sikukuu 14: 3-5

sikukuu 14: 3-5

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
5,755
Reaction score
7,270
sikukuu 14: 3-5 basi ikawa watu wa muungano wa nchi zile mbili walipokutana katika kutaniko kuu ndipo akainuka Mkuu wa ule Muungano, mwana wa Mrisho kutoka kabila la watu wa Mashariki, tena ilikuwa yapata miaka 2014 tangu alipozaliwa Masihi. Basi katika kutano lile walikuwapo watu wengi, mkuu wa nchi alivyoona macho ya watu yakimtazama kwa huruma akazijua nyoyo zao, kwa maana watu wake walipenda kujisherehesha kwa nyama za kuoka na pombe za vimea. Basi mwana wa Mrisho akapaza sauti yake na kusema, enyi watu wa bara, na enyi watu wa visiwani sikieni, natangaza ya kwamba siku ya tano ya wiki itakayofuata mpumzishe miili yenu, na mle bata na hata jua litakapochomoza tena endeleeni hata litakakapozama mpaka pale siku ya tano ya wiki itakapofika. Na tazama palitokea yowe kubwa, halikuwa la vita wala la kuogofya bali la furaha, la kugonga viganja na kupongezana
 
Haya maandiko mengine bwana! Sijui yameshushwa na manabii vikatuni???!!!
 
Back
Top Bottom