nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
RAIS Jakaya Kikwete amesema hakumteua Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu kwa sababu ya urafiki wao bali kwa sababu ya ufanisi wake.
Kikwete ameyasema hayo kupitia kitabu chake cha JK: A Political Biography, kitabu kinachoeleza kuhusu maisha yake ambacho sasa kinapatikana hapa nchini.
Kikwete ameelezwa kutoa maelezo haya mwaka mmoja baada ya tukio la kujiuzulu kwa Lowassa kufuatia kashfa ya Richmond ambayo ililazimu baraza lote la mawaziri kuvunjwa.
"Sikiliza. Ni kweli kwamba Lowassa ni rafiki yangu na nimemfahamu kwa muda mrefu. Lakini pia ninawafahamu watu wengi zaidi kwa muda mrefu, wanasiasa na wasiokuwa wanasiasa na sikuwachagua kuwa Waziri Mkuu.
"Nilikuwa natafuta mtu ambaye atafanya kazi kwa ufanisi na kutekeleza sera zangu. Lowassa alijitokeza vizuri kama mtu anayeweza kutokana na uzoefu wake," kitabu hicho kinamnukuu Kikwete.
Hii ni mara ya kwanza ambapo Kikwete anaeleza wazi wazi mahusiano yake pamoja na tathmini ya utendaji wa Lowassa, tangu kuibuka kwa kashfa ya Richmond.
Sentensi moja katika maelezo ya Kikwete inaonyesha mtazamo wake kwa waziri mkuu huyo aliyejiuzulu; "Lowassa alikuwa mmoja wa mawaziri wakuu wenye ufanisi mkubwa kabisa nchini."
Tafsiri ya maelezo haya ya Kikwete inaonyesha kwamba mwaka mmoja baada ya kashfa ya Richmond, rais bado alikuwa na imani na Lowassa.
Wakati Kikwete alipochaguliwa kuwa rais mwaka 2005, majina mengi yalitajwa kuchukua nafasi ya uwaziri mkuu ingawa la Lowassa lilitajwa zaidi kutokana na ukaribu waliokuwa nao viongozi hao.
Lowassa pia hakuchukua fomu kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, jambo lililotajwa kama kuonyesha azma yake ya kumuunga mkono mgombea huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa, walidai kwamba uamuzi wa Kikwete kumteua Lowassa ungekuwa na athari kubwa kwake kwa vile ukaribu wake ungeweza kuingia kwenye kazi.
Mara baada ya uteuzi huo, ndipo ilipoibuka dhana ya ‘serikali ya kishkaji' kutokana na baadhi ya watu waliotajwa kuwa maswahiba wa Kikwete, akiwamo Lowassa, kupata nafasi katika baraza lake la kwanza la mawaziri.
Kikwete na Lowassa walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1974 wakiwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wote wakiwa wanachama wa Umoja wa Vijana wa chama cha TANU ingawa Jakaya alikuwa katika mwaka wake wa mwisho wa masomo huku Edward akiwa mwaka wa kwanza.
Wote kwa pamoja walifanya maamuzi ya kujiunga na ajira katika chama cha TANU (sasa CCM) wakati huo mara baada ya kumaliza masomo yao, na wote walichukua fomu kuwania urais kupitia CCM mwaka 1995 wakiwa na umri chini ya miaka 50.
Source: Raia Mwema