Simba sc haoooo uturuki

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
SIMBA SC HAOOOO UTURUKI



VIONGOZI wa klabu ya soka ya Simba wanatarajiwa kwenda nchini uturuki kwa ajili ya kumalizia taratibu za ujenzi wa uwanja wake mpya wa kisasa uliopo Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.


Kampuni ya Petroland ya huko ndiyo imepata tenda ya kujenga uwanja huo ambao pindi utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchuakua watazamaji 60,000 walioketi, pia utakuwa na kumbi za burudani, hoteli, mikutano, maduka, vituo vya michezo n.k.



Awali wawakilishi wa Petroland walikuja nchini kwa ajili ya kufanya tathmini ya uwanja huo ambao unatarajiwa kugharimu bilioni 75 za Kitanzania pindi utakapomalizika.
 
Manake utakuwa na capacity kama ya huu wa taifa basi utakuwa mkubwa sana big up simba make It happen mtupe raha watanzania
 
Watazamaji 60,000? una uhakika kweli... taarifa za mwanzo hajikutaja idadi hiyo
 
ni miaka miiingi sana hizi porojo nazisikia si simba tu hata yanga nao porooojo tu. ila naomba iwe kweli itawafanya yanga nao wachangamke! kila la kheri wana wa msimbazi!
 
SIMBA SC HAOOOO UTURUKI VIONGOZI wa klabu ya soka ya Simba wanatarajiwa kwenda nchini uturuki kwa ajili ya kumalizia taratibu za ujenzi wa uwanja wake mpya wa kisasa uliopo Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.Kampuni ya Petroland ya huko ndiyo imepata tenda ya kujenga uwanja huo ambao pindi utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchuakua watazamaji 60,000 walioketi, pia utakuwa na kumbi za burudani, hoteli, mikutano, maduka, vituo vya michezo n.k.Awali wawakilishi wa Petroland walikuja nchini kwa ajili ya kufanya tathmini ya uwanja huo ambao unatarajiwa kugharimu bilioni 75 za Kitanzania pindi utakapomalizika.
me huwa najiuliza swali moja tu,vip hizo pesa za ujenzi zitatoka wapi??
 
Hivi bado mnaweweseka na kile kipigo tulichowapa ee? Acheni kutuchanganya kwani ungesema viongozi wa simba haoo uturuki si ungeeleweka tu.
 
me huwa najiuliza swali moja tu,vip hizo pesa za ujenzi zitatoka wapi??

Arsenal mpaka leo wana deni la EMIRATES sembuse Simba!!! Unataka ujue zinatoka wapi ili iweje? Hata kwa kukopa simba ilipe miaka 15 poa Ndala bakini na wenu wa jangwani pale.
 
Arsenal mpaka leo wana deni la EMIRATES sembuse Simba!!! Unataka ujue zinatoka wapi ili iweje? Hata kwa kukopa simba ilipe miaka 15 poa Ndala bakini na wenu wa jangwani pale.
kaka me ni simba 'damu' nitake radhi tafadhali kwa kunifananisha na hao magamba,kandambili...nilitaka kufahamu michakato ya pesa make honestly...klabu independently haiwez ku afford!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom