Simbachawene - tuhuma za fumanizi ni utata, lugha gongana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simbachawene - tuhuma za fumanizi ni utata, lugha gongana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Jun 25, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Simbachawene: Sijafumaniwa
  NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, ameibuka na kukanusha vikali uvumi ulioenea jana kuwa amefumaniwa na mke wa mtu mjini Singida usiku wa kuamkia jana na kujeruhiwa mkono kwa kisu. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Karatu jana jioni, Simbachawene ambaye pia ni Mbunge Kibakwe (CCM) mkoani Dodoma, alisema habari hizo ni uongo na kudai kuwa zimeenezwa na baadhi ya wabunge wa Chadema aliokutana nao mjini Singida jana wakati akiwa njiani kwenda msibani Karatu.

  Simbachawene alisema kuwa katika hoteli aliyofikia, kuna mtu alifumaniwa akiwa na mke wa askari na kufafanua kuwa watu walizua jambo hilo kwa kuwa naye alilala katika hoteli hiyo. “Ni uzushi tu walidhani kuwa mimi nimefumaniwa, ukweli ni kwamba jambo hilo halijanitokea. Mimi nilifika hapa jana (juzi) nikitokea Dodoma kuelekea Karatu kuhudhuria msiba wa shemeji yangu,” alisema Simbachawene.

  Aliwataja watu wanaodaiwa kueneza uvumi huo hizo kuwa ni wanachama wanane wa Chadema akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho, Christina Lissu. “Baada ya kufika Singida nilikwenda katika baa moja na kuwakuta wabunge wa Chadema na baadhi ya wanachama, nilipata kinywaji na kurudi hotelini kulala,” alisema Simbachawene. Huku akivua shati kuwaonesha waandishi wa habari kwamba hakukatwa mapanga mikononi kama ilivyodaiwa, alisema kuwa alipoamka asubuhi ndipo alianza kusikia habari kuwa amefumaniwa na mke wa mtu.

  Awali taarifa kutoka Singida zilizowekwa pia kwenye mitandao ya kijamii zilidai kuwa Naibu Waziri huyo alikumbwa na mkasa huo jana alfajiri. Tukio hilo ambalo inaelezwa kuwa lilitoka majira ya saa kumi, baada ya taarifa hizo kumfikia mwenye mke, ilimlazimu mmiliki wa hoteli hiyo kutoa taarifa Polisi ili kuzuia maafa zaidi. Uvumi huo ulidai kuwa baada ya taarifa hizo, iliwalazimu askari Polisi kwenda katika hoteli hiyo ili kumuokoa Simbachawene, ambaye tayari alikuwa amejeruhiwa mkono kwa sime na askari huyo mwenye mke.

  Mara baada ya purukushani hizo katika eneo hilo Naibu Waziri huyo alidaiwa kwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi mkoani Singida,
  ambapo ilidaiwa kuwa katika maelezo yake aliandika jina la Josephat Joseph badala ya kutumia jina lake halisi.

  Hata hivyo, Mbunge Christina Lissu, alisema anashangazwa na taarifa za yeye kuhusishwa kueneza uvumi huo. Alisema walikutana na Naibu Waziri huyo, katika hoteli hiyo, wakiwa wanatoka mkoani Tabora katika kesi na wabunge wa Chadema, Conchesta Rwamlaza, Philipa Muturano na John Mrema ambaye ni Mkurugenze wa Bunge na Halmashauri ya chama hicho. “ Tulipofika Singida nilimwoa Simbachawene nimwita jina, alitufuata na kutununulia vinywaji hapo hotelini,”
  alisema Lissu na kuongeza; “Hata tulipofika hoteli, baada ya muda tukasikia kutoka kwa mmiliki wa hoteli akisema kuna watu wanataka kumharibia biashara. Tulipomuuliza kulikoni? Akasema kwani hamna habari si mmewaona Polisi wakati mnaingia hapa, huku akisema kuna kigogo wa Serikali amefumaniwa na mke wa askari.”

