Simba wana mgao kwa Samatta kwenda Aston Villa?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Kuna mpango wa Simba kutakiwa kuidai Aston Villa hela ya uhamisho wa Mbwana Samatta kutoka Genk kwenda Aston Villa kwa mujibu wa Aden Rage.

Sheria za uhamisho wa wachezaji zinaruhusu Simba kudai hela Aston Villa?
 
Ngoja tusubiri wajuaji: ila ni kama nakumbuka vile waliwahi kupiga mshiko fulani hivi wakati samata anahamishiwa Genk kutoka mazembe
 
Tusijemharibia Samatta huko aendako kwa kutanguliza njaa zetu. Nadhani tuache figisu kijana ashindwe mwenyewe
Ishu sio kumharibia samata ishu mkataba unasemaje? Kwa nilivyosikia hapo mwanzoni kuwa kila samata anapouzwa simba ina % yake kutoka kwa timu inayopokea mzigo kwahiyo simba hawataidai AV wataenda kudai Genk
 
waswahili mmeanza mawazo ya njaa, ya kimaskini? kazi hamtaki kufanya mnataka fedha za cchuma ulete, wahay nk. Fikiria utakula vipi wewe na wanao kwa kufanya kazi sio kufikiria utapata vipi fedha za mafanikio na jitihada za mwenzako. Kama MO amejitoa sasa mnafikiria mtapata wapi za kupiga ng'o!! hampati hata shilingi
 
waswahili mmeanza mawazo ya njaa, ya kimaskini? kazi hamtaki kufanya mnataka fedha za cchuma ulete, wahay nk. Fikiria utakula vipi wewe na wanao kwa kufanya kazi sio kufikiria utapata vipi fedha za mafanikio na jitihada za mwenzako. Kama MO amejitoa sasa mnafikiria mtapata wapi za kupiga ng'o!! hampati hata shilingi
Naona juice ya miwa imekulewesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
General Mangi uko sahihi, Genk watalipa 10% kwa Tp Mazembe, Nao Tp Mazembe watatoa 10% ya kiasi walichopewa na Genk. Kwa hiyo hapo ni sawa na asilimia 1% , ambayo ni milioni 23( hapo bado kodi haijakatwa) hivyo ndio hesabu inavyokwenda kama hicho kipengele cha 10% kipo.
 
Tujuzane kidogo.

Kila kitu kinategemea na mikataba/kandarasi iliyoingiwa na club hizo kipindi cha uhamisho wa mchezaji.

Kuna kitu kinaitwa 'sale-on clause' ambacho huwekwa kwenye mikataba (sio lazima) wakati wa kuuziana wachezaji baina ta team na team. Hii huipa uwezo klabu kuwa na haki ya kupewa kiasi/asilimia kadhaa cha/za pesa kutokana na mauzo ya mchezaji waliemuuzia klabu nyingine pindi mchezaji huyo atakapouzwa hapo baadae kwenda klabu nyingine (third party)

Katika kipengele hicho lazima klabu ziafikiane conditions za ku trigger/activate clause hiyo ili kila mmoja kujiweka katika 'win-win situation'.

Kwamfano unaweza kukuta labda klabu zinakubaliana kwamba kama mchezaji akiuzwa kwa kiasi cha pesa kinachozidi labda TShs 10, 000/- basi klabu yake ya zamani watapewa asilimia 5 ya mauzo. Kama akiuzwa kwa Tshs 100, 000/- basi klabu ya zamani watapewa asilimia 10 ya mauzo. (Hiyo ni mifano tu ili tuelewane).

Conditions nyingine ni kama ranking ya league atakayouzwa. Mfano labda mchezaji akiuzwa kutoka Africa kwenda Ulaya rate ya sale on clause inaweza kuwa kubwa kuliko kama akiuzwa klabu ya Africa kwenda labda Uarabuni au hapa hapa Afrika.

Conditions zipo nyingi ikiwa ni pamoja na ku consider kuwa mchezaji anaweza asi realise potential yake hivyo thamani yake kwenye transfer market ikapungua, au akapata career ending injuries n.k. Hivyo klabu lazima pia zikubaliane kama ikitokea hivyo malipo yanaweza kutokuwepo n.k.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom