FT: Ligi Kuu Bara | KMC FC 1-3 Simba SC | Uwanja wa CCM Kirumba 26/12/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mbiringe au Patashika ya Moto wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kugombewa leo Disemba 26,2022 ambapo Vijana wenye vipaji, Wenyeji wa mchezo Kinondoni Municipal Council , KMC FC🟠 watakuwa wanakwaruzana na Wataalamu wa kusakata kabumbu lenye viwango vya CAF Wekundu wa Msimbazi Simba SC kwenye Uwanja wa CCM de Kirumba.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 Alasiri Usikose Ukapata Simulizi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

========================


00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa CCM de Kirumba, dakika 90 za Jasho na Damu.

05' Timu zote mbili zimeanza mchezo wa kasi kwa kutafuta bao kwa mashambulizi kadhaa.

10' Mchezo unaendelea kupigwa katikati ya dimba, lakini hakuna hatari yoyote kwa pande zote.

13' Jaribio la kwanza kwa KMC FC lakini golikipa Manula anacheza hatari ile
14' Sakho anashindwa kufunga bao ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga bao

15' Bocco Goooooooooooooaaal gooal

Captain fantastic John Bocco anaweka kambani bao la kwanza akipokea pasi murua kutoka kwa Kapombe

KMC wanashambuliwa, Okrah anakosa nafasi nzuri ya kufunga, ilikuwa Shambulizi kali mno.

20' Mchezo unaendelea huku KMC wakitaka kufuta makosa ya kukosa nafasi ya kufunga.
25' Free Kick kuelekea KMC, anapiga Chama lakini mpira unaokolewa

Simba wamepiga Kambi eneo la KMC, lolote linaweza kutokea hapa
30' Sakho yupo chini akipatiwa matibabu baada kuchezewa vibaya na Vicente

38' Free Kick kuelekea KMC FC, anapiga Chama lakini anakosa nafasi ya kufunga.
Majogoro anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya | KMC FC 0-1 Simba SC

40' KMC wanapata Free Kick anapiga Ame, lakini anababatiza ukuta wa Simba.
43' George anakosa utulivu mbele ya lango la Simba, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga bao.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko, Kanoute anafanyiwa faulo, ni faulo kuelekea KMC, inapigwa kulee kwake Chama, anamtafuta Bocco, lakini maamuzi anasema mpira ulitoka.

Naaam mpira ni mapumziko

HT: KMC FC 0-1 Simba SC

Kipindi cha lala salama kimeanza uwanja wa CCM de Kirumba

52' Sadala Goooooooooooooaaal gooal KMC wanasawazisha bao kupitia kwa Sadala.

Bocco anapiga shutii lakini golikipa Kisu anapangua na Okrah anashindwa kumalizia.

55'' Okrah Goooooooooooooaaal gooal

Kabla KMC hawajamaliza kushangilia Okrah anaweka kambani bao la pili

Sakho anapiga shutii kali, looooooo golikipa Kisu anacheza vizuri sana.
KMC wanafanya mabadiliko, ametoka Sadala na Vicente na wameingia Gambo na Anthony

Mashambulizi yanazidi kuelekea lango la KMC, ngoja Tusubiri Kuona.
KMC wanajibu na wanakosa bao hapa ilikuwa nafasi nzuri ya Salboko

69' Ameingia Kibu na ametoka Okrah upende wa Simba SC.

Kapombe yupo chini akipatiwa matibabu baada kuchezewa faulo, inapigwa kulee kwake Chama

73' Henock Goooooooooooooaaal gooal

Henock anaruka Header moja matata sana na kuweka kambani bao la tatu akipokea free kick au pasi ya Chama.

Anthony anashindwa kufunga bao ilikuwa nafasi nzuri sana, looooooo

Salboko anapiga shutii lakini golikipa Manula anacheza na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao

84' Kibuuuuu anapiga shutii lakini mpira unapaa nje..! Mabadiliko kwa timu ya Simba.
Wameingia Akpan na Kyombo na wametoka Sakho na Bocco

Kyombo anapokea pasi murua lakini Refa anasema ni Offside.

Anthony gooo laaaaaa anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango la Simba.

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo, Kwake Waziri kule mbele, lakini Simba wanakataa.


Akpan katikati ya dimba, Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba wanaibuka na ushindi mnono wa mabao matatu kwa moja.

FT: KMC FC 1-3 SIMBA SC

...... Ghazwat...
 
Kikosi cha Simba SC kinachoanza dhidi ya KMC FC
20221226_150505~3.jpg
 
Mbiringe au Patashika ya Moto wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kugombewa leo Disemba 26,2022 ambapo Vijana wenye vipaji, Wenyeji wa mchezo Kinondoni Municipal, KMC FC🟠 watakuwa wanakwaruzana na Wataalamu wa kusakata kabumbu lenye viwango vya CAF Wekundu wa Msimbazi Simba SC kwenye Uwanja wa CCM de Kirumba.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 Alasiri Usikose Ukapata Simulizi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Kutoka pande za dar es salaam mItaa ya kijichi nahitakia ushindi mnono KMC
 
Back
Top Bottom