Sikumbuki ushujaa ule nilipata wapi!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikumbuki ushujaa ule nilipata wapi!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ngongoseke, Jul 28, 2012.

 1. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Habari zenu wana Jf

  Leo nataka kushea pamoja na nyinyi mkasa flani ambao uliwahi kunitokea katika maisha yangu'

  Nikiwa nimetimiza miaka 26 miaka ya nyumba niliamua kuowa,kwa kweli mimi na mke wangu tulikuwa na maisha ya kawaida tu,tulikuwa tunaishi kwa furaha tu hapakuwa na tatizo kubwa bali ya kawaida tu,
  Baada ya miaka 2 katika ndoa tulipata mtoto wa kiume,
  Toka hapo tulipopata mtoto wetu hapo ndio nikaanza kuona mabadiliko ya wife,alikuwa busy sana muda mwingi kuchat na kutuma sms sikujua anatuma sms kwa nani lakini sana alikuwa busy,ikabidi nimuulize akanijibu vizuri tu kama hakuna kibaya anachofanya katika simu nikapotezea,
  Kadri siku zilivyokwenda ndio alizidi kuwa busy na simu mpaka siku 1 nikamwambia nina wasiwasi na matumizi yako ya simu sio mazuri,tulibishana sana ila mwisho nikamwambia nitakuthibitishia siku 1 niyasemayo,
  Basi siku 1 aliweka simu yake chaji chumbani na mimi nilikuwa nimelala,basi alipotoka nikatazama simu nikapekua sms zilikuwa zimefutwa hakuna sms yyte,nikatazama simu gani zinaingia sana kwake,nikaona majina mawili moja limeandikwa Mjomba na jingine Kaka.......sitamtaja jina hapa,basi nilichofanya pale nikazifuta zile namba zote halafu nikajaza namba zangu 2 ambazo nilikuwa sana situmii laini zake hata wife alikuwa hazijui,siku hiyo usiku nilikuwa nimekwenda kazini nikaamua nimcheki nikaweka line 1 ile niliyoandika mjomba nikambeep,dakika 3 ikaja sms vipi mpenzi jana nimekuja mpaka kwenu sijakukuta ulikuwa wapi? Haa nikasema hapa mwizi wangu nishamkata basi nikamjibu nikamwambia nlikuwa town lini tena utakuja?akaniambia J2 ntapata muda maana mume wangu ataingia kazini mchana'huwezi kuamini nilichat na wife kama muda wa masaa 2 hivi kiasi msg 30 hivi bia yeye kujua kama ni mimi,nilijua mambo mengi sana nilijua kiasi gani alikuwa ananicheat nilijua jinsi gani huwa ananiaga kwa kweli siku hiyo moyo wangu ulikuwa na ganzi ya ajabu,ila usiku huo huo nikafanya mpaka akajua kama alikuwa anachat na mimi,ukweli kuwa asbh nliporudi home sijamkuta wife alikuwa kisharudi kwao,hakutaka hata maongezi na mimi,baada ya hapo tuliachana na kila mtu alishika njia yake,hili jambo huwa nikilikumbuka nahisi mapigo ya moyo yanakwenda speed sana'
  Ila kidume wangu nilichukua,

  Pls msijaribu kuwafanyia hivi wake zenu kama bado mnawapenda,,,
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda sana conclution yako.................
  Ni kweli kama tunawapenda wake zetu na tunahisi kuibiwa kuna haja ya kuzungunza ili kujua sababu kwa nini una wasiwasi naye, kwani inawezekana wakati mwingine ni sisi tumechangia.......................
   
 3. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Ni kweli ndugu Mtambuzi ila hawa wenzetu ni viumbe hatari sana'kama mimi angekuja mtu kuniambia kama mke wangu anafanya upuuzi nisingeamini haraka haraka,kwa sababu ndani hakuwa na mabadiliko zaidi ya kuwa busy nakuchat basi'
   
 4. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Duh kali ulifanya kosa ulipoenda home usingechati naye ungepiga kimya ..ungepanga mkutane mahali hapo ungemkamata ..
   
 5. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Emma ningefanya vile labda ningekuwa jela mida hii,mke anauma acha kabisa,ningeuwa mtu
   
 6. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Duuuh, kweli hili ni njenje! hata mm nimepata shock ya moyo na miguu, daah, mimi bado sijaona ila najaribu kupiga picha kwa mtindo huo sijui maisha ya ndoa yatakuwaje
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  mapenzi haya.........
   
 8. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Jeff nimetoa angalizo hapo ikiwa tunawapenda wapenzi wetu basi tusipekue sana wanayofanya,maana wengi wetu sio waaminifu
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,316
  Likes Received: 2,280
  Trophy Points: 280
  Story kama hizi zinatufanya tufikirie mara mbili mbili kuoa!!
   
 10. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mi noana uamuzi wako ulikuwa sahihi kwani kumpenda mtu haimanishi ukubali kushare na watu wengine. suala ni kumwambia ukweli na yeye kama atakiri na kuomba msamaha na kuahidi kutokurudia hapo ndipo mnaweza kwenda sawa na sio vinginevyo.
   
 11. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Kweli mnama! Lakini mpk leo sikumbuki ule ushujaa wakuchat nae kwa sms nyng vile nilipata wapi,na sms zilikuwa zinaumiza sana
   
 12. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu sio kwamba zinazidi kukupa uelewa wa mahusiano ndani ya ndoa ili ukiingia sasa una ukomavu wa hali ya juu na kutoa maamuzi ya busara km alivyoshauri Mkuu Ngongoseke badala ya kutoa maamuzi ya kukurupuka?
   
 13. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,316
  Likes Received: 2,280
  Trophy Points: 280
  Zinanipa picha kwamba complications na matatizo katika ndoa ni makubwa zaidi kuliko positive hope.
   
 14. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Usiwaze sana hayo,kwa sababu wanasema kuyakimbia mapenzi ni sawa nakukimbia kivuli chako,mwisho utachoka wewe,nikuyakabili tu ila kwa hekma sana'vinginevyo utaowa sana
   
 15. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mmmh jaman mapenz yanaumiza lakn, hv nibora kutoujua ukweli ili usiumie au kuujua ukweli ili uchukue taadhari mapema??
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ngongoseke, pole sanalakini Hapo unaposema umemchukua kidume wako , pana nipa mashaka kidogo, kwa mwenendo wa huyo aliyekuwa Mkeo, hivi kweli huyo mtoto ni wako?, au uliangalia kucha tu na kujiridhisha?
   
 17. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Umenena vema kiongozi, yaani sikuhz kwakudanganyana mmmh.
   
 18. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaha kwa kidume changu hakina ubishi mzee kama vile copy kila kitu huyu kamanda na mimi,na hata wewe ukiona mimi na kamanda wangu utakubali,
   
 19. m

  mullay Member

  #19
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hamna kitu kibaya kama kugundua mpenzi wako anakusaliti, hiki kitu kimenitokea katika maisha yangu, omba yasikukute.
   
 20. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kabisa, maana kuna wale ambao baada ya kupata matatizo kama hayo wanaishia kusema sitaki tena kuwa involved na mambo haya katika maisha yangu. Lakini mwisho wa siku unaona wana-fall in love again. So,hekma ni muhimu sana katika maisha haya.
   
Loading...