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa alipoulizwa na Mwananchi Jumapili alisema hakuna tukio kama hilo lililotokea mjini Singida wala mahali popote katika mkoa huo. “Huo ni uzushi tu, hakuna tukio hilo mjini Singida na wala sijasikia taarifa zozote za aina hiyo kutoka maeneo mengine mkoani hapa, alisema Sinzumwa.
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hii kitu inaonekana ukweli wake halisi haujaanza kutolewa hii. time will tell.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tuhuma za kufumaniwa ugoni Naibu waziri Simbachawene huko singida ni utata kutokana na lugha gongana ile mbaya.
  1. Simbachawene anasema kuna mtu mwingine aliyefumaniwa ugoni ambaye alikuwa katika hoteli hiyo aliyofikia.
  2. Kamanda wa polisi mkoa wa Singida amekanusha kwamba hakuna jambo kama hilo lilotokea mkoa mzima siku hiyo wakati Simbachawene alisema lilitokea hotelini alikofikia.
  3. Mbunge wa Chadema anasema aliambiwa na mwenye hoteli na kuwaona polisi walipofika kwenye tukio.
  4. Mtuhumiwa Simbachawene alipoenda Polisi aliandikisha kwenye jalada jina lisilo lake la Josephat Joseph.
  Hapa kwa kuangalia tu lugha iliyotumika kutoka kwa watu mbalimbali na mtuhumiwa kuna kujifunga kitanzi kwa vile kuna mgongano unaoashiria kutonyooka vizuri utetezi binafsi wa Simbachawene. Kwa Tanzania tumeshazoea hayo na yaliyotokea Morogoro siku za karibuni ni jambo linaloeleweka vigogo kulindwa kutokana na tuhuma zinazoweza waharibia taswira zao katika jamii.

   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hapo kwenye Red ndiyo utata kabisa
   
 5. Imany John

  Imany John Verified User

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Je simbachawene anaonekana bungeni na suti ya mikono mifupi?

  Je simbachawene ametokea katika tv yoyete kukanusha taarifa hizo?
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umeona Eee! ni mgongano tupu, kamanda wa polisi anakanusha tukio la aina hiyo wakati simbachawene anakubali tukio lilikuwepo lakini si yeye ila mtu mwingine. Hali kadhalika yule mwenye hotel naye alivyowaambia akina Lisu. Kuna kuzunguka mbuyu hapa.
   
 7. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Lets wait and see!!!
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni kawaida ya wabantu kukoleza chumvi zaidi hata kama mpishi alishaitia. Huenda katika purukushani hiyo hakuna kujeruhiwa baada ya kubaini mfumaniwa ni mtu mkubwa na ujuavyo askari polisi wanavyonyong'onyea kwa wakubwa. Badala ya kumtia msukomsuko mfumaniwa yeye alimpigia saluti.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sokomoko la Morogoro la kigogo wa serikali kuibiwa chumbani, siku chache polisi wametoa tamko la tahadhari kwa vigogo kujihadhari na vimwana poa wanaowatia vimelea vya usingizi na kuishiwa kuibiwa.
   
 10. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Uongo una gharama kubwa sana. Subirini tu.
   
 11. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Habari hii nailinganisha na jinsi watu wanavyowapiga vibaka kwa hasira. Hata kama hakuna aliyeibiwa kwenye kundi la wanaomsulubu huyo kibaka, lakini watamponda kwelikweli kwa kukumbukia machungu yanayofanywa na vibaka kwa ujumla. Tafakari!
   
 12. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Muda utafika kila kitu peupeeee
   
 13. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  taarifa ya mwanzo haikuwa na ushahidi wowote hata wa picha sasa muda utafika lini wa kupata ushahidi huo.

  tuachane na mambo ya uzushi yanatupotezea sana muda hapa JF
   
 14. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...watu wazima wameelewa...
   
 15. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kitu chamsingi anachotakiwa kukifanya ng.Josephat Joseph,nikujitokeza kwenye vyombo vya habari kama vile tv na atuonyeshe mikono yote 2,na tumeambiwa akijitokeza atuonyeshe mkono wake wakushoto! JOSEPHAT JOSEPH a.k.a simba+CHAWENE=simbachawene
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kumficha mke wa mtu kwenye hoteli si kitu cha wazi kinachohitaji ushahidi wa mikanda ya picha, wenzetu walioendelea katika haki hutoa hukumu kutokana na mazingira yanayotatanisha. Kauli zinapingana sasa inajenga taswira gani?
   
 17. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,386
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  mods kuweni makini na thread kama hizi pengine zinataka kuchafua reputation nzuri ya JF kwa jamii
   
 18. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,584
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  kama ni kweli basi kiranja mkuu wetu itakuwa alitishiwa ikiwa ataweka picha basi huu mtandao utazikwa kama the .....
   
 19. Imany John

  Imany John Verified User

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Pia ukimya wa Makene na Invisible unatia shaka.
   
 20. Imany John

  Imany John Verified User

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,781
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  UsWEET.
   
Loading...