Simba atafungwa na Yanga Jumapili

CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
7,786
15,732
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kuwa huu ni utabiri wangu binafsi juu ya mechi hii yenye kuamua hatma ya Ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara (NBC PREMIER LEAGUE).

Huu ni utabiri tu, unaweza kuukubali au kuukataa kwa sababu zako, ila kwangu nimetabiri Simba atafungwa na Yanga siku ya Jumapili pale Taifa.

Kwanini nimetabiri hivi? Nakupa facts mbalimbali ambazo kimsingi zitawapa shida zaidi Simba kuliko Yanga.

1. Selection ya Kikosi
Mara zote kwa miaka ya karibuni Simba imekuwa ikitoa Kikosi ambacho ama sio kile kinachoanza Mechi nyingi au Kile kinachokuwa na lengo kubwa la kuzuia bila kuweza kukaba vyema.

Ni matarajio yangu Simba mbele wataanza na CHAMA, BALEKE, NTIBAZONKIZA, SAKHO. Then Viungo Lazima wataanza na MZAMIRU, KANOUTE. So hadi hapo utaona Simba itakuwa na wachezaji 4 wasio na faida Pindi timu yao ikiwa haina mpira.

Wakati kwa upande wa YANGA, lazima ianze na MUSONDA, AZIZ, MOLOKO, MAYELE kwa juu na katikati ni AUCHO NA BANGALA.

Hapo Yanga utaona wazi itakuwa na wachezaji 2 tu ambao hawana faida pindi timu ikiwa haina mpira (MAYELE, AZIZ KI) Hao wengine wote ni watu wa kusaidia sana mabeki na viungo wao.

Game itakuwa ya namna gani?

Kwa ujumla hii game itaamuliwa sana viungo wa Yanga, na kwa namna yoyote NABI ataingia na Mfumo alioutumia kwenye game Vs Azam yaani lazima AZIZ KI atakuwa free role midfielder, atamtaka kutotumia nguvu kubwa kukaba bali awe relaxed akiwa na mpira na aongozwe na maono yake kwa uhuru kabisa.

Unajua kwanini?, NABI anataka kuipa presha SIMBA ya kuzuia Mabeki wake na Viungo wa Chini kupanda bila sababu za Msingi. Hivyo kutengeneza Gap kubwa kati ya Viungo wa Simba na washambuliaji.

2. UFINYU WA MAANDALIZI KWENYE GAME YA WYDAD.
Kwa namna yoyote SIMBA ana kazi kubwa VS WYDAD, hivyo kocha kwa uchache wa machaguo ya wachezaji wake basi atalazimika kufanya SUB nyingi second half ili kuweza kujipanga na Game hiyo ya Klabu Bingwa.

Shida ni nini hapa? Shida ni kwamba Yanga ina machaguo mengi nje ya kikosi cha kwanza na Bado ikakupa matokeo mazuri zaidi hata katika mechi kubwa. NABI anaweza akaanza na KISINDA, MORRISON, MUSONDA, NZIZE
Chini yao akaanza na SUREBOY, na BANGALA na bado akadominate game.

3. Mazingira ya GAME
At any means Yanga wanahitaji kumaliza mbio za Ubingwa siku hii, Ushindi kwao utawahakikishia ubingwa kwani watasaliwa na michezo 4 huku wakihitaji point 1 tu. Mara zote game ambazo Yanga zinaamua hatma yake kwenye Ligi, basi anapata matokeo chanya. Hii itachangiwa pia na Game yao inayofuata ya Kimataifa Vs RIVERS UTD kwamba kidogo wako kwenye uzani sawa hivyo wanaweza jilipua game ya SIMBA na bado wakabattle na RIVERS tofauti sana na SIMBA kwa WYDAD, kwani majeraha yoyote ya mchezaji muhimu wa Simba basi italeta shida game na WYDAD.

4. FORM ZA TIMU HUSIKA
Wadau, kwenye Suala la Form, msimu huu Yanga yuko juu sana ukilinganisha na SIMBA. WORK RATE ya wachezaji wa Yanga iko juu ukilinganisha na Simba ambao wengi wamekuwa ni ingia toka, hasa kutokana na majeraha ya hapa na pale.

Yanga ameshinda Game 12 mfululizo za ligi huku akiwa na Clean sheet 10, na akiruhusu magoli 3 tu. Wakati huo Simba kwenye mechi 12 za mwisho ameshinda game 10 huku 2 akienda sare na AZAM na KAGERA SUGAR na akiruhusu magoli 8 na akiwa na clean sheet 5 tu.

SIMBA ina wastani nzuri wa kufunga kwani wao kwa wastani kila mechi wamepata magoli kuanzia mawili kwenda juu. Wakati huo Yanga wao wastani ni magoli 2 kamili kwa kila mechi.

UTABIRI WA MATOKEO.

Kwa kuangalia game ilivyo, vikosi, mtindo wa uchezaji, na mechi za mbele zao.

FT SIMBA 1-3 YANGA.
Utabiri wa magoli (HII SASA NI RAMLI)
Kwa upande Simba naona kabisa nafasi ya kufunga kama anayo NTIBAZONKIZA wakati Yanga kule nafasi ya Ufungaji wanayo, AZIZ KI (80%), MORRISON na KISINDA.

NAMALIZIA LINDO HAPA. TUKUTANE KWA MKAPA 16.04.2023.
 
