GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,730
- 128,230
Hivi karibuni mwenendo mzima wa timu ya simba ktk ligi kuu ya vodacom umekuwa si mzuri huku tukipewa sababu lukuki za kipopoma ila kwa uchungu wangu na mapenzi kwa mnyama leo nafunguka kisawasawa na hata simba wenzangu mkinichukia poa tu.
0 % za lawama kwa ukawa
Hawa jamaa kwa ukweli nilionao na kwa uchunguzi wangu wa kimantiki hawahusiki kabisa na kwa lolote na maendeleo mabovu ya simba sports club isipokuwa wanaangushiwa tu jumba bovu ili watu au kundi fulani kukwepa lawama kwa upopoma wao.
5 % za lawama kwa benchi la ufundi
Hawa jamaa si wa kulaumiwa sana na kwa kiasi hicho kwani timu kocha mipara mipara kaikuta tu na yeye bila ya kushtuka kuwa anaingizwa mkenge na ktk lawama akakubali kuja kuifundisha huku akisahau professionalism.
Kwa upande wa captain fantastic para mwingine mzambia matola na yeye pia anaonyesha ni jinsi gani asivyojitambua kwani amesababisha makundi baina ya wachezaji na bado hajaacha tabia yake ya kupanga wachezaji kwa kupewa cha juu a.k.a ten percent.
Hiyo ni tisa ila kumi matola sasa imefikia hadi anawanunulia wachezaji viroba vya burudani wachezaji marafiki zake na kuwapelekea mazoezini na ktk mechi ya pili na ya tatu tulizocheza simba kuna baadhi ya wachezaji walikuwa wanacheza mpira huku kiwanda cha bia cha ilala mchikichini kikiwa ktk mibichwa yao.
Kwa kuwasaidieni tu mlio na mkanda wa hizo mechi za pili na tatu rudieni kuangalia kisha mtaniambia ni wachezaji gani na wangapi walikuwa wanakwepa sana kupiga mipira ya vichwa huku wakikataa kwenda ktk mipira ya kona na hata kama walikaa basi ilikuwa ni kwa kuzuga tu.
25 % za lawama kwa wachezaji wenyewe
Tutahangaika sana hapa ila ukweli ni kwamba wachezaji wa timu ya simba wanachukiana na tena kwa msiojua hali ni mbaya kwani imefikia muda mchezaji kama ramazan singano " messi " na nashangaa hajapigwa chini kama wenzie anamwonyeshea chuki tena za wazi wazi.
Mchezaji mwenzie emanuel robert okwi na hadi kufika hatua ya kumwambia au kumtamkia kuwa hatompatia pasi za kufunga magoli uwanjani. huku amri kiemba nae akipita kufanya ushawishi kwa wachezaji wenzake na hadi kuwadindia ( kuwaonyesha jeuri viongozi ) kwa kuwaambia kuwa nanukuu " nyie watoto msiwe wahovyo na msipelekwepelekwe na huyo okwi wao kwani yeye humu ktk timu anafanywa kama vile mungu mtu na yeye ni nani hadi kila safari tu apandishwe ndege huku sisi tukipakiwa ktk meli au basi utadhani mizigo iliyotoka bandarini? "
Mwisho wa kumnukuu aaamini kilemba! na si hapo bali sasa ndani ya mnyama kuna mashindano yasiyo rasmi ya kupigana miba na haswa ikiwalenga wachezaji wa kigeni tu pekee na kuna wachezaji wawili waliokuwa maarufu mno hapa bongo mmoja sasa anakalia benchi kwa wana gongo wazi atokae mkoa wa wanaogoma na mwingine yuko katika timu ya watibuatibua sugar na anatokea mkoa wa wanaotangatanga ndiyo huhusika kuwapeleka wachezaji wa sasa wa mnyama kwa sangoma ili kuwaharibu wenzao huku nia na madhumuni wao kurudishwa ktk dirisha dogo pamoja na akina nyosso na boban.
