Silioni pengo la Niyonzima Yanga

Simba mbona amuongelei ubingwa au mechi za Yanga ndio ubingwa kwenu..WE ARE THE CHAMPIONS
Fungua thread nyingine Mkuu, kisha ndio tuanze kuongelea ubingwa. Mbona nyie vyura wagumu kuelewa hii thread inamhusu Niyonzima(Fundi) halafu wewe unataka tuongelee ubingwa.
 
Sio kwamba SIZITAKI MBICHI HIZI, kila ninvyoangalia sioni ni kwa
namna gani yanga itapata pengo kwa kumpoteza Haruna Niyonzima
Zifuatilie mechi za Yanga halafu katika hizo mechi akosekane Haruna
baada ya hapo zifuatilie mechi za yanga ambazo amekosekana Msuva
halafu urudi hapa utueleze.
mkuu unaweza kuwa sahihi. lakini siye wengine hapa ni akina Tomaso - tunataka uthibitisho kupitia takwimu!

so, kwa uchache fanya mlinganisho ufuatao kwa msimu uliokwisha:

- alicheza jumla ya mechi ngapi
- Yanga ilishinda/shindwa mechi ngapi alipocheza
- Yanga ilishinda/shindwa mechi ngapi ambapo hakucheza
- mlinganishe na viungo wengine wa Yanga kwa takwimu hizi:
a) magoli aliyofunga
b) pasi zilizozaa magoli (assists)
c) alikaba mara ngapi (successful tackles)
d) wastani wa umbali aliokimbia ndani ya uwanja

ni hayo tu mkuu!
 
Hawana jeuri ya kuongelea ubingwa hao matopeni. Mipango yao ya mwaka mzima ni kumfunga Yanga basi. Ufanisi wao kwa mwaka mzima hupimwa kwa kumfunga Yanga.
Na nyie mipango yenu ni ipi kwenda kutia aibu nchi yaan nyinyi ndo wamatopeni na subirini mbona ubwabwa mtaita baba
 
Miaka ya 90 Yanga ilifukuza wachezaji karibu wote na bado timu ilikuwa imara na madhubuti! Kile ndio kipindi kina Anwar Awadhi, Silvatus Ibrahim 'Polisi', Maarim Salehe 'Romario' na wengineo walipoibuka! Kwa hiyo kuondoka kwa Haruna ni fursa kwa wachezaji wengine kuonesha vipaji vyao!
 
Simba mbona amuongelei ubingwa au mechi za Yanga ndio ubingwa kwenu..WE ARE THE CHAMPIONS
Hapo ndipo wakina Aveva wanapowaweza hawa mambumbumbu wa mikiani usajili wote huu walioufanya sio kwa ajili ya ubingwa bali ni kumfunga Yanga na Okwi tena kesho ndio anakuja washawamaliza tayari hoi.
 
izitakimbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom