Simba SC Vs Coastal Union (2-0)| Simba yatwaa Ubingwa msimu wa 2020/21

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL, Kuendelea kupigwa leo July 11, 2021 ambapo Mnyama Mkali, Simba SC, wanawakabili Wagosi wa Kaya, Coastal Union, kunako Dimba la Mkapa Jiji Dar es salaam.

Mchezo ni mgumu kwa pande zote mbili, kwani Simba SC inasaka alama tatu au sare ili kuweza kutangaza Ubingwa wa (VPL) 2020/21 kwa mara ya Nne Mfululizo huku Coastal Union wakihitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka sehemu salama kuepuka mstari wa kushuka daraja.

Simba SC yenye alama 76, kama itashinda mchezo wa leo itafikisha alama 79 na kama itatoka sare itakuwa na alama 77 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ikiwemo Yanga SC iliyopo nafasi ya pili kwa alama 70 ambapo kama itashinda mechi zao mbili zilizobaki watafikisha alama 76.

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola, amesema kuwa wajiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi.

"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi. Tunawaheshimu Coastal Union ni timu nzuri lakini tumejipanga kesho (leo), kutangazwa kuwa mabingwa". Amesema Matola

Naye Kocha Msaidizi wa Coastal Union Joseph Lazaro, amesema kuwa wamekuja kwa tofauti kabisa kwenye mchezo wa leo ili kujinusuru na kushuka daraja.

"Tumekuja kivingine tofauti na mechi nyingine, tumekuja kupambana dhidi ya Simba SC ili kujinusuru kutoka sehemu mbaya tulizopo". Amesema Lazaro

Nani kuibuka kidedea? Dakika 90 za jasho na damu kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

....... Ghazwat....Na Jopo la JF.....

==========

Mwamuzi yupo katikati ya dimba tayari kupuliza kipyenga kuashiria kuanza kwa mchezo.

00' Naaaam mpira umeanza ni dakika 90 za Wanaume hawa kupambana | Simba SC 0-0 Coastal Union.

05' Simba SC wanajipinga kujaribu kupata nafasi huku wakiusoma mchezo wa Coastal.

13' Bocco Goooooooooooooaaal Goooooooooaaal.
John Bocco anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa Free Kick | Simba SC 1-0 Coastal Union.

18' Shuti la mbali la Abushehe linatoka nje ya lango la Simba SC huku Umiliki wa mpira uko upande wa Simba.

23' Mugalu Goooooooooaaal Goooooooaaal

Kope Mutshimba Mugalu anaipatia Simba SC bao la pili, akimzunguka golikipa wa Coastal | Simba SC 2-0 Coastal Union.

Coastal wanafanya jaribu, lakini Defense ya Simba chini Ame wanaokoa hatari ile.

35' Simba SC wapo mbele kwa mabao mawili, huku Coastal wakijaribu kutafuta bao la kwanza, huku mashambulizi yakiendelea.

40' Coastal mbinu zao za kupenya gome ya Simba SC inadunda huku Simba kupitia kwa Mugalu na Miquissone wakipoteza nafasi bomba za kufunga.

45+1' Kuelekea kuwa mapumziko Dimba la Mkapa

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wanaongoza kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Coastal Union. | HT, VPL: Simba SC 2-0 Coastal Union.

Kipindi cha pili kimeanza huku kukiwa hakuna mabadiliko. Je Coastal watafanya maajabu?

50' Simba SC wameanza kama dakika za kipindi cha kwanza, mashambulizi kadhaa kuelekea lango la Coastal huku Coastal wakijilinda

56' Ametoka Bocco na ameingia Kagere upande wa Simba SC | Simba SC 2-0 Coastal Union.

Mashambulizi kadhaa wakishambulia Coastal lakini hayajazaa matunda, hata hivyo kwa sasa mbinu za kujilinda zimeongezeka.

Mabadiliko...Mudathir ameingia upande wa Coastal na Ndemla upande wa Simba SC.

70' Coastal wapo imara kipindi hiki cha pili kwa kuzuia mashambulizi makali ya Simba huku | Simba SC 2-0 Coastal Union.

77' Ametoka Mugalu na ameingia Dilunga upande wa Simba SC huku Simba wakikosa nafasi ya kufunga baada golikipa Abbas kucheza shuti la Miquissone.

85' Pomoja na kumiliki zaidi mpira lakini Simba wanashindwa kuongeza bao. Coastal matumaini ya kusawazisha mabao yakitoweka

89' Simba SC wanapoteza nafasi mbili za wazi kufunga, kupitia kwa Kagere na Bwalya, dakika chache kuanzia sasa mpira utakwisha

90+2' Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wamepata ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Coastal Union.

Hivyo Simba SC kwa ushindi wa leo wameutwaa Ubingwa wa nne mfululizo kwa kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na Timu yoyote.

FT, VPL; Simba SC 2-0 Coastal Union

... Ghazwat...
 
Ubingwa VPL Upo Mlangoni Ni Muda Tu
simbasctanzania_20210711_151552_0.jpg
 
Coastal union inashuka Daraja msimu huu.

Kosa walilofanya Coastal ni kukubali kudhaminiwa na GSM na kumtoa Mwamyeto kwenda Yanga, hivyo wanajikuta wanavunja undugu na Simba.

Kilichowakuta Singida united na Toto Africa ndio kinaenda kuikuta hii timu ya Rais Karia.
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL, Kuendelea kupigwa leo July 11, 2021 ambapo Mnyama Mkali, Simba SC, wanawakabili Wagosi wa Kaya, Coastal Union, kunako Dimba la Mkapa Jiji Dar es salaam.

Mchezo ni mgumu kwa pande zote mbili, kwani Simba SC inasaka alama tatu au sare ili kuweza kutangaza Ubingwa wa (VPL) 2020/21 kwa mara ya Nne Mfululizo huku Coastal Union wakihitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka sehemu salama kuepuka mstari wa kushuka daraja.

Simba SC yenye alama 76, kama itashinda mchezo wa leo itafikisha alama 79 na kama itatoka sare itakuwa na alama 77 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ikiwemo Yanga SC iliyopo nafasi ya pili kwa alama 70 ambapo kama itashinda mechi zao mbili zilizobaki watafikisha alama 76.

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola, amesema kuwa wajiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi.

"Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kupata ushindi. Tunawaheshimu Coastal Union ni timu nzuri lakini tumejipanga kesho (leo), kutangazwa kuwa mabingwa". Amesema Matola

Naye Kocha Msaidizi wa Coastal Union Joseph Lazaro, amesema kuwa wamekuja kwa tofauti kabisa kwenye mchezo wa leo ili kujinusuru na kushuka daraja.

"Tumekuja kivingine tofauti na mechi nyingine, tumekuja kupambana dhidi ya Simba SC ili kujinusuru kutoka sehemu mbaya tulizopo". Amesema Lazaro

Nani kuibuka kidedea? Dakika 90 za jasho na damu kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

....... Ghazwat....Na Jopo la JF.....
Probably 1st 11 ya Simba
Ally Salim
David kameta
Gadiel
Ame
Onyango
Tadeo
Ndemla
Miraji
Kondeboy
Bocco
Kagere
 
Back
Top Bottom