Simba mara ya nne sasa mnakosea tena

kokotani

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
211
151
Nimesikiti sana na club ya simba kwa kurudia makosa yale yale kwa mwaka wa nne sasa
Simba wamekua na timu nzuri sana lakini inapofika mechi za mwisho ili wachukua kombe wanakumbwa na mdudu gani sijui
Kuanzia wachezaji wenyewe hadi viongozi wanapoteza focus kirahisi sana.

Kila mara wanarudia makosa yale yale.
Sasa washajiridhishai kumfunga mbao baada ya kubaini ubingwa wamekosa
Hawajui katika footaball yanga anaweza fungwa mechi zote na wao kushinda mechi yao
Pia wanadharau mbao fc duuuu
Jeri muro aliwakosesha ubingwa mwaka jana kwa kuwatoa kwenye reli kisaikolojia.
Kera saaaaaaaana simba aaaaah
 
Kiukweli Simba inakera sana inafanya makosa ya kijinga mno mfano ilikuwa je kufungwa na kagera na kutoa sare na Toto inayoshuka daraja? Huku tukiweza kuwafunga Yanga tena tukiwa pungufu? Vitimu vidogo vinatusumbua sana usishangae tukatoa draw na Mwadui
 
Timu ya ajabu hii.natabiri watafukuza makocha wote kabla ya msimu unaokuja,kamati wa usajili itasajili kwa maono ya wanakamati halafu wataleta kocha mpya kwa mbwembwe na kumkabidhi timu am ayo hajaisajili yeye
 
Tatizo sio Simba.

Wapenzi wa mpira wanaweza kuulaumu uongozi wa Simba SC kwa kutokuipa ubingwa klabu hiyo kwa muda mrefu.
Tatizo halikuwa kwenye uongozi bali kwenye uwekezaji.
Kila mdau wa michezo anajua kuwa mpira ni pesa.
Katika hicho kipindi timu ya Azamu na Yanga ndizo zilizowekeza kwa kiwango kikubwa katika kuboresha maendeleo ya klabu zao na ndizo zilizokuwa zikibadilishana ubingwa
wa ligi.
Azamu inafahamika kuwa milionea Said Bakhresa amewekeza kwa kiwango kinachoizidi Clabu ya Simba.
Halikadhalika
Clabu ya Yanga Afrika, bilionea Yusuf Manji alijitolea kwa mapenzi yake kuwekeza raslimali zake kwa kiwango cha juu kuizidi Simba,
Yanga Afrika ndiyo klabu yenye wachezaji wa kiwango cha juu kabisa na wa ghalama ya juu kupita Clabu zote hapa tz.
Nakumbuka aliyekuwa msemaji wa Yanga Jery Muro aliwahi kusema
kuwa
Mshahara wa wachezaji wa watano wa Yanga unalipa mshahara wa wachezaji wote wa Simba.
Ivi pale mbele akisimama, NGOMA, CHIRWA, TAMBWE, pembani MSUVA, MWASHIUYA, kati, KAMUSOKO, NIYONZIMA, nyuma BOSOU, YONDANI, DANTE.
Ivi ni timu gani hapa Tanzania itazuia uzito huu.
Mi sio mshabiki wa Yanga lakini ukweli nauona, Manji alijitahidi kusajiri vizuri kwa pesa yake ya mfukoni.
Azam nao wanafuatia kwa kusajiri vizuri, Simba inafuatia ndo maana Yanga na Azamu ndio wanaocheza mechi za kimataifa.
Jambo hili ndilo lililo mkasilisha mwanachama wa Simba MO hadi akaona ni afadhali aweke hisa zake hapo ili Simba ifanye vizuri.
Simba kwa kipindi cha Raisi Aveva, ilikabiliwa na ukata mkubwa hadi akina KIIZA na KESSI, wakaamua kuikimbia timu.
Timu ikabaki kusajiri wachezaji wa bei rahisi na wakiwango cha chini kama akina
Blaginoni
Ni bahati tu Simba ilikuwa na wachezaji wa timu B ambao hawakuhitaji kusajiliwa kwa bei ya juu. Walihitaji kupandishwa kikosi cha kwanza hao ndo wanaosaidia timu la sivyo Yanga wangelipa goli zao TANO au na kuzidi. hao ni akina,
NDEMLA, MKUDE, AJIBU, MUHAMEDI HUSEIN.nk
Wacheni kulaumu mpira ni pesa,
Lazima kuwe na mazingira ya kuwavutia wawekezaji wakubwa wa mpira waje kuidhamini timu.
Simba pamoja na kuwa na wachezaji wa ghalama nafuu wamejitahidi sana hadi kufikia fainali ya F.A na kuwa katika nafasi ya pili ya ubingwa wa ligi.
MPIRA NI PESA.
 
