Jamani rejeeni hotuba ya Mwinyi ya kuleta Azimio la Zanzibar - ipo humu humu JF kwenye mjadala wa Azimio la Zanzibar, kwa kiasi fulani yuko sahihi hawakulifuta kabisa Azimio!
...........wangeacha hata ile miiko ya uongozi....duh hivi ile tume ya maadili ya viongozi pale Ohio netx to Holland house inafanya kazi bado?....
NINAMUHESHIMU MZEE MWINYI ZAIDI YA MAELEZO ! UJAMAA(azimio la arusha) LINABAKI KUWA PEKEE MPAKA SASA LENYE NIA YA KWELI NA YA DHATI KUMSAIDIA MTANZANIA....! HUENDA BABA YETU MWINYI AMEGUNDUA HILO NDO HATA SASA AMEKUJA NA HOJA HII....MZEE HAJAKOSEA INABIDI TUMPONGEZE KWA KUNG'AMUA HILO.......AMELETA UBEPARI LAKINI AMEONA YOTE SI MAJIBU KWA MTANZANIA BALI UJAMAA....(azimio la arusha)HONGERA NA PONGEZI MZEE WETU KWA KUJIREKEBISHA....WENGINE NAO WAUNGE MSTARIIIIII....!
mwacheni Nyerere aitwe Nyerere- Baba wa Taifa
synthesize you are talking, big up men. nimekua nikiliona suala hili exactly as you say, na nimekuwa nikijiuliza sana kwa nini watu wanamuandama sana mkapa wanamsahau mwinyi wakati infact uozo mkubwa sana umefanyika pale kuliko zama nyingine yoyote ya uraisi tanzania. isitoshe, hakukuwa na creativity kabisa katika uongozi wa nchi hii. tujifunze kusema ukweli.
Mkuu nahisi ameanza kuona picha halisi ya Monster waliokuwa wanamtengeneza. Anatishia hata uhai wa wale waliomvumbua. Namuonea huruma sana kujaribu kugeuka nyuma kwa namna ya kutaka tuone kwamba hakukuwa na tatizo lolote baada ya azimio la zanzibar, maana anaweza kugeuka jiwe la chumvi.Ninachoelewa kuhusu AZimio la Arusha ni kuwa ilikuwa kauli ya kiuchumi ilyosema njia kuu zote za uchumi zitamilikiwa na Serikali (Taifa) ndiyo maana msamiati wa kutaifisha ukazaliwa. Kule Zanzibar mwaka 1985 ikatoka kauli kuwa ubinafsi ruksa. Sasa Mzee Mwinyi anataka kutuambia nini? Hajui AD iliuwawa Zanzibar? Lakini kwa umri alionao tumsamehe bila shaka amesahau na hajui tofauti
Kaa kayasema kweli hayo basi atakuwa anataka kuwazuga wakatoliki na kipenzi chao 'saint Nyerere' hususan ktk kipindi hiki cha kuelekea mikwaju ya penati 2010.
BTW, ni vema hii benki imeanzishwa at last, maana last time nilisikia BOT walikua wanaweka kauzibe wakidai wakatoliki wana mapesa mengi wakianzisha benki wataleta mkanganyiko kwenye mambo ya fedha. Tunategemea benki hii itakuwa kimbilio la wakosefu sorry I mean la wanyonge..
Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, amesema Azimio la Arusha halijafutwa kama watu wengi wanavyodhani. Mwinyi alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Benki ya Biashara ya Ukombozi, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
***
Ujumbe kwa Mwinyi:
Ningependa kukumkumbusha Mheshimiwa Mwinyi kile alichosema Mwal. Nyerere baada ya Azimia la Zanzibar, kwamba "Wale wenye akili tukatambua Azimio la Arusha limeshafutwa".
Basi Mheshimiwa Mwinyi, kumbuka unapotoa kauli sizizo na msingi kama hiyo hapo juu wapo watu na akili zao wanaokusikiliza, kama alivyosema Mwalimu Nyerere. Kama huna cha kuongea afadhali ukae kimya na kufurahia pension yako. Kuna mengi uliburuzwa kufanya na wenye pesa, ambayo ni bora kwetu tukayasahau na kuganga yaliyopo, kwa sababu kama kuna kiongozi aliyetengeneza msingi wa ufisadi Tanzania basi ni wewe Mwinyi. Uliharibu misingi ya Azimio la Arusha kufikia hatua watu kuona elimu haina maana tena, bali kuwa mfanya biashara fisadi na wa tenda hewa. Uliua heshima yote ya kuwa mfanyakazi wa serikali na mashirika yake na kufanya wafanyabisahara, hasa wahindi, waonekane watu bora sana nchini. Ukaua heshima ya Ikulu, ya ofisi za Wizara, ya mamlaka za vyombo vya serikali, ukakuza mamlaka na utu wa pesa, tofauti kabisa na misingi ya Azimio la Arusha.
Ukatudanganyia "economy liberalization" wakati hasa policy yako ilikuwa "ufisadi liberalization".
Leo hii unathubutu kusema hukuua Azimio la Arusha!!! Hiki ni kichefuchefu kibaya zaidi ya cha mimba changa.
Mwinyi huna la kutuambia Watanzania, na tunakustahi sana, huenda usivyostahili.
Sasa yeye anamuogopa Mungu?
1.Si ndiye aliyetuletea shida ya umeme na IPTL yake?
2.Tunaambiwa humu JF mwanawe Hussein anajenga apartment blocks hapo Seaview..kapatawapi hiyo plot na hizo pesa?
3.Alimtoaje Capt.Aziz jela na kuwaacha watoto wa walala hoi jela eti kwa kuwa mama yake alienda kumlilia...mama wangapi wana watoto jela wengine bila hatia?