hakika Ni Majonzi Makubwa Kumpoteza Mpenda Maendeleo Ya Kweli Kama Mr. Simbo Ntiro.
Mpaka Mauti Yanamfika Simbo Alikuwa Ni Makamu Mwenyekiti Wa Kitengo Cha Ict Cha Tpn (tanzania Professionals Network).
Pamoja Na Mambo Mengi Mazuri Aliyoyaleta Ndani Ya Tpn, Yeye Na Kitengo Kizima Cha Ict Cha Tpn Waliwezesha Tpn Kuwa Na Tovuti Yake Pamoja Na Jarida Tovuti. Pia Baadhi Ya Michango Yake Ilisaidia Sana Kufanikisha Semina Za Mara Kwa Mara Za Tpn.
Moja Ya Ndoto Alizokuwanazo Simbo Ni Pamoja Na Kufanya Juhudi Za Kuhakikisha Kuwa Kuna Uhifadhi Wa Misitu Katika Mlima Kilimanjaro. Pia Alipenda Kuona Siku Moja Wanataaluma Wakiungana Na Kuendesha Miradi Mikubwa Ya Kiuchumi. Pia Alipenda Kuona Watu Wengi Zaidi Wanapata Elimu Ya Juu Na Kuna Mengi Alishauri.
Katika Kipindi Hiki Kigumu, Kwa Niaba Ya Uongozi Mzima Wa Tpn, Wanachama Na Wapenzi Wote Wa Tpn, Tunapenda Kutoa Pole Sana Kwa Ndugu, Jamaa Na Marafiki Wa Simbo Na Wadau Wote Wa Maendeleo.
Sote Tu Katika Njia Moja. Tulitoka Kwa Mavumbi, Tutarudi Kwa Mavumbi
Sanctus Mtsimbe, Tpn