Nimesikiti sana na club ya simba kwa kurudia makosa yale yale kwa mwaka wa nne sasa
Simba wamekua na timu nzuri sana lakini inapofika mechi za mwisho ili wachukua kombe wanakumbwa na mdudu gani sijui
Kuanzia wachezaji wenyewe hadi viongozi wanapoteza focus kirahisi sana.

Kila mara wanarudia makosa yale yale.
Sasa washajiridhishai kumfunga mbao baada ya kubaini ubingwa wamekosa
Hawajui katika footaball yanga anaweza fungwa mechi zote na wao kushinda mechi yao
Pia wanadharau mbao fc duuuu
Jeri muro aliwakosesha ubingwa mwaka jana kwa kuwatoa kwenye reli kisaikolojia.
Kera saaaaaaaana simba aaaaah
Vichuya FC
 
Tatizo sio Simba.

Wapenzi wa mpira wanaweza kuulaumu uongozi wa Simba SC kwa kutokuipa ubingwa klabu hiyo kwa muda mrefu.
Tatizo halikuwa kwenye uongozi bali kwenye uwekezaji.
Kila mdau wa michezo anajua kuwa mpira ni pesa.
Katika hicho kipindi timu ya Azamu na Yanga ndizo zilizowekeza kwa kiwango kikubwa katika kuboresha maendeleo ya klabu zao na ndizo zilizokuwa zikibadilishana ubingwa
wa ligi.
Azamu inafahamika kuwa milionea Said Bakhresa amewekeza kwa kiwango kinachoizidi Clabu ya Simba.
Halikadhalika
Clabu ya Yanga Afrika, bilionea Yusuf Manji alijitolea kwa mapenzi yake kuwekeza raslimali zake kwa kiwango cha juu kuizidi Simba,
Yanga Afrika ndiyo klabu yenye wachezaji wa kiwango cha juu kabisa na wa ghalama ya juu kupita Clabu zote hapa tz.
Nakumbuka aliyekuwa msemaji wa Yanga Jery Muro aliwahi kusema
kuwa
Mshahara wa wachezaji wa watano wa Yanga unalipa mshahara wa wachezaji wote wa Simba.
Ivi pale mbele akisimama, NGOMA, CHIRWA, TAMBWE, pembani MSUVA, MWASHIUYA, kati, KAMUSOKO, NIYONZIMA, nyuma BOSOU, YONDANI, DANTE.
Ivi ni timu gani hapa Tanzania itazuia uzito huu.
Mi sio mshabiki wa Yanga lakini ukweli nauona, Manji alijitahidi kusajiri vizuri kwa pesa yake ya mfukoni.
Azam nao wanafuatia kwa kusajiri vizuri, Simba inafuatia ndo maana Yanga na Azamu ndio wanaocheza mechi za kimataifa.
Jambo hili ndilo lililo mkasilisha mwanachama wa Simba MO hadi akaona ni afadhali aweke hisa zake hapo ili Simba ifanye vizuri.
Simba kwa kipindi cha Raisi Aveva, ilikabiliwa na ukata mkubwa hadi akina KIIZA na KESSI, wakaamua kuikimbia timu.
Timu ikabaki kusajiri wachezaji wa bei rahisi na wakiwango cha chini kama akina
Blaginoni
Ni bahati tu Simba ilikuwa na wachezaji wa timu B ambao hawakuhitaji kusajiliwa kwa bei ya juu. Walihitaji kupandishwa kikosi cha kwanza hao ndo wanaosaidia timu la sivyo Yanga wangelipa goli zao TANO au na kuzidi. hao ni akina,
NDEMLA, MKUDE, AJIBU, MUHAMEDI HUSEIN.nk
Wacheni kulaumu mpira ni pesa,
Lazima kuwe na mazingira ya kuwavutia wawekezaji wakubwa wa mpira waje kuidhamini timu.
Simba pamoja na kuwa na wachezaji wa ghalama nafuu wamejitahidi sana hadi kufikia fainali ya F.A na kuwa katika nafasi ya pili ya ubingwa wa ligi.
MPIRA NI PESA.

Kuna ukweli mdogo kwenye makala yako ndefu. Unaonekana kuipamba sana Yanga kwa ubora ambao haina.
Tukiacha unazi na kuacha takwimu ziongee Simba ni timu bora zaidi uwanjani kuliko Yanga.

