Simama tetea maslahi ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simama tetea maslahi ya nchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Apr 27, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 27, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Katika miaka ya karibuni Tekinologia ya habari na mawasiliano imekuwa kwa kasi sana kukua huko kumewezesha watanzania wengi kujiunga na forums au mitandao mengine mingi tu kwa ajili ya kutoa maoni yao au kuweka makala na mabandiko mengine ambayo wanafikiri jamii inaweza kujifunza kutokana na kile walichoweka .

  Kwa hili ni pongezi kwa serikali iliyopita na hata hii ya sasa kuhakikisha kila mtanzania anapata nafasi za kuwasiliana na yeyote anayetaka bila kuvunja sheria za nchi au za nchi ambapo mtu wa pili yuko huyo anayewasiliana nae na wataalamu kadhaa wamejitokeza katika kutengeneza au kusajili mitandao yao kwa ajali ya kupashana habari za hapa na pale zinazoendelea nchini .

  Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinaendelea sasa hivi ambavyo vinatia mashaka sana kuhusu maendeleo ya tekinologia hii na watu wanavyotumia tekinologia hii kwa ajili ya kufanikisha mambo yao kibinafsi haswa ya kisiasa .

  Juzi hapa tumeona sakala la kuvujishwa siri za serikali bungeni mmoja wa wabunge akaendelea kusisitiza ataendelea kutoa siri hizi haogopi chochote – hizo nyingi zinapatikana katika mifumo ya karatasi na michache imo kwenye mifumo ya Mtandao ambayo ni secure zaidi kwa mtu kuweza kuchukuwa au kuiba

  Siri zinavujishwa au kuuzwa na watu walipewa dhamana ya kulinda siri na nyaraka zingine za serikali , tujiulize watu hawa ambao wameajiriwa kwa kazi hiyo mikataba yao ya kazi ina vipengele vyovyote vinavyohusu utunzaji wa siri za serikali na huwa wanaweka sahihi mbele ya wasimamizi wao wa kazi je wasimamizi wao wa kazi huwa wanafuatilia au hata kuwatega kuhakikisha wanafanya kazi zao kiufasaha ?

  Ndio siri nyingi ziko katika mfumo wa karatasi ni rahisi kwa mtu kwenda tu kutoa photocopy hata hapo hapo offisini au kufanya scanning tu na kumtumia mwenzake kuna swali lingine hapa , hawa wasaidizi wa ofisi hizi ambapo siri huvuja watafuatiliwaje kuhakikisha vitu hivi havitokei tena ?

  Ninavyojua katika baadhi ya nchi mahakama ndio inaweza kuamua kama baadhi ya nyaraka ziwekwe wazi kwa jamii kama suala hilo likifika katika vyombo vya sheria ila unapoamua kuhonga mtu akupe siri Fulani kwa ajili ya maslahi yako binafsi au kisiasa hayo ni makosa .
  Pia kama siri hizo zilikuwa katika mfumo wa komputa na kuhifadhiwa vizuri halafu zikavuja basi anayehusika na usimamizi wa mfumo huo wa komputa wa kuhifadhi nyaraka anawajibika kwa namna moja au nyingine unapo chukuwa kitu chochote kwenye computer au kuhamisha au kufanya lolote haswa linalohusu data basi ujue kuna kumbukumbu hubaki kuna jinsi ya kudhibitisha hili – wasimamizi wa server hizi na hizi database hizi wasuatiliwe kwa karibu zaidi kutoka katika vyombo binafsi kuhakikisha kazi inatendeka .

  Kwa kumalizia mwanzoni mwa mwaka huu kulikuwa na mkutano fulani uliohusu mambo ya Egovernance ulifanyika katika hoteli ya Movenpick , mimi nilikuwa mmoja wa wahudhuriaji wa mkutano huo , kilichozungumzwa pale kikubwa ni kuhakikisha kunakuwa na chombo kimoja kitakachukuwa kinasimamia mawasiliano yote ya mtandao yanayoingia na kutoka nchini .

