Morogoro: Mtu mmoja afariki baada kupigwa na shoti ya umeme akianika nguo kwenye waya

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
d212e917b8446263ff6bccf9012699b4.jpg
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rahimu Haruni (30), mkazi wa mtaa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro amefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akianika nguo kwenye waya uliofungwa kwenye nyumba ikisadikiwa kuwa na hitilafu kwenye mfumo wa umeme.

Wananchi wamelitupia lawama shirika la umeme TANESCO mkoani Morogoro kwa kushindwa kutatua tatizo hilo licha ya kudai kutoa taarifa Ofisi za TANESCO bila mafanikio.

ITV imeshuhudia mwili wa kijana huyo ukiwa umelala chini huku mafundi wa TANESCO wakizima umeme na kuanza uchunguzi wa tatizo hilo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi kwa kuhofia wananchi kujichulia sheria mkononi.
 
Poleni wote waliofikwa na msiba huo. Mungu amlaze pahala panapo lazwa wema. Ameen
 
Morogoro: Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Rahimu Haruni (30) ambaye anaishi mtaa wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro amefariki dunia leo wakati akianika nguo kwenye waya uliofungwa ndani ya nyumba hiyo baada ya kupigwa shoti ya umeme.

Taarifa zilizothibitishwa zinadai kuwa nyumba hiyo ambayo kijana huyo amepigwa shoti ilikuwa na tatizo la umeme ambalo lilitolewa taarifa kwenye shirika la Umeme TANESCO mkoa wa Morogoro lakini tatizo hilo lilishindwa kutatulia na TANESCO mpaka leo ambapo shoti hiyo imesababisha kifo cha kijana huyo.

Baada ya kutoa kifo cha kijana huyo kabla ya mwili wake kuondolewa ndipo mafundi wa TANESCO walipofika na kuzima umeme kwa ajili ya kuanza uchunguzi wa tatizo hilo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwa kuhofia wananchi kuchukua sheria
 
Alikuwa anaanika nguo kwenye waya wa umeme?? Au Mimi sijaelewa
Duuh
Waya uliofungwa kwenye nyumba wa kuanikia nguo una hitilafu kwenye mfumo wa umeme (yaani waya wa kuanikia nguo na mfumo wa umeme kwenye nyumba hiyo kuna tatizo) ndo maana walitoa taarifa TANESCO

Sijui umenielewa hapo au kunipata?
 
Waya uliofungwa kwenye nyumba wa kuanikia nguo una hitilafu kwenye mfumo wa umeme (yaani waya wa kuanikia nguo na mfumo wa umeme kwenye nyumba hiyo kuna tatizo) ndo maana walitoa taarifa TANESCO

Sijui umenielewa hapo au kunipata?
Asante kwa kuniekewesha mkuu.
 
Back
Top Bottom