Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
JK amewaahidi wakaazi wa Simanjiro kuwarudishia ardhi iliyoporwa na wawekezaji wa TANZANITE ONE mara baada ya mwekezaji huyo kumaliza kuyachimbua madini yote ya TANZANITE yaliyomleta hapa nchini.
HAta hivyo, kulingana na takwimu zao wenyewe TANZANITE ONE uhai wa mgodi huo ni kati ya miaka 50 hadi 100 ikiashiria ya kuwa katika uhai wetu hatutaona ardhi hiyo ikirejeshwa kwa wamiliki halali.
JK hakutoa ahadi ya jinsi gani kama akifanikiwa tena kuendelea na kipindi kingine cha Uraisi ataboreshaje mapato yatokanayo na madini hayo hali ambayo inamaanisha anaridhika na makombo kidogo ambayo Halmashauri ya Simanjiro hutupiwa na mwekezaji huyo.
Kwa hiyo na kwa kifupi sana miaka mitano ya JK na CCM yake itakuwa "business as usual" na wala hakuna mabadiliko makubwa ya kisera au kisheria ili kufanikisha njozi ya watanzania wote ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA."
Hilo jimbo si la ole sendeka yule mbunge "machachari" ambaye hana mpinzani ama?

Unajua ccm sasahivi hawatoi ahadi tena, wanachofanya ni kulaghai watu. Kama huo mgodi uta-exist kwa miaka 50-100 ni kusema kwamba watu wa simanjiro wataendelea kukosa maeneo ya kuchimba madini au ardhi ya kufanyia shughuli zao kwa muda wa miaka takribani 80 ijayo. Kama mgodi umeanza kuchimbwa mwanzoni mwa miaka ya 90 hadi sasa ni takribani 20 kwahiyo, kikwete anaahidi kutekeleza ahadi yake baada ya miaka 80 na kwa namna yoyote ile haitarajiwi awe hai miaka 80 ijayo.
Kweli ccm ni waongo sana, na ahadi zao hazitekelezeki.
Umachachari autoe wapi pumbavu tu naye..JK hana cha kusema kwa wananchi na CCM wameshikwa pabaya yaani kwa dadkika hizi msuli ushawadondoka uko magotini...Kuinana kuuokota wanaogopa nyuma yao wako watu wa pwani ...hahaaaa
Vita ikitokea kama angola, rwanda,ivor coast, etc.. Ndio tutajua umuhimu wa democrasia na tatakuwa na maendelea ya haraaka mana tumeshindwa kuwatoa ccm