70 % za lawama kwa rais na uongozi wake mzima
kwa kuanzia tu rais aveva hakujiandaa na kuwa tayari kiukweli kuiongoza simba isipokuwa aveva alishinikizwa tu na watu fulani walio na maslahi yao klabuni. kwa msiojua ni kwamba simba haiongozwi na aveva bali aveva ni kama ufunguo tu wa gari ila waendeshaji ni wengine
( hapa nikimaanisha kwamba gari linaendeshwa na kila mtu ) na hapo hapo aveva huyu ni mwoga na anapangiwa kila kitu na mzee wa pama captain mstaafu, tajiri kigoma, meneja wake kipa maarufu mkaa benchi klabu kubwa ya mafurikoni jangwani.
lakini pia aveva huyu huyu kapanga kikosi chake cha kazi kwa kutoa fadhila pasipo kuhusisha administrative professionalism ili tu kuwaridhisha mapopoma fulani.
kwa mfano aveva huyu huyu na viongozi wenzake walipokaa kikao na wachezaji south africa aliwaahidi kuwa kuanzia sasa wachezaji wote watalipwa stahiki zao na kutakuwa na posho za kutosha sasa naomba kuuliza je kilitokea nini baada ya mechi ya yanga?
wachezaji waliahidiwa fungu la milioni 50 na uongozi kama watashinda na tsh milioni 30 kama wakitoka suluhu na matokeo yake baada ya mtanange ule tu kudadadeki kila mcheza aliyecheza kapewa tsh laki moja na wasiocheza tsh elfu hamsini ( na wachezaji takribani nane walimaliziwa pesa zao hizo juzi ktk mechi ya simba dhidi ya prison ).
anayejua hesabu vizuri naomba unipe kiasi kamili walichopewa wachezaji baada ya kutoka sare na wana mafuriko je kinakaribi au kufikia hiyo tsh milioni 30 waliohaidiwa kama wangetoka sare na gongo wazi?
kubwa kuliko na msilolijua na mimi leo nawapasulia ni kwamba sasa hivi uongozi wa simba haswa rais aveva na wenzake wamemtenga na kumbagua ktk maamuzi yote makamu wa rais kaburu kiasi cha kupelekea hadi wakubwa hao kununiana.
Tatizo ni nini? tokea mwanzo aveva hakumtaka kaburu ktk nafasi hiyo bali alimtaka mtu mwingine ( ambaye ktk tamasha la simba day la mwaka huu yeye ndiyo alikuwa mratibu mkuu na aligombea umakamu huo na akawa mshindi wa tatu bomba ). Hivyo basi sasa hivi ndani ya mnyama kuna makundi ktk uongozi a.k.a aveva original na kaburu chipolopolo! je mnategemea nini hapo?
Mechi mbili za mwanzo za simba kuna viongozi hawa wawili mmoja mpenda kuvaa mashati ya kubana ( wenyewe mnayaita mashati ya kimodo ) ambaye hupenda kufuga nywele na mpenda sifa na kimbelembele.
Nilibahatika pia kusoma nae shighatini secondary 1993 - 1994 ambaye muda wote umwonapo lazima awe amebeba simu zake mbili tatu mkononi na akining'iniza funguo za mkoko wake na mwenzake ambaye ana mguu mbovu wa kushoto ila ana vihela vyake na ni mtani wangu wa kihaya ambaye umwonapo lazima shingoni kwake utahesabu micheni ya dhahabu ya asante migomigo ( magomeni ).
Hawa walipewa jumla ya tsh milioni 20 ili kila mechi marefarii wapewe chao tsh milioni 10 na kilichotokea hapo mechi ya kwanza refa alipewa tu tsh laki 7 na kuambiwa kuwa mtandao unasumbua lakini baada ya mechi kuisha hakupewa tena chake na mechi iliyofuata refarii alipewa tsh milioni moja na laki tano ila ktk hiyo hela tsh laki tano nzima zilikuwa ni fake kitu ambacho kilipelekea marefarii hao kuitishana kikao na kukubaliana kuwa sasa mwendo ni kulipiza kisasi kwa mnyama kitu ambacho wamefanikiwa kwa 100 %.
ukweli mtupu ndiyo huu na najua nitachukiwa na kununiwa sana ila poa tu..............nawasilisha.