Sikumbuki ndoto

Pelly

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
265
Reaction score
341
Habari zenu, nakuja tena wataalam mnaoweza kunisaidia, sitaki kuwachosha sana, kama kichwa cha habari, nimekuwa nikiota tena sana lakini nikiamka sikumbuki hata kitu kimoja nilichoota nimefuatilia nimeambiwa hivyo ni vifungo fanya kutafuta mtu ufungue haraka sana, nimeamini ni kweli maana hadi ugomvi na wife haushi, pesa zenyewe mara unapata kidogo au nyingi lakini ukipata haitoshi maana hapohapo imeshapata shida maana siyo matumizi, mfano mgonjwa au msiba.

Asanteni
 
Habari, kama nilivyopost kusahau ndoto yaani sizikumbuki kabisa, kuna watu wanasema majini yanakufunga, wengine vifungo vikali sana,nuksi nk, naomba nielezee hiyo mushroom na gharama zake,
asante
 
Huyo mke wako atakuwa na walakini.

Kiufupi, kama kabla hujamuoa ulikuwa unaota ndoto na ukiamka unazikumbuka, basi tatizo la kusahaulishwa ndoto utakuwa unalo chumbani kwako.
 
 
Potezea tu huenda unalala vibaya au harakati za mchana zinasumbua ubongo
"harakati za mchana zinasumbua ubongo"🀝

NB:SUBCONSCIOUS MIND,INABIDI IMSAIDIE KUKUMBUKA PALE UFIKIRI WAKE UKIGOTA KTK JAMBO ALILOLIOTA,IKISHINDIKA NDIYO
"harakati za mchana zinasumbua UBONGO" LINAPOINGIA KM MOJA YA 7BU.
AFANYE MAZOEZI MWILI UTOE JASHO,TARATIBU SUBCONSCIOUS MIND ITAKUWA ACTIVE.
 
Huyo mke wako atakuwa na walakini.

Kiufupi, kama kabla hujamuoa ulikuwa unaota ndoto na ukiamka unazikumbuka, basi tatizo la kusahaulishwa ndoto utakuwa unalo chumbani kwako.
Asante, kama nakuelewa vile!!!!
 
Hata mimi huwa sikumbuki ndoto japo najua napta sana tu ila sizikumbuki nikiamka. Binafsi niko okay na hilo.
 
Kikristo kuna maana nyingi ukisahau ndoto
1. Ni mpango wa Mungu usahau ili utafute mtu wa kukusaidia (ref, Daniel na mfalme Nebkadreza)
2. Shetani anakusahaulisha ili usijue muelekeo wa maisha yako mf, wa ngano na magugu ktk biblia
3. Wewe ni muota ndoto kama Yusufu, lakini malango yako ya ndoto yamemetekwa na adui. Pia kama ulikuwa unaota ndoto zamani na hizo ndoto zinatokea, ukasimulia watu, kuna uwezekano mkubwa walikuibia hiyo karama wanaitumia wao. Anza kuiombea karama yako na malango yako ya ndoto kwa kutumia Damu ya Yesu, utaanza kuzikumbuka zoteπŸ™πŸ™
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…