Simba (Tanzania) vs Ahli Shandy (Sudan)

Hongereni sana SImba Tanzania kwa kuwapa watanzania raha, matokeo mazuri sana hayo
 

Hongera sana kwa kuweka unazi pembeni na kutanguliza utaifa. wewe kama mimi, kwani mimi ni mnyama damu lkn ktk mechi za kimataifa siku zote nasapoti timu za Tanzania hata Yanga. Mimi kwangu uzalendo mbele.
 
Hongere sana Mnyama Kwa ushindi mtamu. Zitto 25 (a.k.a Okwi) nakufagilia sana umenipa raha kwa goli la tatu. Pokea busu langu Mwaa mwaa mwaa
 
Asanteni Sana maana hapa nipo ku pori MayaMaya. Kondoa Jamii Forums kiboko iko siku na sisi tutaona Live kwenye Mobile huyo Zito na jezi yake 25
SIMBA 3.- Ahly Sudan 0
 
66,77,88 dakika ambazo al alhly shendi hawawezi kuzisahau

hii ni nadra sana kutokea katika soka. Hii kwa utabiri wa kinyota na bahati inawapa nafasi nzuri tena ya kufika mbali katika mashindano haya timu ya simba.

NAMBA YA BAHATI (6+6+7+7+8+8=42=4+2=6) KWA SIMBA NI 6 (s-perfect number). Namba hii kwa vile huunda na namba 1,2 na 3 inaashiria kuwa Simba katika mashindano haya itakuwa na uwezo wa kufunga kati ya goli 1, 2, 3 au 6 katika michezo yao yote. Ukifuatilia mechi zao za nyuma ndivyo alivyokuwa. Namba 6 huashiria furaha hivyo kila mechi simba watakayocheza tutegemea furaha kutoka kwao.
 
Simba juu, juu, juu zaidi.

Wanastahili kila sifa kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania ipasavyo.
 
Hahaha yani kwao hadi waje washnde zaid ya hizo sie tumesimama tu loh. Ahsante Mungu
 
Ushindi halali kabisa, vijana wamecheza. Nimependa hii dk ya 66 bao la kwanza, dk ya 77 la pili na dk ya 88 la tatu.
 

Bala, kumbe upo Mkuu, nlikuwa sijiakuona, nimeamini kuwa wewe u mzalendo halisi.
 
Simba kumbukeni kuwa mkitwaa ubingwa wa CAF mtawasaidia Yanga kupata nafasi ya kushiriki michezo ya CAF, kwani nyie Simba mtashiriki kama bingwa mtetezi. Hili ndilo dua langu......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…