- Ndiyo timu pekee ambayo bado inapigania makombe mawili. Yanga inapigania kombe 1 tu, Azam imeshamaliza msimu
- Ndiyo timu pekee iliyozifunga timu zote washindani, yaani Yanga na Azam. Azam hajaifunga Yanga wala Yanga hajaifunga
Simba.
- Ndiyo timu iliyoweka rekodi ya kuwa na umiliki mpira mkubwa ktk mechi zote bila kujali matokeo au upungufu wa
wachezaji uwanjani.
- Ndiyo timu yenye wachezaji wengi ktk timu Taifa pamoja na Azam

Ukiacha kiwango cha mshahara naamini Simba uwanjani imekuwa bora zaidi kuliko Yanga na Azam, na hata uwezo wa wachezaji ni mkubwa sana. Kilichoaigharimu nadhani ni kuchelewa kupata muunganiko, na kupiga hesabu vizuri za kuwania ubingwa
 
Mkuu niruhusu nitofautiane na wewe. (1) Kuishia kupigania makombe zaidi ya moja kunategemea pia na kipaumbele cha timu husika kwa mashindano ya makombe hayo. Inakuwa si busara, mathalan, kwa Mourinho kuweka mkazo zaidi kwenye EPL ili apate nafasi mojawapo kati ya nne za juu tangu alipoingia robo fainali ya Europa. Huenda hata Simba kukamia sawa makombe yote mawili kwa pamoja kukawa kumemchangia kufikia nafasi aliyo nayo sasa kwenye VPL. 2. Kuzifunga timu zote kubwa katika ligi ni kigezo sawa cha ubora wa timu na kile cha ubovu wa timu hiyohiyo kufungwa na timu zilizo kwenye nafasi za chini za msimamo wa ligi. Waingereza husema a chain is only as strong as the weakest link. 3. Kumiliki mpira ni mbinu mojawapo lakini siyo pekee ya mchezo. Timu ya kwanza kwa ubora ni inayomiliki zaidi mpira na kuishia na ushindi, ikifuatiwa na inayozidiwa kwenye umiliki lakini ikashinda, ikifuatiwa na inayomiliki zaidi ikashindwa mchezo na mwisho ni inayozidiwa kumiliki mpira na ikashindwa mchezo. Hii sifa unayoipa timu yako ya kumiliki zaidi licha ya kufungwa ndiyo ile wanayotaniwa Wazanzibari wa enzi za Gossage Cup: twafungwa lakini chenga twawala! 4. Kuwa na wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa kunategemea timu ya kwanza ya klabu husika kuwa na wachezaji wangapi wa kigeni. Kwa timu yenye wachezaji wengi wa kigeni wanaoanza, inakuwa ni vigumu kuwa na wachezaji wengi wazawa kwenye timu ya Taifa. Kumbuka VPL inaruhusu wachezaji 7 wa kigeni. Maana yake ni kuwa wakicheza wote, ni wazawa wanne tu ndio watapata nafasi. Kwa hivyo kigezo cha kuwa na wachezaji wengi wazawa kwenye timu ya Taifa kinaweza kuwa pia ni kigezo cha usajili mbovu wa wachezaji wa kigeni, hasa kama timu husika imesajili wote saba.
Kigezo kisicho shaka cha ubora wa timu ni wingi wa magoli ya kufunga, uchache wa magoli ya kufungwa, uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa, upana wa kikosi na ari ya kupambana.
 
Nakubaliana na mengi uliyoyasema, ndio maana sikuweka kigezo kimoja pekee. Unapokuwa na timu yenye vigezo nilivyovitaja ukataka uifananishe na timu ambayo haina vigezo hivyo basi unakuwa umeamua kulazimisha mambo.
Labda acha nikuonyeshe upande wa pili wa hoja nilizoleta.

Kwanza, wewe mwenyewe unajua kuwa ni shauku ya kila timu kuchukua makombe yote inayoshiriki ikiwezekana. Ni pale tu imapoona haina uwezo au raslimali za kutosha ndio inaanza kuchagua nguvu ipeleke wapi. Hapo ndio timu inaweza kuweka kipaumbele iingie ktk top 4 kwanza au ipate angalau kombe la FA. Lakini timu bora inataka kuchukua vikombe vyote na huu ni ukweli ambao haupingiki. Na ndio maana Yanga, Simba na Azam wote kwa pamoja walisikika wakitaka kutwaa vikombe vyote vya FA na Ligi. Yanga alitwaa vyote mwaka jana nataka kuamini ni kutokana na ubora iliokuwa nao kuliko timu nyingine na sio vinginevyo.

