Simanjiro: James Millya vs Ole Sendeka

Jamani yote kwa yote nimeshitushwa na taarifa ya elimu ya mbunge wetu Sendeka....Div-0 ya form six???


Binafsi nimefarijika sana kama aliyosema Milya ni kweli kuwa Sendeka alipata Div-0. Hii ina maana moja tu, the guy is exceptional! kama anaweza kujenga hoja zenye nguvu na kutikisa bunge kiasi kile, kama anaweza kusimamia principle bila ya kuweweseka, kama anaweza kusimamia rasilimali za nchi kwa kiwango anachosimamia na kama anaweza kuongoza kwa kutoa michango bungeni yenye mashiko, then I will go for Sendeka badala ya wapuuzi waliojaa kwenye cabinet na PhD feki.
 
Mmmh! Siasa za siku hizi, mbona watu wazima wanalialia tu kama watoto wadogo?

Haya kuyasema ukiwa kwenye politics ni dalili za utoto.

Pole kijana, but you have to grow up.


Duh! kama hii mada imeweza kumtoa mama Ntilie pangoni ni lazima itakuwa kiboko. Usipotee hivyo Bibi.
 
Naona mawazo ya jumla ya wengi yanashindwa kuangalia vipengele vingine vinavyotia mashaka kama alivyosema Millya, IMEKAA KAAJE SHAHIDI MUHIMU WA MASHTAKA KUANDAA MAPOKEZI YA MSHTAKIWA?

Mnadhani hapo hakuna mikakati miovu iliyofanyika?
 
.
Jaman.Tuacheni uswahili sasa.
Elimu yake inahusikaje ni hiyo presentation yake.Mbona amejitahidi sana.
Ni yale yale ya Bongo ya kuangalia sana vyeti, kitu ambacho wenzetu waliayaacha muda mrefu.

Kikubwa sana kinachotusumbua sana watanzania na pengine waafrika ni ile ya kujiita mimi ni msomi au mimi nimesoma chuo fulani.

Inanikumbusha nilipmaliza masoma yangu nchini uingereza na kuanza kutafuta kazi.Kila nikienda kwenye interview, hao waliokuwa wananifanyia intavyuu,walikuwa hawana haja ata na vyeti vyangu zaidi ya kuviangalia sekundi moja na kunirudishia.Mambo mengine nikukupima uwezo wako na post iliyotangazwa

Makampuni mengi sana nchi uingereza unakuta yanaongwa na vijana waliomaliza sekondari na wanafanikiwa.

Pungzeni kasumba za kusema sijui kasoma mpaka wapi au chuo gani.
 
Mimi mambo ya division... CV.... Phd.... kwa Tanzania naona ni kama makaratasi tu... Hayaonyeshi usomi wa mtu...
 
afande, presentation ya milya ni poor kulingana na alivyojitambulisha kwamba amesoma sheria na ana degree mbili na ni mwanahrakati... asingesema hivyo watu wasingeishangaa hiyo release!!

Hayo ya interview ni kawaida hata ingekuwa wapi.. kwani wao wana mitambo ya kucheki authenticity ya vyeti? wao focus ni namna unavyojibu maswali

MILYA KAFULIA, AMEANZA MIPASHO NA YEYE
 
Naona mawazo ya jumla ya wengi yanashindwa kuangalia vipengele vingine vinavyotia mashaka kama alivyosema Millya, IMEKAA KAAJE SHAHIDI MUHIMU WA MASHTAKA KUANDAA MAPOKEZI YA MSHTAKIWA?

Mnadhani hapo hakuna mikakati miovu iliyofanyika?

Mbona kuna mashahidi walioenda kumpa pole Millya kwa kushindwa kesi, kuna ubaya gani wengine wakienda kumpongeza Sendeka kwa kushinda kesi.
 
