DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,470
Ngoja leo niongelee kidogo timu yangu ya zamani ya Simba SC.
Hapo nyuma niliwahi kusema Jonathan Sowah siyo chaguo sahihi kwa Simba na nitakupa sababu kubwa tatu.
1. Sowah ni mzee na hajawahi kuonyesha uwezo wowote kimataifa. Huyu jamaa hata ukiangalia tu maumbile yake utagundua anachezea miaka 32-35. Kwa levo za Simba na kile wanacholenga kufanya, huyu alitakiwa kuwa chaguo la pili au tatu na siyo la kwanza.
2. Wachezaji wa Ghana wana masikhara mengi na viburi. Ghana ya miaka hii siyo ile ya kina Abedi Pele au Anthony Yeboah. Ndiyo maana wachezaji wao hata wa kimataifa wakirudi kuchezea timu ya taifa unasikia migomo na drama kibao. Ni watu wanaojiamini sana na wenye viburi.
3. Uhusiano wake na Hersi haiwezi kufutika kwa kumwambia achane picha yake. Tusidanganyane, Hersi anajenga mahusiano ya karibu mno na wachezaji. Ndiyo maana pale Yanga, Simba haina uwezo wa kumchomoa mchezaji yoyote yule hata wamuahidi mara tatu ya mshahara anaolipwa sasa. Sowah amesema Hersi alimfanyia jambo kubwa ila hajawahi kulitaja hilo jambo. Sowah kuja Simba ni kwa sababu Hersi amempa baraka za kufanya hivyo, tusisahau hilo.
ZIADA: Kitendo cha kuchana picha ya Hersi kumempa pressure itakayomfanya asiende kufanikiwa. Juzi nimetoka kusema Simba haijui kujifunza, inapenda kurudia makosa yake. Ateba aliongea maneno ya shombo dhidi ya Yanga kabla ya derby na anaondoka Tanzania bila kuifunga Yanga hata goli la mkono tena akiwa amepotea kabisa na haeleweki.
Kitendo cha viongozi wa Simba kumfanya achane picha ya Hersi ni utoto na kujikosha tu kwa mashabiki kama ambavyo walitengeneza drama za Feisal. Kiufupi, viongozi wa Simba wanacheza tu na hisia za mashabiki wao.
Simba mkumbuke ubingwa wa ligi ya Tanzania unaamuliwa kwa mechi zisizozidi mbili. Simba ilikosa ubingwa si kwa kufungwa na Yanga mara mbili bali kwa kutoa sare za kizembe dhidi ya Coastal Union na Fountain Gate.
Sowah atachoma mechi kama mbili zitakazowahakikishia ubingwa Yanga. Jiandaeni kisaikolojia.