Sijui ni vipi Simba inaonekana haipo kwenye Form ila mimi nachokiona ni tofauti na wengi wanavyoona. Kiuhalisia Simba ndio timu yenye watu wengi wanaojua kutengeneza mashambulizi tofauti na Yanga.

Kwa maeneo ya mbele na pembeni Simba wapo vizuri. Simba ina weakness ya kiungo mkabaji tu na upande wa nyuma timu zote zina tatizo linalofanana la kuacha mianya na mabeki kujisahau. Simba sio mbovu kama inavyokuzwa
 
Sijui ni vipi Simba inaonekana haipo kwenye Form ila mimi nachokiona ni tofauti na wengi wanavyoona. Kiuhalisia Simba ndio timu yenye watu wengi wanaojua kutengeneza mashambulizi tofauti na Yanga. Kwa maeneo ya mbele na pembeni Simba wapo vizuri. Simba ina weakness ya kiungo mkabaji tu na upande wa nyuma timu zote zina tatizo linalofanana la kuacha mianya na mabeki kujisahau. Simba sio mbovu kama inavyokuzwa
Kumbuka hapa zinafananishwa SIMBA VS YANGA. So kama Simba sio Mbovu ni kwa timu zingine, ila ukifanya comparison na Yanga basi Simba ni mbovu kwa Yanga. Au ww hujaelewa mada?

Mbaya zaidi unarudi kusema ubovu kwenye Kiungo na beki. Sasa unakataa nini na hapo umesemaje?
 
Sawa tunalinganisha Yanga vs Simba.
Kwenye angle ya ubora, unatumia nini kuhitimisha kuwa timu A ni bora kuliko timu B? Je ni takwimu kwa ujumla? Au hisia? Au h2h? Kama ni takwimu basi njoo na takwimu upande...
Mbona hapo takwimu nimeweka kaka? Nimesema hapo SIMBA ana wastani nzuri wa kufunga akiwa na wastani wa magoli 2 au Zaidi kwa mechi wakati Yanga ana wastani wa Magoli 2 kamili kwa mechi, hujui kusoma kaka?.

Takwimu zingine zote Yanga anaongoza tu.

Magoli ya kufungwa
YANGA 11
SIMBA 14

MAGOLI YA KUFUNGA
YANGA 50
SIMBA 60

POINTS
YANGA 68
SIMBA 60

USHINDI
YANGA 22
SIMBA 18

DROO
YANGA 2
SIMBA 6

YANGA MECHI ZOTE ZA LIGI IMEPATA GOLI.

YANGA AMERUHUSU GOLI kwenye Mechi 7 tu.
Vs Azam magoli 4
Vs Ihefu Magoli 2
Vs Simba 1
Vs Geita 1
Vs Ruvu 1
Vs Singida 1
Vs Polisi 1
 
Mm nimetabiri tu, kutokana na kuangalia hints mbalimbali za hizo timu.
Sawa..ila Simba SC kwenye game ya tarehe 16, wameapa kutoruhusu Young African kurudisha goli/ Magoli ( level score board).

Goli likiingia halichomoki, hawataki mazoea ya kila wakifunga Young African wanasawazisha.


Utabiri wangu ( just prediction)

Simba SC 4 : 1 Young African
 
Sawa..ila Simba SC kwenye game ya tarehe 16, wameapa kutoruhusu Young African kurudisha goli/ Magoli ( level score board).

Goli likiingia halichomoki, hawataki mazoea ya kila wakifunga Young African wanasawazisha.


Utabiri wangu ( just prediction)

Simba SC 4 : 1 Young African
Yanga hajawahi kuruhusu zaidi ya goli 2 Mwaka wa 3 huu sasa kwenye ligi.
 
Sawa..ila Simba SC kwenye game ya tarehe 16, wameapa kutoruhusu Young African kurudisha goli/ Magoli ( level score board).

Goli likiingia halichomoki, hawataki mazoea ya kila wakifunga Young African wanasawazisha.


Utabiri wangu ( just prediction)

Simba SC 4 : 1 Young African
Ishu sio kuapa, ishu hapa ni uwezo, sio kwamba Timu inapenda kufungwa ila uwezo mdogo.
 
Game haitakuwa na magolli mengi, sanasana draw ya 1 - 1 ama kutofungana kabisa, matokeo mengine Yanga kuongoza.
Mchezo utakuwa wa kuviziana sana, wanaweza kutokutumia nguvu, kuogopa majeruhi.

End of the day, Yanga ana kila sababu ya kushinda, katika kipindi hiki ambacho iko hot.
Aziz KI ana goli lake, Farid M. Kipindi cha pili kama kawa, ushindi upo...
Kila la kheri Yanga, tunaanza na Mungu na tutamaliza na Mungu 🙏🙏🙏🔰🔰🔰

DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.
YANGA MBELE MIKIA NYUMA.
 
Ishu sio kuapa, ishu hapa ni uwezo, sio kwamba Timu inapenda kufungwa ila uwezo mdogo.
Inawezekana...ila Simba SC walikuwa na tabia ya kuridhika mapema sana.

Wakipata goli hata moja wanajiona wamemaliza game, na wanacheza kwa kurilax wana sahau kuwa kuna Mayele, sasa hiyo tabia wameiacha. Na this time wakipata goli moja, wata force kupata lingine na lingine tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom