Simbachawene: Mitambo ya Gesi Mtwara ing'olewe

Simbachawene: Mitambo ya Gesi Mtwara ing'olewe

hata msomi akiona mambo aliyoyapanga ili kijinufaisha yanakwenda mrama hutoa lugha kama hizo. rejea kauli ya pinda wakati ule wa sokomoko la dr ulimboka mkuu.

hiyo ni fact.....nimekusoma
 
Ngoja ngoja ngojea mbona mwaka huu 2013 patafahamika Na hii kitu unaambiwa Bunge halijaanza.. Ngojea lianze..
Watasingizia kuwa swala hilo liko mahakamani lisijadiliwe!
 
Mnara wa Babel(CCM) huo taratibu unaanza kudondoka, Mtu akitumwa nyundo anapeleka Shoka! wakitumwa mbao wanapeleka misumari...

CCM Wangefanya lamaana sana kwa kuwaondoa wawekezaji wote nchini...hadi wale wanaochukua Dhahabu zetu burebure kule Geita, Kahama, Singida, Nyamongo, Serengeti na Chunya...Waondoeni wote wenye kuchimba Uranium, Almasi, Tanzanite, Gesi, Nickel na hata Gypsum kule upareni...Mkimaliza waondoeni wawekezaji mliowapa vitalu vya uwindaji kwa bei chee...sababu, nia na uwezo mnao coz Wananchi wote kwa sasa ni Wahaini Kwa CCM na Serikali yake...

...mgetusaidia sana ili 2015 tuanze upya ...!!! kisha baada ya miaka 10 tuwatoe keko/ukonga mshuhudie kwa mshangao nchi ya ahadi tunayo iota kila kukicha...
Kwakuliona hilo hapo kwenye Red,jamaa wameamua kukomaa.Hao wengine si walikuwa wajinga tu. Wajinga ndiyo waliwao. Hapo ni kekundu tu.Big up machinga wamezidi kuwaonea.
 
Hiyo sasa itakuwa Sindimba! Sijui kama anaijua kuicheza. Kule Tarime ingeitwa Litingu, kazi ipo!
 
Kauli Kama hizi ndio zitawaaribu wana mtwara akili. Yani badala ya kuwaomba na kuwaelimisha yeye anawatisha? Maajabu ya muss Haya. Kwa iyo Kama wana mtwara ni waasi basi wajitangazie uhuru wao maana waziri kashawatenga na kuwaita waasi.

Hii ni hatari sana cdm nusuruni hili Jamani ccm inatupeleka pabaya
 
Suala la gesi Mtwara lisitugawe watanzania! Upande wowote usipuuzwe!!!
Tulipofikia ni pazuri! Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!
 
Jamani msimlaumu Simbawachene, kauli kama hizi hazina budi kutokea ili hata waliousingizini waamke tushirikiane kwa pamoja kuikomboa Tanzania yetu mikononi mwa wakoloni weusi!

count down towards 2015
 
Suala la gesi Mtwara lisitugawe watanzania! Upande wowote usipuuzwe!!!
Tulipofikia ni pazuri! Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!

uNA MAANA hata KILAZA na vijembe vyake asipu-uzwe?,kuwa makini ww....,acha u-poyoyo.ngoja Uranium ichotwe sumbawanga ndo ulete khadithi hizo.
 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kibakwe-CCM,George Simbachawene ametoa mpya.

Amependekeza mitambo ya kuchimba gesi asilia mkoani Mtwara ing'olewe ikiwa ni kuwaadhibu wananchi wa Mtwara aliowaita wahaini. Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Makada wa Chama cha Mapinduzi walioko Ofisi Ndogo za CCM -Lumumba Dar es Salaam, Simbachawene alisema watu wa Mtwara ni waasi na wanapaswa kushughulikiwa ipasavyo.

Mazungumzo hayo yalifuatia nia ya Makada wa CCM kutaka kupata maoni ya Naibu Waziri huyo juu ya nini hasa alijionea alipofanya ziara ya kushtukiza mkoani Mtwara. Simbachawene, bila kubana maneno, amesikika akisema: 'Cha kufanya ni kuwaamuru Wawekezaji wote waliopo katika machimbo ya gesi Mtwara kung'oa mitambo yao ili tuone kama gesi hiyo itatumika nao wananchi hao'

Katika kile kinachoonekana ni kuchoka kuoongoza kwa CCM,baadhi ya makada maarufu wa CCM akiwemo William Lukuvi,kwa nyakati tofauti leo, wameonesha kuguswa na kukubaliana na pendekezo la Simbachawene. Pia inapendekezwa kuwa Mh.Murji (Mbunge wa Mtwara Mjini-CCM) afikishwe kwenye vikao vya chama ili kufunzwa uzalendo wa kusimamia maamuzi ya chama na Serikali.

Wenu,
VUTA-NKUVUTE a.k.a Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam

Hivi tuna mawaziri wenye akili ndogo hivi........wananchi wanataka maendeleo
Kisaa yeye kuzomewa....?
 
MUNGU ibariki Tanzania na watu wake na mwisho wa maccm kutawala iwe 2014 AMINA.
 
Back
Top Bottom