  Kuna mtu pale aliyejitambulisha kwamba yeye ni msimamizi wa chombo Fulani ila akasema kampuni nyingi na mashirika bado hayajajiunga nao ili waweze kupitisha mawasiliano kwao – basi serikali inabidi ifanye kazi ya ziada kulazimisha kampuni hizi na mashirika haya kupitisha mawasiliano yao yote ya mtandao katika chombo hicho

  Kwa kufanya hivi naamini tukio kama la kudhalilishwa raisi lililotokea wiki iliyopita yanaweza kupungua na hata kupunguza wateja katika tovuti hiyo kwa sababu itakuwa haitazamwi kutoka nchini Tanzania kama serikali ya uchina inavyofanya katika kudhibiti mawasiliano yake .

  Pia tovuti zote zinazohusu mambo ya Tanzania au chochote kinachohusu tanzania zikaguliwe kuhakikisha hakuna taarifa za uwongo au uchonganishi wa namna yoyote ikidhibitika hivyo basi tovuti hizo zizuiwe kuangaliwa kutokea Tanzania labda hao wa nje tu

  Ndugu zangu lazima tusherikiane na serikali yetu kufichua wale wote wanaouza siri za serikali au kuzitoa kwa nia mbaya ya kuharibu jina la nchi na viongozi wetu hapo hapo lazima tushirikiane katika kujenga nchi yetu bila kujali tofauti za kisiasa au kidini .

  Usiogope kufichua Yule ambaye unahisi anafanya mambo ambayo hayana tija kwa taifa , kuanzia makazini , mitaani , mashuleni , vyuoni na popote pale watu wanapoishi ukifanya hivyo utakuwa umeokoa mengi sana .

  Popote pale ulipo hakikisha unatetea maslahi ya nchi yako , uwe mzalendo kwa njia yako , fanya jambo Fulani kwa ajili ya maslahi ya nchi yako na jamii yako wale wanaosema nchi imeoza ni mitazamo yao ya kisiasa nchi haijaoza bado inahitaji changamoto mpya haswa za vijana

  HII NCHI NI YETU SOTE LAZIMA TUILINDE NA KUITETEA KWA NJIA ZOZOTE ZILE
   
 2. 911

  911 Platinum Member

  #2
  Apr 27, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Acha upofu wewe,kati ya hayo yote yaliyoanikwa huku yakiwa na muhuri wa 'confidential' je ni yepi yasiyo na harufu ya WIZI na ufujaji wa mali za waTanzania.Haya mawazo mgando uliyonayo ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo,wakati tunazinduka na kutoka kujikwamua hapa unakuja na wazo litakalotufanya tuendelee kupiga marktime katika uozo huu.Shame on you for taking time writing this bollock.Damn!
   
 3. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,729
  Trophy Points: 280
  Ahsante,
  Laiti huyo ndugu angejua kuwa kinachoitwa 'siri za serikali' ni nyaraka za wizi, ikiwa ni pamoja na mikataba ya hovyo, tenda hewa, kupeana vyeo kirafiki na uchafu mwingineo.
  Nadhani huyu mwandishi ni wakala wa dola linaloanguka/linalokaribia kubadilishwa.
   
 4. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hiki ki nchi jamani? Mtu mzima anasimama anatetea upotofu? Lakini tutaonewa mpaka lini jamani?
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Apr 27, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Ninachosema mimi kuamua tu kufichua siri au kuuza siri za serikali au za
  sehemu zako za kazi kwa ajili ya faida binafsi au za kisiasa hayo ni makosa
  kwanini suala hilo lisifikishwe katika vyombo vya sheria ndio sheria
  ichukuwe mkondo wake ndio sasa waamue kama ziwekwe wazi au la ?

  hao wote wanaovujisha siri hata dr slaa hajawahi kudhubutu kwenda katika
  vyombo vya sheria kushitaki apewe siri hizi kwa faida ya ummah yeye anaiba
  na wenzake anazurusha au kubwatuka sasa hii ndio nini huu sio ustaarabu sio
  democrasia hii ( HIO NI SAWA NA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKATI VYOMBO
  VYA SHERIA VIKO )
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hakuna mtu anayeuza siri hapa , hapa tunawazalendo wenye uchungu wa nchi yao ambao wanaaccess ya hizo nyaraka na uzalendo wao ndio unawafanya wawapelekee watu wanaoweza kuzitumia nyaraka hizo kwa manufaa ya nchi yetu!! hakuna wizi wa nyaraka hapa; acheni ujinga wenu .
   
Loading...