Simanjiro: Afa kwa shoti ya umeme baada ya kutamani waya ulioshikilia nguzo ya umeme

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Umeme wa REA ni muhimu kwani utaleta maendeleo vijijini. Lakini Elimu ya kutosha yafaa itolewe kwa jamii ili kuwaepusha na athari zinazoweza kujitokeza!

Morani mmoja Simanjiro alitamani waya unaoshikilia nguzo ya umeme ardhini. Aliukata chini, na kuanza kuukung'uta ili udondoke akatengenezee bangili za miguuni & mikononi.

Wakati akiwa kwenye juhudi za kuuchukua, waya ule uligusana na nyama za umeme na kumsababisha morani kupoteza maisha baada ya kupigwa shoti.

1469795592039.jpg

1469795613606.jpg
 
Pumzika salama Morani..
Kuna kila sababu ya kuelimisha jamii kuhusu vitu vya hatari..
 
Kikawaida hizi waya kabla ya kufika chini hapo katikati huwa zinainsulator ili ikitokea case kama hii umeme usifike chini, sasa kwa nini huu waya haukua na insulator, ni uzembe wa shirika la umeme
 
Alishaukata chini hivyo akawa anautikisa ili uachie juu kumbe katika kuukung'a akaupiga waya wa juu wenye moto

Alishaukata chini hivyo akawa anautikisa ili uachie juu kumbe katika kuukung'a akaupiga waya wa juu wenye moto
mstim.jpg
nifahamishe vizuri sababu kuanzia hapo kwenye red hadi kushuka chini huwa umeme haupiti sasa imekuwaje mpaka umeme umemuua?
 
Duuh, huu ni umeme mkali sana. Nadhani utakuwa 11,000 Volts
Huu tunaotumia majumbani umepozwa mara hamsini na ni around Volts 220!
 
Back
Top Bottom