Siloam church

Ingia katika maombi upate majibu maana maswali yako sidhani kama humu utapata majibu sahihi...
 

Uwe unauliza kwanza ndugu yangu! BWAKATA sio dhehebu bali ni Taasisi ilo kwanza lazima uielewe, pili, Hao mabohora na makadiani sio waislam kwasababu hawafuati mafundisho ya uislam na tatu, Answar Sunah sio dhehebu bali ni sifa ambayo kila mwislam anatakiwa awe nayo,(Maana yake ni kunusuru ama kuendeleza suna za mtume,) kwani hawa ni waumini wanaouhuisha suna za Mtume Muhammad (s.a.w) na kila kitu wanachokifanya kipo ndani ya mafundisho, na hata huo unaouita utofauti kipindi cha kufunga ama kufungua, kila kundi liko sahihi kwa maana limefuata mafundisho, mf. mafundisho yanatoa ruhusa kufungua tunapouona mwezi, ama kusikia kwa ushahidi usiokuwa na shaka, ama kukamilisha siku. hivyo ukifuata moja kati ya hayo utakuwa haujakosea. Umeelewa sasa.
 

Waislamu wa la boko haramu na waislamu wa Tanzania wana imani moja? Kama wako tofauti tunasema wale wana madhehebu yao ndani ya uislamu tofauti na dhehebu lingine la uislamu lililoko Tanzania.Dini moja,mtume mmoja imani tofauti kwenye vipengele fulani.Vile vipengele tofautishi ndivyo vinaunda dhehebu.

Dhehebu ni kundi linaloamini tofauti na dhehebu lingine yaweza kuwa ndani ya eneo moja.Sasa kidini mtu mwingine akisema Ramadhani fungua jumapili mwingine akasema jumatatu hapo wataalamu wa dini husema kuna madhehebu mawili tofauti ya dini moja.Kuna lile dhehebu la fungua jumapili na lile la fungua jumatatu.Na hata kukitokea ugomvi wasajili wa dini serikali nyingi huamua kusajili watu wa aina hiyo kama dini tofauti na kila mmoja kumpa hati yake ya usajili.
 

Aliyekuambia hayo ni Makabila ni nani...??? Hebu wacha kukurupuka na vitu vya ajabu......KAma hujui uliza maana ulichoandika ni kichekesho..
 

Muislam ni muislam tu, Na mafundisho yake ni Qur-an, Hadith na Sunnah za Mtume Muhammad (S.A.W), kundi ni moja tu, nyumba ya ibada ni moja tu, Hao wanaojitambulisha kwa madhehebu mf. mimi kadiani, mimi ahmadya, sijui mimi bohora hao si miongoni mwa waislam kwani hawafuati mafundisho ya uislam wao wanamafundisho yao na majumba yao ya ibada. Hivyo ndivyo ilivyo. Natumaini umelewa sasa.
 
Alimchezea mungu kisha mungu akamuonyesha ukuu wake
Kujitangaza yeye ndiye aliyemuua shetani mwaka 2008 hapo sasa alizidi. Hakujua hata Musa hakugusa Kanani kwa kosa la kupiga chini fimbo na kuwaambia wana Israel nimewapa maji badala ya kusema Mungu amewapa Maji.
 

Huo ni mtizamo wako ambao inabidi niuheshimu maana ni mtizamo wako ambao una hati miliki nao.Akili ni nywele kila mtu ana zake.Kukupinga kwenye mtizamo wako nitakuwa nakuonea.Ni haki yako kuwa na mtizamo huo japo sikubaliani nao na mimi kwa mtizamo wangu.Tukubaliane kutokubaliana kwenye hili.
 

tuko huru na dhambi,Yesu katuweka huru,dhambi haipo maana yesu amelipa garama zake.

Damu ya yesu imetutakasa kabisa na kutuweka huru,Yesu katupa uhuru wa kufanya chochote.

Ukisema kuna dhambi uniambie Yesu alikuja kufanya nini?

Naupenda ukristo kwa sababu moja tu nayo ni kwamba zambi zangu zote zilishabebwa na Mtu mmoja anaitwa Yesu hivyo niko huru.
 
Huko nikujidanganya...... maandiko yanasema baada ya kifo ni hukumu.Sasa kama hakuna dhambi hukumu ya nini?

Hukumu kwa wale wasiokubali kama Yesu alibeba dhambi zao.

Sisi tunaomkubali Yesu hatuna hukumu yoyote maana Yesu alishajitoa kubeba dhambi zetu.

Biblia inasema ukimkubali mwana unakua haujahukumiwa,ukimkataa unakua umehukumiwa.

Hukumu ni kwa wale wasiomkubali yesu.
 
Hakuna kutoposha,huo ndio ukweli,hakuna dhambi duniani. kama kuna dhambi yesu alikuja kufanya nini? Labda uniambie kwamba yesu alikuja kutalii.

Hebu twende na maandiko mkuu...

Kamata hii
1 Yohana 1:8 "Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani mwetu"

Sasa Mkuu hebu nikuulize unajua maana ya TOBA....??? Kwanini twahimizwa kufanya toba kila siku ikiwa dhambi haman Duniani...???

Vipi Yesu alopowaambia wafuasi wake kuwa hakuna asiye na dhambi ila Baba yangu wa Mbinguni...??
 

Huu sio mtazamo wangu ndiyo mafundisho yanavyotaka, labda nikushauri kitu, jaribu kuwa unasoma soma mambo ya dini tofauti naamini utagundua kitu tu, kwani dini si jambo la kurithi bali ni kuthibitisha kile unachokiamini kama ni sahihi au la.
 

asante kwa ufafanuzi mzuri...nimejifunza pana watu wanabisha tu bila kujua...
kama dhambi hakuna...kitabu cha ufunuo ni cha kazi gani?!!
pana mtu mmoka alikuwa anasema chochote unachambiwa na mchungaji au mtume nk ni lazima umuulize maswali kama kwa nini+kivipi nk na kukaa tu kama mfu.

kuna haja ya #unknown aje na andiko kitakalo justify hayo madai yake. kwamba hakuna dhambi duniani.

Yesu amekuja kutoa second chance (nafasi ya upendeleo) ili watu tutubu.
 

so wamaanisha waliokubali hayo maandiko usemayo hata wakitenda maovu hukumu hawahusu?!
 

Yesu aliyasema hayo kabla hajafa,alipokufa tu dhambi ikaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…