Hoja yako ya pili sikubaliani nayo kabisa, na ninaamini kutokana na uelewa mkubwa uliouonyesha kwenye ufuatiliaji wa masuala na kanuni za soka; umeitoa kwa bahati mbaya. Kufunga timu pinzani za hadhi sawa na wewe ni kigezo kikuu kuliko kufungwa na timu iliyoshuka daraja. Wenye mpira wameweka kigezo cha head-to-head ambacho ninaamini unafahamu maana yake. Unapotaka kujipima uwezo wako wa kugombea ubingwa lazima ushindane na mabingwa na ukiwapiga hao unaweza kusema wewe ni bora kuliko wao, (of course if other things remain constant).

Wewe mwenyewe unafahamu kuwa msimamo wa timu hizi tatu za Simba, Yanga na Azam kwa mwaka huu ni kama ifuatavyo;

P W D L PTS
Simba 4 2 2 1 7
Yanga 4 1 2 1 4
Azam 4 1 1 2 4

Sina tatizo na hoja yako namba 3, lakini nakuongezea siri iliyoko katika kumiliki mpira ni uwezo wa kulazimisha wapinzani wafanye unachotaka wewe wafanye, na mbinu muhimu sana ya sio tu kupangilia mashambulizi lkn pia kujilinda. Inafurahisha sana pale timu inapokuwa pungufu lakini inaweza ku-dictate mchezo. Kila shabiki mzuri anatamamni kuwa na timu ya aina hii, of course hasa kama mwisho wa mchezo inaondoka na matokeo. Kinyume chake haina maana.

Hoja yako ya nne, iko sawa lakini ni irrelevant kwa Simba na Yanga! Yanga ina wachezaji 3 tu wanaochezea timu za taifa tofauti na Tanzania, almost sawa na Simba ambayo licha ya kuwa na wachezaji 7 katika Taifa Stars ina wengine 2 ambao ni muhimili wa timu zao nje ya Tanzania.

Ni kwa vigezo hivi na hasa mchangayiko wake ndio maana nikasema Simba inaonekana bora kuliko Yanga kwa ligi ya mwaka huu.
 
Nimefurahia sana hoja zako. Ni fundisho kwa wengine humu JF na nje ya humu kwamba hoja hujibiwa kwa hoja, si matusi ama kejeli. Laiti ungekuwa karibu, ningekualika kahwa tukapata muda zaidi wa kujadili hoja hii pana. Naogopa tukiendelea kuijadili humu tutawanyima wengine wasaa wa kujadili mada kuu ya mwanzisha uzi; tutamtekea nyara mada yake. Ila niseme tu kwamba hadi sasa Kombe la FA hapa kwetu linategemea zaidi bahati kuliko uwezo. Bahati inakutana na timu gani kwenye uwanja upi, hakuna fair ground kwa washindani kwa sababu inachezwa kiwanja cha mmojawapo tena mzunguko mmoja tu. Bahati ya timu gani kubwa utakutana nayo baada ya kuondoka timu zote zilizoingia kushiriki. Yaani tusitumie sana kombe la FA kuwa ni kigezo cha ubora wa timu, mpaka hapo kasoro hizo zitaposawazishwa. Head-to-head yes. Ni kigezo kinachotumika kupima ipi bora kati ya timu mbili. Ni Hispania tu ndiko kinatumika kuamua bingwa wa Ligi, lakini tu itokezeapo timu mbili za juu kufanana kwa kila kigezo chengine. Kwa hivyo sitakosea kusema kuwa head-to-head ni kigezo cha ubora wa timu mbili wakati wanapokutana; baada ya hapo vigezo vya ubora wa timu ndani ya ligi vinachukua nafasi yake. Kuendekeza ubora kwa kigezo cha head-to-head kunapelekea timu kukamia mechi badala ya kukamia Ligi. Ndio kosa mojawapo la Simba.
Ni kweli kila timu huanza na dhamira ya kuchukua makombe yote. Lakini kadri timu za kwenye mashindano ya makombe hayo zinavyojichuja kimsimamo ndivyo timu inavyorekebisha mwelekeo wake kwenye mashindano hayo kwa kuweka vipaumbele vyake. Barcelona inaweka nguvu zake zote kwenye La Liga hivi sasa, lakini ukiangalia kwa undani utaona Real pamoja na kutaka ubingwa wa nyumbani kwa nguvu, lakini imeelekeza nguvu zake zaidi kwenye Champions League final. Naamini hata Yanga walifanya hivyo kwa Mbao, hasa walipoanza kuona mambo ni magumu kwenye nusu ya kwanza ya mechi ya nusu fainali dhidi ya Mbao. Nina wasiwasi Simba hawakufanya hivyo.
Mkuu nakushukuru tena kwa hoja zako fasaha, na ni fahari yangu kuona kwenye JF kuna watu makini na mahiri kama wewe. Big up!
 
Back
Top Bottom