SIMBA inashuka daraja kama utani

SIMBA inashuka daraja kama utani

Kwani SIMBA ya ngapi katika msimamo... na mechi zimebaki ngapi ligi kwisha!!..... Nyie kandambili kama simba inafanya vibaya si ndo mnatakiwa kufurahi,, sasa maneno ya nini..!!! Tuachieni timu yetu tunajua tunapitia kwenye kipindi gani... Nyie endeleeni kununua mechi mkikutana na wanaume huko nje mnapigwa mnarudi kwenye ligi yetu ya ndondo
Like@kiongozi
 
Simba ina mafundi wengi lakini haina soldiers

ndo maana timu ikicheza jihad kama mbeya city au Stendi leo inaisumbua Simba

walipaswa kutafuta soldiers pia sio mafundi peke yake

Kwa hiyo unachosema ni Kuwa Stand UTD CHAMA la wana!! Haina Mafundi au??
 
...ishuke tu ikacheze umishumta na umiseta,huku wanatupotezea muda hakuna cha maana wanafanya...
 
...sio mshabiki wa Simba lakini naamini hawawezi kuteremka daraja.

...vilabu vikongwe vina fitna sana
 
Simba pole yao,ila wanaeza kujipanga mda upo na mechi bado nyingi

...mkuu walivyotoka kwenye umiseta zanzibar wakaja na mkakati wa mechi tatu pointi tisa,wako wapi ?walikula mashuti ya mbavu mpaka wamekaa. Izo mechi zilizobaki watapigwa hamna mfano maana wamesha legea wanakalishwa tu...
 
simba ina mafundi wengi lakini haina soldiers

ndo maana timu ikicheza jihad kama mbeya city au stendi leo inaisumbua simba

walipaswa kutafuta soldiers pia sio mafundi peke yake

interesting
 
Hawa yebo yebo badala wafuate yao wanakalia uswahili kufuatilia yasowahusu. Wamekalia ushirikina tu wa uwanjani.

Ninyi mikia mirefu fc mmesahau tayari yaliyotokea kule morogoro wanakati mnacheza na polisi moro!! Si mlitaka kuzichapa wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya uchawi!!? Ama kweli mikia haina kumbukumbu na ndio maana mwenyekiti wao aliwaita mambumbumbu.
 
Tutapigana kufa na kupona kuhakisha simba inabaki ligi kuu kwani kumpoteza mtani ni shida bora ya kuchanika kwa nguo.
 
Simba na Yanga zingeshuka daraja halafu zife kabisa kama Pan Africa na Nyota Nyekundu, mi ningefurahi sana.​
 
Simba na Yanga zingeshuka daraja halafu zife kabisa kama Pan Africa na Nyota Nyekundu, mi ningefurahi sana.​

Kwa hili utangoja sana mkuu. Hawa jamaa wawili wanawaweka mjini watu wengi sana kuanzai TFF mpk watu wa kawaida. So kushuka kirahic ivyo ni ngumu asee.
 
Huo ni mtaji wa akina Malinzi, kama kushuka kihalali ilikuwa mwaka 1988.
 
Kwa mwenendo wa ligi Simba mwaka huu inaelekea kuaga Ligi Kuu na kucheza ligi Daraja la Kwanza.

Llakini hii inatokea kama utani vile japo ni swala la muda na wengi hawataamini
Msipomuongelea Mume wenu naona vitoto mapacha viwili tulivyowapa Disemba vinacheza cheza tumboni?
 
Ninyi mikia mirefu fc mmesahau tayari yaliyotokea kule morogoro wanakati mnacheza na polisi moro!! Si mlitaka kuzichapa wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya uchawi!!? Ama kweli mikia haina kumbukumbu na ndio maana mwenyekiti wao aliwaita mambumbumbu.
Kama ungeangalia Sports Bar ya Clouds jana na kuona jinsi Yeboyebo walivyoingia uwanjani na Akilimali wao ungeelewa nini maana ya Yanga kuitwa vigagula.

Big up Sports Bar kwa kuweka wazi uozo wa Soka la Bongo.
 
Nisingependa hii kitu itokee, maana watani tutawakoma, ila ingependeza kama tukishuka, naona tunafanya mambo kimazoea tu, kuwa sisi ni chama kubwa hatuwezi cheza daraja la kwanza.

Viongozi waamke, kwa kiwango wanachocheza simba, inawezekana kabisa kushuka daraja. Niliangalia mechi na Standa United, sikuamini kiwango wanachocheza simba, ni cha chini ya chini, wachezaji hawana hamasa, yaani kiwango cha mechi nyingi za simba ni chini ya average.

Simba karibu yote inahitaji overhaul, na waganda mie binafsi wala siwafagilii ndani ya Simba. Hawana mchango, mchango wa Coutinho pekee kwa yanga ni mkubwa kuliko wachezaji wote wa nje walio simba.

Ifike wakati uongozi ukubali kuwa kusajili wachezaji wa nje sio fashion, kiwango ni muhimu, kama yawezekana wasajili majembe ya hapa hapa bongo na pia uongozi ujipange.

Wachezaji simba karibu wote wamekuwa laini laini tuu, beki laini, kiungo laini, ushambuliaji ndo kabisaaaa, yaani simba sasa hivi nikiangalia, huwa naona angalau Ndemla ndo anajitahidi, na Singano kidogo (kinachomwangusha lishe) hawa huwa wanakimbia uwanjani kusaka kila mpira, mkude sijui kimemkuta nini. Isihaka anatumia akili sana ila mbavu hana, alitakiwa awe na partner wake mwenye roho mbaya, sasa wote wawili ni akili ila mbavu hamna.

Inasikitisha sana hii Simba!!
 
...ishuke tu ikacheze umishumta na umiseta,huku wanatupotezea muda hakuna cha maana wanafanya...

Nikisoma maoni haya nashindwa kuelewa kama kweli aliyeandika anaelewa vizuri sula linalojadiliwa hapa na kama kweli anaelewa mpira (soka) unavyoendeshwa. Maana anadai samba inamptezea muda halafu wakacheze umishumta na umiseta vitu vyote hivi haviwezekani katika uhalisia wa mambo
 
Nilimaanisha samba sio "samba" samahani
 
kwani kuna mzungu simba? aondoke atuachie timu yetu
 
Back
Top Bottom