John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Miezi kadhaa iliyopita mwekezaji wa Simba, Mo Dewji alitangaza kujiweka pembeni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya klabu hiyo, kisha ‘kishkaji’ akamkabidhi nafasi hiyo Try Again, baada ya hapo Mo akapotea, akawa anaonekana kwenye matukio machache ya klabu, ni kama aliamua 'kukata waya' na kuendelea na mishe zake.
Zile kelele za uwekezaji wa Bilioni ngapi zile ukapotea…
Straika wao Dejan akatangaza kuvunja mkataba akidai kuna vitu kkabu haijatimiza, Simba wakasema watamchukulia hatua, kimya kikafuata...
Hivi karibuni Simba wakamchukua Juma Mgunda wakitangaza wamemuazima kutoka Coastal Union, wenye kuazimwa wakatangaza hawana mkataba na Mgunda, inamaanisha kuna jambo lilikuwa linafichwa.
Katiba ya Simba inaonesha wanatakiwa kuwa wameshafanya Uchaguzi Mkuu hadi kufikia Novemba 2022 lakini hilo halijafanyika na hakuna taarifa rasmi kwa mashabiki na wanachama wao.
Timu haina kocha wa viungo (viongozi wapo kimya), hatma ya Mgunda tulitangaziwa amekopwa, miezi inakatika hawajasema kinachoendelea (wapo kimya).
Selemani Matola ametangaza anaondoka kwenda kwenye masomo (kama ni kweli), hatima ya msaidizi mwingine haijatangazwa (viongozi wapo kimya).
Baada ya Muharami Said Mohammed ‘Shilton’ kutangazwa anashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na madawa, klabu inaibuka na kusema haikuwa na mkataba naye na alikuwa kocha wa muda tu, inamaanisha Simba haikuwa na kocha wa makipa (viongozi wana la kujibu hapa).
Katika kile kinachoonekana ‘kupaniki’ Simba wanamtambulisha Chlouha Zakaria kuwa kocha wa makipa, taarifa yao ya haikusema katoka wapi, CV yake japo kwa ufupi, ataanza kazi lini, mkataba wake upoje…n.k
Nahisi Simba kuna shida kubwa zaidi ya hii inayoonekana nje na mambo yakiendelea hivi viongozi wa Simba watakipata wanachokitaka, nadhani kila shabiki wa soka anajua ‘nature’ ya mashabiki wa soka hasa la Tanzania.