Mbona kuna mashahidi walioenda kumpa pole Millya kwa kushindwa kesi, kuna ubaya gani wengine wakienda kumpongeza Sendeka kwa kushinda kesi.
watanzania tuna memory fupi sana... Milya anasahau kwamba sisi ni wanafiki? amejifunza kwa vitendo sasa
 
Akiwa mkuu wa utawala wa UVCCM alipata tuhuma za kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wakati huo na sasa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ndugu Guninita

Bwana James Millya,
Please go back through your facts, as I still remember, Mkuu wa utawala wa UVCCM kipindi cha Guninita alikuwa Comrade Habil Lazaro Londo (RIP). Namkumbuka huyu Comrade kwa sababu alikuwa mwalimu wangu wa siasa jeshini, kabla sijakutana naye tena kwenye siasa akiwa mmoja wa makada muhimu wa UVCCM na CCM katika kipindi kile cha mpito.
 
Millya ni mfa maji sasa anatapatapa, mara Ole Mangi mara mchezo mchafu wa Sendeka. Si akubali kushindwa tu, Millya akumbuke huwezi kuingia vitani kama hujui nguvu ya adui!
 
Duh! kama hii mada imeweza kumtoa mama Ntilie pangoni ni lazima itakuwa kiboko. Usipotee hivyo Bibi.

Mafuchila,
Asante. Mada hii haikunitoa pangoni bali nimehuzunika kuona kijana wa Kimasai 'Morani' anaweza kulialia kwenye vyombo vya habari badala ya kuwa ngangari!

Kwa taarifa yako ni msomaji mzuri wa mada za JF lakini nguvu ya kuchangia kama ilivyokuwa kule Nyezi.com imepungua. Utu uzima na ustaafu tatizo! Lakini tuko pamoja katika kusukuma gurudumu....sijui ni la nini siku hizi maana zamani lilikuwa gurudumu la maendeleo ya watu wote!
 
De Novo, umesema kila kitu, mwenye masikio na asike, hii tayari imeshakula kwake Ole Milya, ameshateleza na asipoangalia ataanguka kabisa, bora atafute mahali pa kujishikiza ili aweze kusimama tena.
 

Hila hiyo dissertation yake imenifurahisa hasa kwenye acknowledgement na recommendations, haina tofauti na nyuzi yake iliyoko hapa.

https://www.up.ac.za/dspace/bitstream/2263/5843/1/millya_2007.pdf
 

Hivi Sendeka hakuwepo katika kikao cha bunge kilichofunga mjadala wa Richmond?
 

Kwa hiyo amewaambia uongo watanzania. Huo ndio utetezi wake anaopanga kwenye rufaa yake, ya nini sasa kutoa nondo zake hata rufaa hajakata? Halafu kwa nini hakuutumia utetezi huo ili ashinde kesi ya awali? Kama aliutumia na haukukubalika maana yake si utetezi halali.
 
Maneno ya Mkosaji haya. Kama yeye Millya aliona mahakama ni sehemu pekee pa kupatia haki na akapeleka ushahidi kwenye vyombo vya dola kuwa Sendeka amefanya kosa la jinai dhidi yake, alitakiwa kukusanya ushahidi wa kutosha ili mahakama ithibitishe kuwa kweli sendeka alifanya kosa hilo, Kitu ambacho yeye kama shahidi wa kwanza ameshindwa kuinesha mahakama.

Suala la kukata rufaa si la lake ni suala la Jamhuri, anapopita na kuanza kulalamika ovyo anazidi kuifanya mahakama ione kuwa Ole Milya ana "MALICE" dhidi ya Ole Sendeka na hivyo anataka kuitumia mahakama kutekeleza nia yake hiyo. Yeye angekaa kimya tu kuhusu kesi maana hiyo ndiyo imetoka.
 
.

Mzee Mengi na Media Zake ni kikwazo kikubwa sana katika demokrasia ya nchi hii.Huyu mzee kuna siku yatakuja kumpata ya kumpata.

Tatizo kubwa hapa jf,wengi ni washabiki na hawamjui huyu mzee kwa undani alivyo yeye na media zake..

Na tatizo kubwa la ninyi mnaomjua Mengi vizuri zaidi ni kuwa hamtaki kutuletea habari za undani (za kuthibitishika) kuhusu mfanyabiashara huyo na media zake.Until you do that,baadhi ya wana-JF wataendelea kutimiza haki zao za kibinadamu kumheshimu (wewe unaita kushabikia) Mengi kutokana na wasifu uliopo.
 
Ni walewale tu wanaonunuliwa ili kuwapinga wanaopambana na mafisadi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…