Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Ukisikia kufuru ndio hii...
Wang'oe tu halafu waihamishie Mtwara kwenda Msumbiji.
hivi atakuwa anamkomoa nani?? ila kwa ninavyomfaham huyo bwana, ni ngumu kuamini kama ni kweli maneno hayo yametoka kinywani mwake.....angesema lukuvi (std VII) Nisingekuwa kuwa na shaka sana......:becky::becky:
Masikini, huyu jamaa anahitaji mapumziko. Apelekwe hospitali.
kauli ya kikwete kwenye gazeti la mwananchi,ya kusema kwamba wananchi wa mtwara awataki mikoa mingine itumie gesi,itatuletea matatizo nchini,maana hiyo ndio itakuwa kauli ya wanaccm,japokuwa sio wana mtwara wanavyotaka.Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kibakwe-CCM,George Simbachawene ametoa mpya.
Amependekeza mitambo ya kuchimba gesi asilia mkoani Mtwara ing'olewe ikiwa ni kuwaadhibu wananchi wa Mtwara aliowaita wahaini. Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Makada wa Chama cha Mapinduzi walioko Ofisi Ndogo za CCM -Lumumba Dar es Salaam, Simbachawene alisema watu wa Mtwara ni waasi na wanapaswa kushughulikiwa ipasavyo.
Mazungumzo hayo yalifuatia nia ya Makada wa CCM kutaka kupata maoni ya Naibu Waziri huyo juu ya nini hasa alijionea alipofanya ziara ya kushtukiza mkoani Mtwara. Simbachawene, bila kubana maneno, amesikika akisema: 'Cha kufanya ni kuwaamuru Wawekezaji wote waliopo katika machimbo ya gesi Mtwara kung'oa mitambo yao ili tuone kama gesi hiyo itatumika nao wananchi hao'
Katika kile kinachoonekana ni kuchoka kuoongoza kwa CCM,baadhi ya makada maarufu wa CCM akiwemo William Lukuvi,kwa nyakati tofauti leo, wameonesha kuguswa na kukubaliana na pendekezo la Simbachawene. Pia inapendekezwa kuwa Mh.Murji (Mbunge wa Mtwara Mjini-CCM) afikishwe kwenye vikao vya chama ili kufunzwa uzalendo wa kusimamia maamuzi ya chama na Serikali.
Wenu,
VUTA-NKUVUTE a.k.a Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam
masters kaitoa wapi?? std VII yule, na ushahidi tunao.....Tena?mbona tuliambiwa lukuvi ana master degree'mnatuchanganya wakuu