SI KWELI Simba SC itacheza mechi ya kirafiki Oktoba 29, 2025

SI KWELI Simba SC itacheza mechi ya kirafiki Oktoba 29, 2025

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1

1761377784122.png


 
Tunachokijua
Ipo video inayotajwa kuwa ni habari za ITV iliyochapishwa na danger_t4 katika mtandao wa TikTok ikieleza kuwa Klabu ya Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Barcelona tarehe 29, Oktoba 2025 ambapo imetazamwa na watu zaidi ya laki moja, huku katika sehemu ya maoni mtumiaji wa mtandao huo akiandika "wewe sister we kweli akili imerud unaelewa unacho kizungumza.

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidijitali umebaini kuwa video hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa Akili Unde, pia ina nembo ya 'Sora' teknolojia ya akili unde iliyotumika kutengeneza video hiyo.

Aidha video ina mapungufu mengi ambayo yanakinzana na uhalisia, mosi kukosewa kwa nembo ya Simba SC, pili matumizi tofauti ya grafiki na kituo cha televisheni cha ITV, tatu tiketi za mechi haziuzwi kupitia tovuti ya ITV TANZANIA

Kadhalika timu ya Simba SC Okoba 26 inatarajiwa kucheza michezo wake wa pili wa kufuzu hatua ya makundi kombe la mabingwa barani Afrika dhidi ya Nsingizini Hotspurs na haina ratiba ya kucheza mechi ya kirafiki Oktoba 29, 2025 kama ilivyoelezwa katika video hiyo.​
Back
Top Bottom