Simba mstaafisheni Juma Kaseja

Mbegu Jr

Senior Member
Sep 23, 2020
137
160
Itakuwa ni jambo la faraja sana kwake maarifa yake ni muhimu kwa bench la ufundi, Manula ni kipa mzuri hatuhitaji kuendelea kuthibitisha hili lakini anahitaji mwalimu atakae kuwa mfano halisi kwake.

Kaseja Juma kwa sasa hiv hachezi mpira kuwavutia watu tena anacheza mpira kuwafundisha watu mpira unavyotakiwa uwe.

Vilevile kwa sasa anacheza kwa sababu awamu hii bila kufanya kazi huli kwakuwa hauwezi ishi kwa kutegemea jina tu, kwa hapo kila mtu atakuwa na faida kwa mwezake Simba itapata mwalimu bora wa makipa pia vilevile timu ya taifa na Kaseja atapata kuendelea kutunza Familia yake

Hata Ndairagije anamuita huyu jamaa sio kwa sababu ya kudaka tu lakini pia kuwapa madini Manuna na Metacha. Simba kama hamkung'amua hili habari ndio hiyo.
 
Mimi pia bado nashangaa kuona kwanini Mwameja hakaribishwi karibishwi pale Simba kwa ajili ya kuwaongezea 'madini' makipa wetu. Na wala hatukumuaga kwa heshima.
Mwameja bado Wanasimba tumenuna kwa jinsi alivyotufanyia umafia pale Shamba la Bibi Fainali za Caf mwaka 92 dhidi ya Stella Abdijan. Malegend watanielewa ila watoto wa mwaka 90 hamuwezi kunielewa, all in all Mwacheni avune alichopanda ndani ya Msimbazi.
Kaseja alituacha wakati mbaya sana akatimkia Yanga bila kuangalia ndani ya Simba alikuwa na Goodwill kiasi gani, Fedha ya Bilionea Manji ilivunja heshima yake na Wanasimba wakubwa bado hawajapona Maumivu aliyowaaachia maaana kuziba pengo lake ilichukua takribani Makipa 10 kusajiliwa na kutemwa.
Kwaherini Vijana wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom