Sikukuu ya Wafanyakazi (MEI MOSI 2012) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikukuu ya Wafanyakazi (MEI MOSI 2012)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by marejesho, Apr 23, 2012.

 1. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Kutokana na yaliyoendelea bungeni,imenilazimu kujiuliza maswali mengi!
  Tarehe 1/5/2012 ni sikukuu ya Wafanyakazi !Je, Serikali pamoja na kuwa na deni la trilioni 14,watathubutu kukopa tena kuadhimisha siku hii?
  Kutakuwa na ulazima gani wa kusherekea siku hii wakati wananchi wana majeraha mioyoni mwao?
  Wabunge ambao ndio wawakilishi wao,wamedharauliwa mchana kweupe!!!!

  Nimekumbuka mambo ya mbayuwayu,nikasikia uchungu sana!Mwaka jana,wafanyakazi waliambiwa itachukua miaka mingi sana kwa Serikali kuweza kulipa kima cha
  chini cha 350,000/ kwa mtu mmoja!Sasa wafanyakazi hawa wanagundua kwamba Serikali ilikuwa na uwezo wa kuwalipa hata zaidi ya laki 5 kwa mtu mmoja kama fedha za wizara moja tu zisingeibwa na mawaziri!

  Hivi kweli,mwananchi ambaye analipwa laki na nusu,ataenda uwanjani kupiga makofi?Ili iweje?Mchele,sukari,mafuta ya kupika,unga,sabuni,mafuta ya kujipaka,kuni,mkaa,gas,umeme,maji vyote vimepanda bei kutokana na watu wachache walioaminiwa wakaamua kuwasaliti wananchi!!
  Mfanyakazi huyu kwake maisha yamekuwa machungu na ndio maana wanafanya alimradi liende tu!!
  Tegemeo lake,lilizimia mwaka jana(TUCTA)!!Je,watafufuka tarehe moja!!!!!!!

  I am crossing my fingers ili nisisikie kwamba hizi sherehe zikitangazwa kwamba zitakuwepo tarehe moja!!!
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Sikukuu ya wafanya kazi hugharimiwa na TUCTA
   
 3. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa kunijulisha!!
  Ina maana TUCTA,wanalipia viongozi wote wakiserikali watakaoalikwa sehemu itakayofanyika kitaifa?
  Na sherehe za mikoani ni TUCTA peke yao wanahusika?
  Kwa namna ninavyosoma comment za watu baada ya Bunge letu kuhairishwa,sidhani kama wafanyakazi wana hamu na hiyo sikukuu tena!Angalau walizoea kupata maneno ya faraja,but this time, it won't happen!!!Mishahara haitaweza kubadilika kwani serikali haina fedha!
   
Loading...