Simba vs Tiger

Wewe sio mambo yote yanayotokea uko maporini yanaweza kurekodiwa.Video zinazowekwa mitandaoni ni sehemu kidogo sana. ila kwa kiasi kikubwa watu wanaofanya kazi uko maporini wanaona mambo mengi zaidi kuliko wewe unayesubiri matukio machache yanayorekodiwa nakuwekwa kwenye mtandao.
 
Ndivyo wabongo tulivyo ndugu. ujuaji mwingi kumbe hewa tu.
 
Aise tena acha kabisa kumfananisha Simba wa Afrika na hivyo vipaka vingine vya uko asia vinavyowinda sungura.
 
Mziki wa nyati usikie tu.Simba mwenyewe kuna wakati akijichanganya vibaya inabidi arudi nyuma kujipanga upya..Sasa ukitaka ufurahi ukute tifu la simba dume bachela na nyati dume aliyejeruhiwa.Hivyo vipaka vingine vyauko ulaya na asia vingekua afrika vingekua vinawinda swala wadogo tu ila sio Nyati.
 
Aise tena acha kabisa kumfananisha Simba wa Afrika na hivyo vipaka vingine vya uko asia vinavyowinda sungura.
Bora uwaambie vijana wa YouTube. Wao wakimuona African Lions wanamlinganisha na Simba wa kwy PlayStation. Baraaa la Simba wa apa African sio mchezo. wanyama wote wa Africa ni hatari tupu, anaua mnyama mkubwa na kumvuta umbali mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani alikwambia simba dume hawindi?.Simba dume ataacha kuwinda akishapambana akapata himaya yake, hapo sasa anakua mfalme kazi yake kubwa nikulinda himaya yake yamajike na watoto isijekuvamiwa na madume wengine.Ila anapokua bachela anawinda kama kawaida na hao ndo wanakuaga wakorofi kuliko dume mwenye majike.
 
Mjadala umekuwa mkali sana ishara ya kwamba wengi tunafuatilia na tunawapenda wanyama. Ni dalili nzuri na ishara kwamba kwa hili ustawi wao utawezekana maana kama kitu unakipenda ni dhahiri kwamba utakilinda.
Tuendelee kuwapenda wanyama hasa wa porini maana ustawi wao unategemea sana upendo wetu kwao na juhudi za kuwalinda. Tuache matumizi ya bidhaa zao kama nyama, kucha, ngozi na pembe zao, tisiingilie na tusitishe shughuli za kibinadamu katika maeneo yao ya asili ila pia tuendelee kuzitembelea mbuga na mapori wanamo hifadhiwa kwani kwa kufanya hivyo sio tu itapatikana pesa ya kuendelea kuwalinda kwa waliopewa mamlaka ila pia tutaendelea kupata elimu na kuwajua zaidi na hivyo kuwa na ari ya kuguswa na kuzidi kuwapenda.
Ni viumbe muhimu sana kwenye eco system kwahiyo uwepo wao unastablize uwepo wa uhai endelevu katika ulimwengu huu.

Pamoja na hayo yote simba aka baunsa wa gym za uswazi maana kutokuwa na vifaa mahsusi vya mazoezi vinamfanya avimbe kifua tu huku chini anaisha hawezi kuchukua round kwenye fight na Tiger wakiwa one on one. Hua nikiangalia umbo la simba dume namfananisha na tonge la ugali limechomekwa kwenye kijiti cha meno😀😆😀
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…