Sikumbuki ushujaa ule nilipata wapi!!!!

Wakati nilipokuwa nausoma huu uzi mwili ulikuwa unanisisimka,siuji tutaishje katika ulimwengu huu wa usanii kila mahala? Imagine mtu alikubali mwenyewe kuolewa halafu anakucheat ndani ya ndoa?....duuuhhh
 
Wakati nilipokuwa nausoma huu uzi mwili ulikuwa unanisisimka,sijui tutaishije katika ulimwengu huu wa usanii kila mahala? Imagine mtu alikubali mwenyewe kuolewa halafu anakucheat ndani ya ndoa?....duuuhhh
 
Jf inaninoa sana, kila jambo hapa linafunzo ndani yake, mi'naona huyu ndugu hakuwa na papara zozote katika kugundua udanganyifu aliyo kuwa anafanyiwa, nampa pongez sana.
 
Aisee hii ngumu kumeza. Hongera kwa kutulia, na mmama naona aliona hana thamani ya wewe ndio maana akasepa!

Vipi umeoa tena au umeshaathirika kissikolojia?

Na unamuona mkeo mpya kama wa zamani, au umeshaweza kutrust tena!

A word of advice kwa wengine waliotendwa kama wewe na hawajarecover bado!

Kaunga moyo una sifa 2 kusahau nakubadilika,ni muda sasa umepita nimeshasahau ila kuowa nataraji January next mungu akipenda ntajaribu tena bahati yangu'
 
Ndio maana naipenda JayEfu, nimeshapata ma tactic mengine ya kuendesha shughuli za kipelelezi. Mimi bado naamini kuwa information is power...sikubaliani kabisa na wanaounga mkono kuwa ni bora usijue...napenda sana kuwa informed. Lol. Kwa sababu nina kifua cha kufanya maamuzi...


Kama kifua unacho ruhsa kufanya,lakini angalia mwisho wenu usije kuwa mbaya na maisha yanasonga!
 
Pole sana...umesema tusijaribu kuwafanyia kama bado tunawapenda, unajua kuna vitu vingine ni vya ajabu sana....am sure wewe kilichokufanya uchunguze ni ule u-busy wake, inafikia wakati mpaka unamuuliza lakini bado....hashtukii tu!
Kwa hiyo hapa kama mtu unampenda mkeo basi uendelee kukaa kimya, huwezi kujua nini kingefuata kuna migonjwa,kuna izo issue za watoto mzee unajiona unao watatu kumbe hamna lolote.

Dah kweli kabisa mkuu!
 
Duuh pole yalikukuta....mimi bado nahisi umefanya maamuzi mema. Ni ujinga ukiwa mtu uko kwenye ndoa na 100% kujiamini kwa maisha ya bongo ni kama ndoto. Inatakiwa from time to time, to check just in case.


Shukraan madame x ni kweli ujinga kujiamini kama tuko salama kwa mazingira haya ya kwetu
 
Mkuu, yaani kama movie. Jambo moja nalokusifia ni kuwa ulicontrol hasira zako. Hapo nimejifunza mkuu. Sasa umeoa??-na kama umeoa, je huwa hupati mang'amung'amu kwamba utakuwa cheated tena???? Pole sana.

Mkuu kuna jambo 1 nilikuja kugundua nililifanya mwanzo,ntakuja kuweka mada yake hapa ubaoni kwa sababu nahisi labda ndio ilikuwa sababu'sasa sijaowa lakini namuamini my future wife,mungu ataleta kheri
 
daaa,we mkaree,ulisomea ushushushu MOSAD nini,hii technic yako ni superb,pole sana mjomba,that's hw life it iz,jipange upya,aluta continua,goodluck ulimstukia mapema na akajindoa mwenyewe,ndo maana mi nasemaga nikimfumania mke wng anagongwa laiv,nawatumbulia macho halafu natoka nje hata siwadhuru,utaona kiwewe watakachokipata,wyf mwenyewe atafungasa virago bila kufukuzwa halaf mm najifanya kushangaa tu


Hahaha umenifurahisha sana hapo,unamtumbulia macho tu unasepa
 
QUOTE=pangu pakavu;4332330]Wakati nilipokuwa nausoma huu uzi mwili ulikuwa unanisisimka,siuji tutaishje katika ulimwengu huu wa usanii kila mahala? Imagine mtu alikubali mwenyewe kuolewa halafu anakucheat ndani ya ndoa?....duuuhhh[/QUOTE]

Pangu pakavu, sio wewe mzee hata mimi japo miaka kibao imepita ila huwa nikikumbuka lile tukio hata sielewi ndio maana heading yng nimesema sikumbuki ushujaa ule nimepata wapi'maana sikutaraji kama ningeweza kufanya vile:
 
