Simba SC yamfukuza kazi kocha wake Logarusic

Simba SC yamfukuza kazi kocha wake Logarusic

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,393
Kufuatia klabu ya simba kufanya usajili wa pesa nyingi na timu kuonyesha kiwango duni kwenye mechi ya jana na kupata kipigo cha goli 3 kwa bila , uongozi wa klabu umechukua uamuzi mgumu wa kusitisha mkataba wa loga



SIMBA SC imevunja Mkataba na kocha wake, Mcroarta Zdravko Logarusic siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Rais wa Simba SC, Evans Aveva amesema kwamba Logarusic amevunjiwa Mkataba kwa kukiuka masharti ya mwajiri wake na sasa Nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama' aliyekuwa Msaidizi wa Loga, ndiye anakuwa kaimu kocha Mkuu hadi atakapopatikana mwalimu mwingine.

[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]
Kibarua kimeota magugu; Zdravko Logarusic amefukuzwa Simba SC baada ya miezi 10
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kinidhamu na kikubwa ni kuwatolea maneno yasiyofaa wachezaji.

Inaelezwa Loga alifikia hatua ya kuwadharau na kuwatolea maneno yasiyofaa hadi viongozi wa klabu hiyo.
Loga anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.

Loga aliyerithi mikoba ya Mfaransa, Patrick Liewig aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.


 
Soka la kimaigizo la wabongo sijui litaisha lini?.
 
Kufuatia klabu ya simba kufanya usajili wa pesa nyingi na timu kuonyesha kiwango duni kwenye mechi ya jana na kupata kipigo cha goli 3 kwa bila , uongozi wa klabu umechukua uamuzi mgumu wa kusitisha mkataba wa loga

timu za ovyo kabisa hizi yaani mechi ya kirafiki iwe hivyo? shame on you simba sc
 
Simba wajinga mechi moja unafukuza kocha hii timu ya majuha.
 
Kufuatia klabu ya simba kufanya usajili wa pesa nyingi na timu kuonyesha kiwango duni kwenye mechi ya jana na kupata kipigo cha goli 3 kwa bila , uongozi wa klabu umechukua uamuzi mgumu wa kusitisha mkataba wa loga
simba nayo timu? siku hizi ni yanga, azam na mbeya city tu. wengine tulishawasahau kama wana exist!
 
Hii habari ina ukweli?? Source please....!!
 
Kama ni kweli basi watakuwa mazoba sana mechi moja tu unamfukuza
 
kikao kiliitishwa cha dharura na mwenyekiti wa club na kuudhuliwa na wajumbe
 
Mwenye kasababisha alienda kutukana wachezaji.
 
Hii kali man city kapigwa tatu leo na watu wanaendelea kama kawaida.hizi ngozi nyeusi kama tuna laana.simba hawatapata kocha tena kama huyu.manchester walikuwa wanamtaka huyu.

makocha wazuri wapo wengi na atapatikana mwingine zaidi ya loga
 
Tangu simba imfanyie fitina wambura siipendi tena, natamani wafungwe mechi zote. Wameacha kuzingatia misingi ya mpira wanatamani madaraka ili tu wawafukuze wale wenye fikira tofauti na wao watafune mali za klabu. Shame on you msimbaziz
 
Ni kweli kabisa kocha kafukuzwa.......source nyingine ni michezo radio one.
 
Simba walipaswa kujua kwamba mwendawazimu haponi, hupata nafuu tu. Kosa linlosemekana limemfukuzisha kocha ni kutukana watu, hasa baada ya mechi. Alikwishafanya hivyo msimu uliopita na kulalamikiwa na wachezaji. Lakini uongozi ukawabeza kwa kuwa uliamini ndivyo nidhamu kwa wachezaji invyojengwa. Inasemekana mara hii kibao kiliwageukia hadi viongozi wenyewe! Tabia ni ngozi, kuivua huiwezi! Ni uamuzi mzuri, lakini ulipaswa kuchukuliwa kwa kutomsajili tangu mwanzoni. Wacha 'taulo' Kibadeni arudi kuwafuta jasho!
 
Back
Top Bottom