Simba SC 2-1 Azam FC | Ligi kuu NBC | Benjamin Mkapa

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Happy New Year Kwa Jamii Sports Members Wote ! Salamu za Mwaka Mpya Ziwe nanyi Popote Pale Mlipo Katika Dunia Hii Ambayo ni Sayari Ya 3

Katika NBC Premier League, leo tunauanza mwaka mpya wa 2022 kwa mzizima derby ni Simba Sc dhidi ya Azam FC

Mechi hi itapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.

KATIKA MZIZIMA DERBY

Azam FC haijapata ushindi wowote mbele ya Simba kwenye ligi kuu tangu msimu wa 2017/18, wakati Simba ikishinda mechi nne na kutoka sare mechi nne. Katika mashindano mengine nje ya ligi kuu tangu msimu wa 2017/18, Simba na Azam wamekutana mara tano, Azam ikishinda mara mbili na Simba ikishinda mara tatu. LEO wanakutana katika mchezo wa 14 kwenye mshindano yote tangu msimu wa 2017/18, Simba
ikiwa imeshinda michezo saba NA Azam ikishinda michezo miwili.

Je, nini kitatokea Leo?

Je, ni mnyama SimbaSC ama AzamFC nani kuondoka na alama 3?

Tuwe hapa Kufuatilia Mubashara kwa Dakika 90

Update

Vikosi vya Timu zote Mbili vimetoka

View attachment 2065320View attachment 2065324

=============

01' Mpira umeanza kwa kasi sana uwanja wa Benjamin Mkapa

09' 🟡Zulu anapewa kadi ya njano

12' Penaaalt, Domayo anamchezea ndivyo sivyo Sakho ndani ya 18

14' Bwalya anashindwa kuweka ndani mkwaju wa penalt, Ahmed Ali anaudaka barabara. Simba 0-0 Azam

17' Azam wanapata kona, Sebo anagonga kichwa na kutoka nje ya lango la Simba

20' Almanusura Sakho aiandikie Simba bao la kwanza, shuti lake kali kutoka nje ya 18 linagonga mwamba na kurudi ndani

28' Azam wanapata kona kuelekea Simba, inashindwa kuzaa matunda

28' Inonga yuko chini msuli ukiwa umekaza

33' Simba wanapata kona ya pili ya mchezo, Ahmed Ali anauficha mpira mikononi.

35' 🟡Onyango analambwa kadi ya njano

43' Sakho anaangushwa nje kidogo ya 18, mlingoti unawatendea wema Azam kwa mara nyingine kwa mpira kugonga mwamba

45+2' Mpira mapumziko

45' Mpira umerejea na Azam wanaanza kwa kupata kona ambayo haijazaa matunda

48' Simba wanapata kona, mlinda mlango anakaa barabara na kudaka

50' Paul Katema anapiga shuti kuelekea lango la simba na linapaa juu

58' Chilunda anaingia kuchukua nafasi ya Mudathiri, Rodgers anachukua nafasi ya Idriss kwa upande wa Azam

65' Sakho anajaribu na Ahmed Ali anauficha tena mikonini

65' Kagera anaenda nje, Mugalu anachuku nafasi yake. Bwalya nae anakwenda nje

66' 🟡Wadada anapewa kadi ya njano

67' ⚽ Sadio Kanoute anaiandikia Simba bao la kwanza kwa mpira wa kichwa, free kick kutoka kwa Zimbwe

72' ⚽Sakhooooo anaiwekea Simba bao la pili, Simba 2-0 Azam

79' ⚽Goli safi kutoka kwa Rodgers Kola, akituliza mpira kifuani na kutandika shuti huku Manula akijinyoosha mpaka mwisho

90+4' Simba wanaanza na ushindi 2022, mpira umekwisha uwanja wa Benjamin Mkapa
 
Happy New Year Kwa Jamii Sports Members Wote ! Salamu za Mwaka Mpya Ziwe nanyi Popote Pale Mlipo Katika Dunia Hii Ambayo ni Sayari Ya 3

Katika NBC Premier League, leo tunauanza mwaka mpya wa 2022 kwa mzizima derby ni Simba Sc dhidi ya Azam FC

Mechi hi itapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.

KATIKA MZIZIMA DERBY

Azam FC haijapata ushindi wowote mbele ya Simba kwenye ligi kuu tangu msimu wa 2017/18, wakati Simba ikishinda mechi nne na kutoka sare mechi nne. Katika mashindano mengine nje ya ligi kuu tangu msimu wa 2017/18, Simba na Azam wamekutana mara tano, Azam ikishinda mara mbili na Simba ikishinda mara tatu. LEO wanakutana katika mchezo wa 14 kwenye mshindano yote tangu msimu wa 2017/18, Simba
ikiwa imeshinda michezo saba NA Azam ikishinda michezo miwili.

Je, nini kitatokea Leo?

Je, ni mnyama SimbaSC ama AzamFC nani kuondoka na alama 3?

Tuwe hapa Kufuatilia Mubashara kwa Dakika 90
Timu ya azam mbovu sana watafungwa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom