Silly season part II si ya kukosa

Status
Not open for further replies.
Dec 11, 2010
3,321
6,328
Ukumbi wa Gwajima unatarajiwa kufurika watazamaji wa movie kali ya silly season part 2 inayo tarajiwa kuruka hewani muda wowote katika kipindi cha masaa kadhaa yajayo.

Miongoni mwa Sterling ambae alikaribia kufa kwenye maua kabla ya kujisalimisha mbele ya wakovu wa jeshi la wana Gwajima tayari yuko mikononi mwa wanajeshi eneo la Kova.
Eneo la Kova litakuwa limetega macho na masikio kusikia nini kitakuwa kimesheheni kwenye filamu hiyo. Inasemekana usingizi utakuwa wa mang'amung'amu sana kwa wakazi wa eneo la kova wakiwaza filamu hiyo.

Mhanga wa filamu aliyeoko kusini mwa Afrika ndio mwenye kifuniko cha siri kinacho tambua muandishi wa script na location manager aliye chagua eneo. Hataweza kuwepo kwenye part 2 ya filamu hii ila wengi tunategemea akirudi salama ataweka sawa upepo wa liwalo na liwe na huenda akafyatua part 3 ambayo bila shaka itaitwa silly season hidden with truth.

Kuna wasiwasi kuwa yale madai ya eti baadhi ya wachungaji ni wauza unga huenda yakaibuka upya endapo filamu itakuwa na chengachenga kama mwangwi wa filamu hauta pendeza masikio ya watu wa eneo la kova, hii itakuwa kama kulipa kisasi endapo ile dhana ya kizungu ya Scratch my back, i will scratch yours kama itapuuzwa.

Mliopo Dar hii sinema siya kukosa. Vunjeni makabati muende gwajina sinema hall mkadhibitishe kuwa ni ukumbi wa tenzi za rohoni au ni location nzuri mpya kwa movie za kiintelijensia?
 
Nimeipenda hii mkuu, ngoja hayo masaa twayangoja kwa hamu, tujue wanapalilia au wanang'olea magugu
 
Atakuwa na ujasiri wa kucheza hii sinema kweli? Na ataichezaje, na kwa hiari au maelekezo maalum?
 
Akiamua kujinasua na tope kama kiongozi mkuu wa gwajima ataweza kuondokana na wingu lililotanda juu yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom