Sikujua kama LUKUVI na SENDEKA ni Matabularaza!

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Kwa wale ambao tumekuwa tukifuatilia mjadala wa Bunge asubuhi hii mtakubaliana na mimi kwamba Lukuvi ni tabularaza wa kujitakia kwa kutoweza kuielewa mchango wa mchungaji Msigwa(mbunge CDM Iringa Mjini). Msigwa alisema waziri mkuu alikuja na ndege mbili na msafara wa magari 50 na barabara zilifungwa kwa masaa 4 na kuzuia magari yanayotoka Dar, Moro, na Mbeya kuingia Iringa.

Yeye Lukuvu au ILUVI akageuza hoja na kuomba mwongozo wa spika na ku-edit hoja ya msigwa na kusema ifuatavyo" Mbunge amedanganya na atueleze inakuwaje waziri mkuu anapanda ndege mbili kwa mpigo kuja Iringa na pia Mbunge atueleze ni lini Waziri mkuu alikuja Iringa barabara zikafungwa huko Dar, Morogoro, Mbeya na huku Iringa". sasa hii ni kutabulazara au uzushi au kumvumishia Mbunge tu kwa sababu anatoka Upinzani. Hivi Lukuvi kwa namna hii tuseme kichwani ana ubongo au sifongo kwani ujinga alio- comment kwa mtu wa kada yake umemdhalilisha.

SENDEKA yule shujaa wa zamani naye naona anazeeka vibaya kwa kutaka kuviza analysis za watu wanaolinganisha muda tuliopata uhuru wa miaka 50 na kiwango cha maendeleo tulicho nacho. Yeye anasema eti mtu kulinganisha nchi hii na mtoto mdogo eti ni kutukana na kuudhi!!!!. Akili zake za kipori hazitaki kuweleza kwanini kila mtu anaweza kuelezea ktu kilekile kwa mtazamo tofauti.

Anachotaka anataka watu wote waelezee mafanikio ya uhuru wa nchi yetu kwa mtazamo wa CCM au akili yake. Huu ni ujinga kwa sababu kuna watu hawakuwahi ona tofauti ya TZ kabla na baada ya uhuru. SENDEKA asilazimishe watu kusema uongo ili tu kuishabikia CCM.

Analysis ya kila mtu kuhusu kiwango cha maendeleo ya hii nchi tangu uhuru inatofautiana kwa kila mtu utakayemwuuliza na hata mifano itakayotolewa itatofautiana. Aliyetoa mfano wa mtu wa miaka 50 anafanya mambo ya stage ya mtoto mdogo hajakosea kabisa kwani hiyo ndo analysis yake.

Wao ni Tabularaza wa kuelewa au kwa makusudi au kwa kukosa ufahamu wa jinsi maendeleo ya nchi yetu hayafanani na nchi iliyopata uhuru mwaka 1961. Kama nabisha akafananishe TZ na nchi nyingine.
 
Jamani CCM kama kuna mwenye naninihii basi huwa baada ya muda flani huwa zina-expire!! anaekataa akatae tu
 
Mimi nilishasema huko magamba hakuna mwenye akili timamu hata mmoja , huko kuna manyang'au tu, huoni yanavyoparurana yenyewe kwa yenyewe?
 
Mi leo nimeshuhudia wanayosema watu kuwa CCM hamna mwenye akili. Wanakwenda bungeni ku-block wenzao ambao lengo lao bungeni ni kuitoa nchi kwenye umaskini na ujinga wa zamani. Wao kwa sababu hawataki wanzo mbadala basi wata crash kila kitu kinachosemwa na kambi ya upinzani. Sas inapofika mahali hata Lukuvi anajiunga na wajinga tu- question ufahamu wake wa mahitaji halisi ya watanzania including expectation za watanzani
 
sendeka ana akili timam lkn ameziacha umasaini alipokuwa anaondoka kuja dom
 
Hii kali haki ya mama................! Haya ndo matatizo ya kujiandaa kubishia kila kitu billa kujiuliza mara mbili!
 
Ndugu wana Jamvi Elimu ya Lukuvi Mwaijua?
Yaani hapo amejitahidi kweli utafikiri analikuwa na DESA!
 
Katika semina za wabunge wasisahau kupewa semina ya Philosophical Language hasa kwenye kipengele cha Analytical Philosophy, inaonekana Ole Sendeka amejikita zaidi kwenye surface meaning, kitu ambacho kwa level yake ni kichekesho, katika mijadala mingi huwa kuna technical and philosophical term zinazohitaji deep analysis na si mtu kutaka Mwongozo wa spika kumtaka Mbunge aongee kwa mafikirio ya Ole Sendeka na WanaCCM. Tafadhali kama elimu na ujuzi wa kupembua hoja unakutupa, then ni bora uka kaa kimya, si kila kitu ni lazima ukichambue na kukitolea masahihisho, kuna masahihisho mengini ni ya kujiaibisha ni kama hili la leo la Ole Sendeka
 
Ndio chama cha magamba hicho! wanakaba mpaka penalti wataelewa tu mwaka huu lazima bungeni zitapigwa.
 
Ndugu wana Jamvi elimu ya Lukuvi Mwajua?
Mara ya mwisho kusoma kitabu cha Mafisadi wa Elimu kile cha Kainerugaba
Alikuwa na Ngazi Ngazi ya elimu ya Mwalimu wa UPE!wale ambao hata Form 4 hajafika!
hapo leo Amejutahidi ile mbaya!
 
tatizo hawa wamekaririshwa na viongozi wao jinsi ya kukabiliana na cdm
bunge lililopita watu kama kina selendeka, kahama,kimario, seleli, mwakyembe walikuwa wanaweka maslah ya Taifa mbele sasa hivi Nape na JK wamewaambia wote waweke maslah ya ccm mbele na mitumbo yao! nao wamenywea wakaufyata!
 
Lukuvi hana Elimu, UpE UNAMTAFUNA. . . . Hana hadhi ya mimi kumjadili ni kilaza tu mzungu wa reli.
 
Yaani ningekuwa mimi msigwa ningemuumbua pale pale bse lukuvi kaongea vitu tofauti na msigwa alivyoongea!
 
dah inahudhunisha saaana kuona magamba kumbe ni vilaza wasiojua zuri na baya ni lipi.
 
Back
Top Bottom