Simba na yanga walipishwe kodi

Simba na yanga walipishwe kodi

Mars 12

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
221
Reaction score
349
Kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango.Kwa kuwa vilabu hivi viwili yaani Simba na Yanga (Young Africans) ni vilabu vikubwa vya mpira wa miguu tena vina wapenzi kwa mamilioni nazo zitozwe kodi kama biashara zingine zozote.

Mpira ni biashara ndio maana wanaoingia kuwatazama wanalipa viingilio na pia huko wanapofanya kazi ziwe za kuajiriwa au kujiajiri wanalipishwa kodi na TRA.Suala la kulipa kodi sio la mzaha.Isitoshe wanao wachezaji wa kigeni wanaolipwa mamilioni tena wengine kwa pesa za kigeni kama dola za marekani .nao pia watozwe kodi.

Ikiwa hizi timu zimeamua kufuata utaratibu wa kuwaleta wachezaji wa kigeni na kuwaacha vijana wa kitanzania solemba,basi sheria ifuate mkondo wake.Wanao makocha,technical bench wote wageni.

wameiga ulaya.Sasa kule akina Ronaldo,Messi wengineo wanalipishwa kodi kutokana na malipo yao sioni kwa nini wachezaji wa Zambia,Burundi,Kenya,Tunisia,Uganda,Ghana wasilipishwe kodi Pamoja na klabu zao yaani Simba,Yanga,Na nyinginezo.Isitoshe hata klabu hizi nazo zitoe mapato yake kila mwaka kama biashara zingine.

Wake up Waziri Nchemba.
 
Waziri alivyo atapendekeza Simba itozwe afu uto waachwe hali ya uto Ni mbaya jmn
 
Back
Top Bottom