Simba wana mgao kwa Samatta kwenda Aston Villa?

Kwenye kipindi cha KIPENGA EXTRA usiku huu Rage amepigiwa simu kuhusu kipengele cha Simba kupata % .
Amesema ni kweli kipindi wanamuuza kwenda TP MAZEMBE walisaini kipengele hicho.
Yaani kila Samatta anapohama timu Simba wanapata 20% yao... Ila akasema hajui kama UONGOZI mpya ulisimamia vzr kipengele hicho au walifanya ujanjaujanja.
 
General Mangi uko sahihi, Genk watalipa 10% kwa Tp Mazembe, Nao Tp Mazembe watatoa 10% ya kiasi walichopewa na Genk. Kwa hiyo hapo ni sawa na asilimia 1% , ambayo ni milioni 23( hapo bado kodi haijakatwa) hivyo ndio hesabu inavyokwenda kama hicho kipengele cha 10% kipo.
Utakuwa ulifeli hesabu wewe bila shaka.
 
General Mangi uko sahihi, Genk watalipa 10% kwa Tp Mazembe, Nao Tp Mazembe watatoa 10% ya kiasi walichopewa na Genk. Kwa hiyo hapo ni sawa na asilimia 1% , ambayo ni milioni 23( hapo bado kodi haijakatwa) hivyo ndio hesabu inavyokwenda kama hicho kipengele cha 10% kipo.
Kurukaruka koote huko kumbe mweupe kwa hesabu? Ngoja nikusaidie iwapo asilimia ulizotoa ni sahihi.

Kama Genk wakilipwa bilioni 30, inamaana 10% watakayowalipa Mazembe ni bilion 3. Na kama Mazembe watalazimika kuilipa Simba asilimia 10% ya walichokipata kama ulivyodai, basi itakuwa million 300. Siku nyingine utulie, uache kukurupuka.
 
Kwa mkataba upi? Simba issue yake iliishia kwa TP Mazembe
Kweli bhana, siona namna Simba itakavyoweza kupeleka madai Genk au Aston Villa kwakuwa Simba haina mkataba na Genk. Labda kama Simba ingekuwa na mkataba na mchezaji mwenyewe. Tuache kudanganyana hapa.

Kwahiyo Aston Villa ikimuuza Man U Simba inapata mgao, na Man U wakimuuza Real Madrid Simba wamo tena! !! Kufikilia hivyo ni uvivu wa kufikiri
 
Wewe ndio hutaki kuelewa hicho kipengele kilielezewa toka mbwana anaenda mazembe kuwa mara zote atakazouzwa simba wana mgao, nikwambie tu mimi sio simba fan
Ha ha ha unachekesha. Walikubaliana na Mazembe popote watapomuuza watakatiwa sehemu ya dau hilo siyo kila atapokuwa anauzwa
 
inategemea na mkataba walioingia ingawa Rage anadai waliweka hicho kipengele ila cha kusikitisha nikauli yaTry again anadai Samatta alipohamia Genk walipaswa kulipwa euro laki moja lakini mazembe waliwafanyia uhuni wakawalipa $50000 huu ni uzembe wamakusudi
 
General Mangi uko sahihi, Genk watalipa 10% kwa Tp Mazembe, Nao Tp Mazembe watatoa 10% ya kiasi walichopewa na Genk. Kwa hiyo hapo ni sawa na asilimia 1% , ambayo ni milioni 23( hapo bado kodi haijakatwa) hivyo ndio hesabu inavyokwenda kama hicho kipengele cha 10% kipo.
Haya CEO kamaliza ubishi wenu.

IMG_20200119_083300.png
 
Mzee usibishe vitu usivyovijua wakati samata anauzwa Genk hao Genk walipewa taarifa kuwa kunakipengele hicho, kwa taarifa yako mazembe ndio hawana mgao hapo
Simba atamdai nani hapo kwa kipengele feki cha mkataba kati ya mazembe na simba? Inawezekana mazembe walikubaliana na hiko kipengele lakini sina uhakika na Genk na Aston Villa? na sina uhakika kama Genk na Aston villa wamewahi kuuona mkataba wa kati ya Simba na TP
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom