Sisi alikuwepo ambae mashetani yalimpanda akachukua nguo zote akataka piga moto.
Mwingine haogi, hafui nguo zake muda wote mtandio.
Mwingine alikuwepo mwizi huwezi amini aliiba vitu nikiwa nimelala wakishirikiana na wamasai afu wote wakaondoka.
Mwingine anavuta sigara.
Ila mmoja alikuwa msafi sana anaoga, kuvaa navaa vizuri sana hivi sasa anamalizia diploma yake ya nursing
Usiombe kukutana na HG mwizi, utalia, kuna mmoja huyo, dada swaiba, nililetewa na babangu mdogo, binti alikuwa anaoneka muislamu safi, mzuri wa sura na umbo, lol! Mtoto aliiba,unajua kuiba? kwani aligusa kila idara kuanzia pichu hadi mapazia, nguo za mtoto, za husband yaani alihakikisha amegusa kila sehemu hadi midoli, jamani huyu binti sitakujaga kumsahau, tshirt zenye nembo ya ofisi alizoniibia ndo zilisababisha nikampata.
Niliambulia vitu vichache tu katika alivyoviiba, alikaa police central siku 3, nikawaambia polisi sihitaji hata kumuona mtajua jinsi mtakavyomrudisha kwao, niliwaelekeza nilikomtoa, polisi wakamsafirisha kwa warrant, aliposhuka tu kituoni polisi wa hapo wakampokea wakampeleka hadi kwa babake, mwaka jana nilienda huko kwa babangu mdogo, binti alifukzwaga kwao baada ya kurudi kwani babake ni shekhe, anadai kitendo alichofanya cha kuiba kilimuabisha sana, nowdays ni changudoa tu maskini.
Nilikuwaga sijui kufunga chumbani, tangu wakati huo binti akanifundisha kufunga room kila ninapotoka kwenda kazini japo ni kazi kweli kweli
Hahahaaaaaaaaaaaaaaa....hii kali kuliko. Yaani wao ndio walikuwa mahousehelp wake!! Yeye kazi yake ni kulala na kuhudhuria vikao...Dah! Mungu atusaidie tu kuhusu hawa watu.
dah! nimeipenda hii mada mana hawa watu wana vituko yataka uvumilivu kuishi nao
mimi kuna mmoja alikuwa hali chakula cha usiku tumekaa naye miaka 4 lakini hata siku moja
hajawahi kula nilikuwa namshangaa tu
mwingine naye ulikuwa ukimtuma dukani au gengeni kama kumefungwa anakaa chini anamsubiri
mwenye duka au genge mpaka aje ndo anunue ulichomtuma
huyu mwingine naye alikuwa mtu wa mood siku akiamua haamki kufanya kazi ukimuuliza
anakwambia kazi nilizofanya wiki hii zinatosha ila alikuwa anapenda kufagia uwanja yeye muda wote na fagio loh!!!!
hilo la kuoga na kufua nguo zao naona ni janga la kitaifa mana mpaka uwakumbushe
haaaa
mbona anatudhalilisha hivi
haa haa huyo aliyekuwa anapenda kufagia uwanja alikuwa mngoni nini? maana sie wangoni uwanja ndio kila kitu yaani uwanja utakuta msafi 24/7, ndani mmmhmmmh!!!
kipindi niko sekondari form one..house gal wetu alifanikiwa kuhamisha vitu vyangu,alibeba nguo zote,chafu na safi...nikabakiwa na uniform nilizokua nimeenda nazo shule....sitasahau
house gal aliefata ye akatoroshwa na jirani....kwa ahadi ya kupelekwa kuolewa..yalimshinda akarudi..akakuta tayari yupo mwingine..ambae tuko nae nyumbani almost miaka 6 saivi
Sometime huwaga najiuliza are they serious? Haya ni mambo ambayo nimejionea kwa wadada wangu wa home. lols.