Pole sana mambo kama haya hata adui yako usimuombe, manake inaumaa sana hasa mtuu unaemuamini
 
Mkuu kuna jambo 1 nilikuja kugundua nililifanya mwanzo,ntakuja kuweka mada yake hapa ubaoni kwa sababu nahisi labda ndio ilikuwa sababu'sasa sijaowa lakini namuamini my future wife,mungu ataleta kheri
Sawa mkuu. Tunaisubiri kwa hamu ili tuiunganishe.
 
congrats are definitely in order for the way you handled this matter in a patient and matured manner... many other people would have dealt with it differently, with possible dire consequences for you, your wife and the guy she was cheating with
 
Ulijitahidi sana kucontrol hasira zako ni watu wachache sana wanaoweza,hongera!
 
Ujamalizia vizuri, what you did was right? Kama ulikuwa wampenda na Alikuwa anacheat ulitaka akwambie hataridia tena ili muendelee kuishi? I would so very the same, but sitapenda ajue hiyo kitu, ningekuja Mwambie Kiaina.


UOTE=Ngongoseke;4328326]Habari zenu wana Jf

Leo nataka kushea pamoja na nyinyi mkasa flani ambao uliwahi kunitokea katika maisha yangu'

Nikiwa nimetimiza miaka 26 miaka ya nyumba niliamua kuowa,kwa kweli mimi na mke wangu tulikuwa na maisha ya kawaida tu,tulikuwa tunaishi kwa furaha tu hapakuwa na tatizo kubwa bali ya kawaida tu,
Baada ya miaka 2 katika ndoa tulipata mtoto wa kiume,
Toka hapo tulipopata mtoto wetu hapo ndio nikaanza kuona mabadiliko ya wife,alikuwa busy sana muda mwingi kuchat na kutuma sms sikujua anatuma sms kwa nani lakini sana alikuwa busy,ikabidi nimuulize akanijibu vizuri tu kama hakuna kibaya anachofanya katika simu nikapotezea,
Kadri siku zilivyokwenda ndio alizidi kuwa busy na simu mpaka siku 1 nikamwambia nina wasiwasi na matumizi yako ya simu sio mazuri,tulibishana sana ila mwisho nikamwambia nitakuthibitishia siku 1 niyasemayo,
Basi siku 1 aliweka simu yake chaji chumbani na mimi nilikuwa nimelala,basi alipotoka nikatazama simu nikapekua sms zilikuwa zimefutwa hakuna sms yyte,nikatazama simu gani zinaingia sana kwake,nikaona majina mawili moja limeandikwa Mjomba na jingine Kaka.......sitamtaja jina hapa,basi nilichofanya pale nikazifuta zile namba zote halafu nikajaza namba zangu 2 ambazo nilikuwa sana situmii laini zake hata wife alikuwa hazijui,siku hiyo usiku nilikuwa nimekwenda kazini nikaamua nimcheki nikaweka line 1 ile niliyoandika mjomba nikambeep,dakika 3 ikaja sms vipi mpenzi jana nimekuja mpaka kwenu sijakukuta ulikuwa wapi? Haa nikasema hapa mwizi wangu nishamkata basi nikamjibu nikamwambia nlikuwa town lini tena utakuja?akaniambia J2 ntapata muda maana mume wangu ataingia kazini mchana'huwezi kuamini nilichat na wife kama muda wa masaa 2 hivi kiasi msg 30 hivi bia yeye kujua kama ni mimi,nilijua mambo mengi sana nilijua kiasi gani alikuwa ananicheat nilijua jinsi gani huwa ananiaga kwa kweli siku hiyo moyo wangu ulikuwa na ganzi ya ajabu,ila usiku huo huo nikafanya mpaka akajua kama alikuwa anachat na mimi,ukweli kuwa asbh nliporudi home sijamkuta wife alikuwa kisharudi kwao,hakutaka hata maongezi na mimi,baada ya hapo tuliachana na kila mtu alishika njia yake,hili jambo huwa nikilikumbuka nahisi mapigo ya moyo yanakwenda speed sana'
Ila kidume wangu nilichukua,

Pls msijaribu kuwafanyia hivi wake zenu kama bado mnawapenda,,,[/QUOTE]
 
Jamani kuibiwa mke inauma mhh.. Acheni.. Bt mi nakuunga mkono bora umejua mapema maana angeweza hata kukuambukiza magonjwa
 
Jeff nimetoa angalizo hapo ikiwa tunawapenda wapenzi wetu basi tusipekue sana wanayofanya,maana wengi wetu sio waaminifu

Kuku na samaki ni watamu sana, lakini ukichunguza sana ili kujua kwa nini ni watamu unapowala, utanuna sana. Mapenzi ni matamu sana usipoyachunguza, utakapoanza tu? nyongo itaingia, ukitaka kufaidi, acha.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom