Inasikitisha dunia ya leo watanzania bado wanaamini uchawi na wengine wanadiriki hata kusema wazi kwenye tv na radio eti ukawa ndio wanasababisha simba ipate sare. Hao ukawa mnawapaisha bure si walikuwepo mwaka jana wakati simba inafungwa hovyo na kupata droo za kutosha mbona hawakuzuia hayo matokeo. Tatizo la simba wachezaji hawana umoja kwa sababu wengine wanapendelewa na wenzao wanaona. Ni kichekesho cha hali ya juu mfungaji bora wa mwaka jana kulipwa mshahara nusu ya mshahara anaolipwa okwi. Mwakani akienda yanga/azam tumlaumu nani. Haya ya okwi yalishatokea enzi za elisha john akiwa yanga zamani wachezaji wote waliku wanamuacha azunguke uwanja mzima mwenyewe kutokana tofauti ya mshahara.