Simba SC kamwe haiwezi kuiombea dua jema Yanga

Simba SC kamwe haiwezi kuiombea dua jema Yanga

Nasikia mnaitwa kilimo kwanza. Ushafyeka sehemu yako bunju?

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
.....Wanasahau walivyohamasishana kununua kwa maelfu jezi la TP Mazembe mpaka leo zimezagaa jijini... leo wanaomba dua za Watanzania... :rofl:

wapigwe tu.
 
Ukiomba dua mbaya ndiyo wanafanya vizuri, pole sana, hata mchezo wa awali wa Yanga na Al-Ahily Simba walijifanya kuwachukua wapenzi wake ili wakafyeke bunju eti wajenge uwanja ndani ya suku 100, mradi tu wasiende uwanjani, kiwanja cha mpira kijengwe kwa siku 100? Labda cha makuti, duwa yao ikagonga mwamba mapato 484M na ushindi juu, Yanga ikapata 232M Simba ikaambulia 4M mbeya, ndiyo maana mishahara hakuna Simba.

hilo ndo tatizo lenu,ndomana huwa tunawapiga 5-0.sasa pitch huwezi kuandaa kwa siku 100 hata wewe?mapato hutokana na aina ya mechi,HAMTAWATOA WARABU NYIE.Mtapigwa 2-0 utaona.
 
Dua la kuku halimpati mwewe, endelea kuota hivyohivyo. Mlianzia kuwanga hapa na tukawaonyesha kazi yaani siku ile tulizifunga timu mbili, mkiwemo simba.

Yani goli la kubahatisha la canavaro?hivi canavaro ana magoli mangapi toka ajiunge na yanga?ile ni bahati nasibu tu ambayo haitajirudia,profesheno straika walishindwa kufunga Dar,wataweza misri bantu lady?
 
Yanga wanafungwa 2-0,wakija nyumbani mnyama nae anajipigia kama ilivyo ada.
 
Warabu full fitina. Yanga mkichomoka leo, mganga wenu mumnunulie V8.
 
Warabu full fitina. Yanga mkichomoka leo, mganga wenu mumnunulie V8.

Simba mmepigwa fine laki tano kwa uchawi! Na safi hii Simba ilivyo mbovu + wachezaji wana njaa hakuna mshahara wataanza kupigwa na Azam 4 - 0 na siku hiyo ulinzi mpaka jukwaani sijui mtang'oaje viti. mkikutana wa wazee wa Uturuki mtakula wiki qudalaleki.
 
Yani goli la kubahatisha la canavaro?hivi canavaro ana magoli mangapi toka ajiunge na yanga?ile ni bahati nasibu tu ambayo haitajirudia,profesheno straika walishindwa kufunga Dar,wataweza misri bantu lady?

Mpira dakika 90 sawa acha kupiga mayowe pixel wacha mjionee wenyewe.
Kama tuliweza kuwapiga home hapa, tutashindwaje kwao. Tena timu imeenda ikiwa na kujiamini hii tayari ni silaha, hawataogopa na watacheza kufa na kupona kuleta ushindi home. Mungu ibariki Yanga.
 
baada ya dkk 90 leo naomba uje hapa jamvini u confess,mimi pia nitarudi hapa.
 
baada ya dkk 90 leo naomba uje hapa jamvini u confess,mimi pia nitarudi hapa.

Sina tatizo la kurudi hapa baada ya mpira. Ndio maana nikakwambia mpira ni dakika 90. Lolote laweza kutokea ila sisi wenye mapenzi na Yanga tunaiombea ushindi, ndicho tunachohitaji. Hata ikifungwa bado ni timu yetu na nitaipenda mpaka mwisho wangu.
 
......... Kwa kweli Yanga kiboko kumbe hamhitaji dua za wa TZ !!!!!!

Yanga na Simba ni bora Zibinafusishwe tu ziwe Kama Azamu Hakuna wanachama tuwe na Mfumo Digtal ktk Soka Maana huu mfumo Analogia wa Wanachama Kuwa na Sauti umechangia kudidimiza Soka la Tz hata mechi za kimataifa baadhi ya wanachama hutumika Kuwa mamluki baada ya kupokea vijecent na kuzihujumu Timu zao hii Dua za Yanga au Simba hazina Nafasi ktk Soka la sasa kwani watu hawataki maendeleo pasipo migogoro Timu ziwe na Viwanja vyao Miladi Yao Timu zisitegemee mapato ya mlangoni ili kujiendesha iwepo kamati za mipango ya maendeleo kwa vitendo Haya Ndio wapenzi wa soka Tunayataka Lakini kinyume na hapo Wanachama wataendelea kuziyumbisha hz Timu kwa Migogoro isiyokwisha na kuendekeza Dua za kuku .
 
Tokea 1936 hadi Leo Timu hazima Viwanja vyao bora hii ni aibu kubwa
 
Simba mmepigwa fine laki tano kwa uchawi! Na safi hii Simba ilivyo mbovu + wachezaji wana njaa hakuna mshahara wataanza kupigwa na Azam 4 - 0 na siku hiyo ulinzi mpaka jukwaani sijui mtang'oaje viti. mkikutana wa wazee wa Uturuki mtakula wiki qudalaleki.

Hizi imani za kishirikina za kusaka Ushindi nje ya Uwanja ndizo zimesababisha hata Timu ya Taifa Kuwa Dhaifu kwani Mchezaji Akiwa Simba au Yanga anazoea kurahihishiwa kazi kwa kununulia mechi matokeo yake anabweteka na kutojituma Mazoezini kisha mechi za kimaraifa wanachemsha kwani huko Hakuna magumashi
 
Sina tatizo la kurudi hapa baada ya mpira. Ndio maana nikakwambia mpira ni dakika 90. Lolote laweza kutokea ila sisi wenye mapenzi na Yanga tunaiombea ushindi, ndicho tunachohitaji. Hata ikifungwa bado ni timu yetu na nitaipenda mpaka mwisho wangu.

sawa,mimi naomba mfungwe tu.nitafurahi iwapo ombi langu litafanikiwa.
 
Yanga baba lao, mwarabu leo hatoki hata muombe dua mbaya au musiombe hiyo ni juu yenu...YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO!.
 
Tambue Kuwa Makao makuu ya CUF yapo hapo Cairo na wakati wa kupanga Ratiba Timu za club bingwa Africa huwa wanaombea wapangwe na Timu za Tanzania kwani ni Vibonde wao Tokea Nchi ya Tz inapata Uhuru japo Simba aliwahi kufurukuta Mara moja akawafunga kwa penati Lakini Timu ya Taifa yaani Taifa Starz ni Kibonde number one wa Timu ya Taifa ya Misri kiasa kwamba hata wakiamshwa usingizini wataifunga Taifa starz tu . Yatupasa sasa tuukatae huu Uteja wa vilabu vya Misri kwa kuwafunga na kuweka Historia kubwa barani Afrika
 
Back
Top Bottom