1. Kuweka nguo na viatu kwenye fridge bovu.
2. Kutengeza juice ya passion kwa kublend kila kitu. Yes. Aliosha tu akatumbukiza kwenye blender. Tukawa tunajiuliza huu wekundu umetoka wapi. Tulipoenda kwa wakwe akawatengezea hivyo hivyo. Siku nimeenda wakaniomba nitengeze juice kama mtego. Lols. Ndo wakaniambia flani alitengeza hivi na hivi. hahaaa.
3. Kujaribisha nguo zangu na viatu, wigs etc na kujipiga picha.
4.Kuna mmoja alikuwa hapendi wageni, so mtu akija kuniulizia anasema sipo. Sasa nikaja kugundua much much later watu mtaani washanimaindi bila mi kujua.
5. Kuna mmoja alikuwa anaenda kunyonya maziwa directly kutoka kwa ng'ombe wa jirani. Aisee huyu I fired immediately.
6. Kuna mwingine alikuwa anapanda ukuta kwenda kwa jirani kuiba machungwa. Sikujua mpaka siku dirisha limevunjwa. Kumbe walikuwa wanamrushia mawe kama ka nyani. lols. I was furious. Aibu zingine bwana!! Kama vile siwezi ku afford chungwa?!
&. I had another one kuoga kwake mwiko!! Halafu kipindi kile I was so so busy. Nikawa siwezi kumfatilia. Nilipokuja kustuka ikabidi nim force aoge. Wapi? Atajipaka majo usoni mikononi na miguuni. Atamwaga maji ukutani weee.
9. Nilipoenda kujifungua house help wangu aliita bf wake wakaniibia mandoo ya rangi, mafeni ambayo hayakuwa yamefungwa, maboksi ya tiles etc etc. Damn!!
10. Kuna mmoja ambae mtoto wangu alikuwa anamuogopa kweli. Nikitoka kazini nakuta mtoto kwenye kona amejikunyata. Back then kalikuwa ma miezi 9. He was gaining weight na wakwe walimpenda sana. But siku ya siku akamwambia mtoto 'shenzi wewe mamako yupo sikufanyi chochote'. I told her to leave immediately.
Haya, wewe yamekukuta yapi?
Bora uoe tu nijue moja!!Fuatilia utaona huyo miss neddy anavo choke !!!!!
Kwani kama ni kumuoa naye si dini ruksa au !!!????
kwetu..kwa baba yangu na mama yangu
Okay nlshangaa kidogo
Fuatilia utaona huyo miss neddy anavo choke !!!!!
Kwani kama ni kumuoa naye si dini ruksa au !!!????
Huyo aliyekuwa anaenda kunyonya maziwa ya ng'ombe wa jirani ni kiboko ya wote!
Usiombe kukutana na HG mwizi, utalia, kuna mmoja huyo, dada swaiba, nililetewa na babangu mdogo, binti alikuwa anaoneka muislamu safi, mzuri wa sura na umbo, lol! Mtoto aliiba,unajua kuiba? kwani aligusa kila idara kuanzia pichu hadi mapazia, nguo za mtoto, za husband yaani alihakikisha amegusa kila sehemu hadi midoli, jamani huyu binti sitakujaga kumsahau, tshirt zenye nembo ya ofisi alizoniibia ndo zilisababisha nikampata.
Niliambulia vitu vichache tu katika alivyoviiba, alikaa police central siku 3, nikawaambia polisi sihitaji hata kumuona mtajua jinsi mtakavyomrudisha kwao, niliwaelekeza nilikomtoa, polisi wakamsafirisha kwa warrant, aliposhuka tu kituoni polisi wa hapo wakampokea wakampeleka hadi kwa babake, mwaka jana nilienda huko kwa babangu mdogo, binti alifukzwaga kwao baada ya kurudi kwani babake ni shekhe, anadai kitendo alichofanya cha kuiba kilimuabisha sana, nowdays ni changudoa tu maskini.
Nilikuwaga sijui kufunga chumbani, tangu wakati huo binti akanifundisha kufunga room kila ninapotoka kwenda kazini japo ni kazi kweli kweli
Acha kazi ukae nyumbani kulea familia huo ndo ushauri wangu swaiba.