Simba anateseka mikumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba anateseka mikumi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uliza_Bei, May 30, 2012.

 1. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Wakuu heshima mbele.

  Nimesikitika kuona hii picha ya simba wa Mikumi akiteseka na hii ni siku chache tu tangu waziri wa maliasili awasimamishe viongozi wa Serengeti national park. Kuna uzembe wa hali ya juu kwa Park warden wengi katika mbuga zetu na hii ni kwasababu wamepewa madaraka makubwa na wanajiona kama miungu watu hata hawajali wanaingiza ngapi achilia mbali wanapoteza ngapi kwa uzembe wao.

  Hawahawa wameua kitengo cha daktari wa mifugo katika mbuga kwa kukifanya kiwe chini ya Ikologia (Ecology) wakati ktk mbuga zote anzia za South afrika hata hapa Kenya Daktari wa mifugo wana ripoti moja kwa moja kwa Mkurugenzi mkuu ili wasicheleweshwe katika kuhudumia wanyama. Waziri Kagasheki nakuomba mulika idara hizi na uhakikishe idara hii nyeti itenganishwe.

  Halafu bahati mbaya nasikia daktari wa Mikumi national park wamemfukuza kazi kisa kutofautiana na Chief park warden wa Mikumi na majungu

  Picha angalia :: IPPMEDIA Simba anateseka mikumi
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Old soup, na imeshachacha.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Nasikitishwa sana na mtu anayejari na kumuonea huruma mnyama eti anateseka wakati Watanzania kibao wanakufa kwa utapiamlo, huu ni uvivu wa kufikiri kwa 100%
   
 4. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Nadhani ndugu wewe ndio umekuwa mvivu wa kufikiri. Sasa kwani daktari wa wanyama ndio anawatibu binadamu? We hujui kuwa uwepo wa hao simba pia ni muhimu kwa kuwa unatupatia fedha za kigeni (utalii) zitakazotusaidia kuendesha sekta nyingine ikiwemo ya afya?
  Hoja ya Reginamduma haina uhusiano na vifo vya utapiamlo. No correlation at all!
   
Loading...