Simba dume

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,405
1> Ndevu zake ni sharubu,shingoni zamzunguka.Haziwezi kusharabu,tabia yake ya paka.Toka enzi za mababu,simba aliheshimika.
Simba dume ni mkali,ila mvivukuwinda.

2> Mwili wake ni mkubwa,ulojawa na maguvu.Wala halagi ubwabwa,hawezi tegwa kwa nyavu.Ingawa tembo mkubwa, simba atoa uvivu.Simba dume ni mkali, ila mvivu kuwinda.

3> Atisha angurumapo,msitu watetemeka.Pindi jua lituapo, swala wengi wateseka.Bora yangu mimi sipo,simba ningelimfyeka.Simba dume ni mkali,ila mvivu kuwinda.

4> Simba huyu wa ajabu,anayo sumu ya nyoka.Rangi yake ya dhahabu, tumpende ka bazoka.Kwa kauli zake babu, simba huyu nimzuka.
Simba dume ni mkali, ila mvivu kuwinda.

5> Simtaki simba huyu,hasara kubwa porini.Anauvunja mbuyu,arukiapo tawini.Laana yake kibuyu,imuandame kichwani.Simba dume ni mkali,ila mvivu kuwinda.

Shairi=SIMBA DUME.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382386.
0655519736
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom