SIMBA SC mnaua timu kwa kuendekeza ushikaji

SIMBA SC mnaua timu kwa kuendekeza ushikaji

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
8,548
Reaction score
17,246
Wakuu habari.

Moja ya shida kubwa inatugharimu sisi wanazi wa Simba kukosa furaha na timu yetu kutoeleweka ni kutokana mambo ya kuendekeza ushikaji na huruma za kipuuzi. Mfano zaidi ya misimu minne timu haijawahi kufanya usafi wa uongozi pale juu ,matokeo yake tunaenda na mbinu na mikakati ile ile kila siku mwisho tunabaki kulingia historia.

SELEMANI MATOLA kila mwaka yeye kocha msaidizi tu wanakuja makocha na kuondoka wanamkuta na kumuacha position ile ile, sidhani kama makocha wanaokuja wanaelewana falsafa na huyu bwana sioni ulazima wa Lunyasi kufanya hivyo imekua sasa kama desturi kila kocha akija analazimishwa kupewa msaidizi.

TRY AGAIN huyu nae mtu mwingine miaka nenda miaka rudi yuko pale atatolewa miezi miwili atarudishwa tena yaani vurugu tu.

MAGORI nae kama try again miaka inaenda na kurudi utamkuta pale pale na wengine .

SKAUTI yule mzungu nae amekua anatupiga miaka na miaka tunamchekea tu kisa mzungu.

Kila siku Wajumbe wa Bodi ni wale wale India toka ila watu wale wale kulikoni na walishafeli ?

Hata huyu tajiri yetu MO DEWJI nae siwezi mtetea tena ni moja ya watu wanaokwamisha timu kuendekeza ushikaji na urafiki uliopitiliza na maneno ya uswahili uswahili. Atateua watu wale wale wanaofelisha timu halafu atakuja hadharani anasema anapata hasara wakati timu imejaa matangazo yake kibao kwa malipo ya buku jero.

Tumekua tunatabirika sana kua atakuja kocha msimu mmoja atafukuzwa kisha MATOLA NA MGUNDA watapewa timu watu wanatafuna 10% zao maisha yanaendelea.

Sasa ona kwa Vyura wao wana👇
HERSI SAIDI huyu jamaa atatusumbua sana acheki na kima ,Sio vibaya kuiga mambo mazuri kwa watani wetu wao timu yao wamekomesha ushikaji ndo maana leo husikii migogoro kila mtu atafanya kazi akiwa na uwezo hawataki ushikaji na ukianza kuwavuruga wanakupiga chini haraka na leo imekua timu tishio Ndani na Nje ya nchi. Ndo maana timu nyingi zinakuja kujifunza uongozi kwa huyu jamaa. Wenzetu hata makoxha wakileta hawalazimishi lazima awe na fulani kwenye benchi na hawana huu upuuzi kulazimisha watu wale wale waliofeli.

SHABIKI LIA LIA WA LUNYASI,ALAMSIKI
 
Tuwe na shukrani! Haya, ndiyo aliyoyasema yule Mwamba, kuwa mtu kavimbiwa mihogo yake huko, anakuja kutapika hapa! Hivi huyo mtoa hela, tunafikiri yeye haumii kwa kuchoma pesa tu, bila sisi mashabiki kupata raha?
Sumu HAIONJWI!
 
Inakera Sana ila Simba day mlifanya kitu cha kukumbukwa.
 
Back
Top Bottom