Mimi naamini kuna udhaifu ndani ya uongozi wa vilabu vyetu na kwa waandishi wetu wa habari.
Lakini siamini kwamba Aveva & Co. ni washenzi kiasi cha kuthubutu kutudanganya kama inavyofikiriwa.
Ninahisi:
1. Ni kweli Simba ilicheza na Orlando Pirates ya Afrika ya Kusini na kutoka 0-0, lakini si hii Orlando ya Premeir. Hata hapa Tanzania kuna Simba (na Small Simba) nyingi tu huko mitaani, au
2. Inawezekana wamecheza na Orlando Pirates yenyewe na kutoka nayo 0-0, lakini ni Orlando ya wachezaji wa akiba na wa akademia, huku wa kikosi cha kwanza wakiwa mashindanoni. Ndio maana Malinzi anasisitiza kuanzisha akademia kwa 5%, au
3. Inawezekana walicheza na timu waliyoamini kwamba ni Orlando Pirates, kwenye uwanja walioamini kuwa ni wa Orlando Pirates, lakini kumbe walicheza na kundi la wajanja fulani hivi walioona wasipoteze fursa ya kula mshiko wa nje nje. Nani kasema wenye bongo za kutapelia wako Bongo tu?, au
4. Simba hawajacheza wala hawajamwambia yeyote kwamba wamecheza na Orlando Pirates, ila wanaudaku (wanahabri?) wetu wakajua tu kimahesabu kwamba kwa sababu Simba huwa inatoa sare kila mechi, na kwa sababu awali ilisemwa kwamba wangecheza na Orlando Pirates, na kwa sababu sare pekee ambayo Simba haijatoa kwenye mfululizo huu ni hiyo ya 0-0, basi mkokotoo (calculation) rahisi ni kuwa hiyo ndiyo sare iliyopatikana. Hivyo ndivyo udaku unavyokokotolewa, au
5. Hatuwezi kujua, labda 'Kamati ya Ufundi' iliagiza kwamba ili ishinde mechi ya 18/10, Simba lazima itoe sare nyengine kabla ya hapo, hata kama ni ya kubuni, au
6. Jinsi Simba inavyoendeshwa Kisayansi, wameona wawazuge watani wao kwamba wametoka sare nyengine, watani hao wazidi kubweteka ili Mnyama awashtukize hiyo siku ya siku, au..........