kuleta hiki ki uzi chako humu.

Kanone,

Nashukuru kwa mchango wako.

Bahati nzuri mimi ni kati ya wadau wa usalama katika nchi hii. In fact, hayo ndiyo majukumu yangu ya kila siku ninapoamka na kusema naenda kazini. (Usini-quote vibaya, sijasema nafanya Usalama wa Taifa) Kwa hiyo tutakapoongelea swala la usalama, najua kabisa Syria kuna ladha gani, au Afghanistan kuna shida zipi zinawakuta wanawake na watoto. Na siamini kama umewahi kutia mguu vitani ukaona hiyo ladha! Mimi naijua.

Kwa kuzingatia msingi wa hoja yako, sioni ni vipi unaamini, kwa mfano, polisi na magari kadhaa, wanaweza kupambana na ugaidi wakati kwa jinsi ninavyoona hata vibaka wa kawaida wanawashinda! Labda kabla sijaendelea unifafanulie, wewe usalama unauchukulia kwa sura ipi? Umeshawahi kufanya tathmini ili kujua walau kama tunaweza au hatuwezi kiasi gani kupambana na uhalifu? ......then tutaendelea
 
Back
Top Bottom