Sikubaliani na Waziri Membe Kuhusu Rada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikubaliani na Waziri Membe Kuhusu Rada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ELNIN0, Mar 30, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  WanaJamii Sikubali kabisa na serikali yetu kwamba Pesa za ziada za ununuzi wa rada zirudi Serikalini ( HAZINA)

  Jana nimemsikiliza Waziri wetu Membe akihojiwa na Charles Hilary wa BBC kuhusu pesa za zaida ambazo serikali ililipia katika ununzi wa Rada. Waziri anasema serikali ya Uingeleza lazima irudishe pesa hizi Hazina kwa sababu ni mali ya walipa kodi wa Tanzania.
  "Lazima pesa hizi zirudishwe serikalini - HAZINA maana ni mali ya walipakodi na si vinginevyo, pamoja na mambo mengine pia nimekuja kufuatilia jambo hili kuhakikisha hawa wenzetu wanatuelewa" - Membe akiwa U.K.

  Wakuu mimi sikubaliani kabisa na waziri kwa misingi ifuatayo
  i) Baada ya fununu kuwapo na harufu ya rushwa katika sakata hili - je serikali ilifanya uchunguzi wowote?
  ii) Na kama uchunguzi ulifanyika je serikali ilichukua hatua gani pamoja ya kuwafikisha wale wote waliohusika kufikishwa katika vyombo vya dola na sheria?
  iii) Baada ya kusikia habari kuwa Serikali ya uingeleza inaanza kuchunguza sakata zima je serikali ilitoa mchango kamilifu?
  iv) Je Serikali mpaka sasa imechukua hatua gani katika sakata hili baada ya kupata riporti kwamba kulikuwa na rushwa katika ununuzi na ushahidi kutolewa? na kama bado kivipi basi inakuwa nyepesi (serikali) kuomba pesa ambazo kwanza haikuwa na uchungu nazo zirudi serikalini?

  Binafsi sina imani kabisa kwamba endapo pesa hizi ( 28,000 pounds) zikirudi Hazina zitakuwa salama, nina wasiwasi zisije zikaelekezwa kwenye matumizi mengine kama kampeni au hata kuyeyuka tu.Ninachoomba serikali iwaachie wale waliotusadia kuzikomboa hizi pesa waamue watazielekeza wapi kama aibu na tushaonekana ni watu wa aina gani mbele ya mataifa.

  Wakuu nisaidieni hapa hii senario: Unaibiwa kitu then mtu anakwambia umeibiwa humjali - mtu huyo huyo anafanya uchunguzi na kukusaidia kupatikana kwa kitu chako na ushahidi anakupa kwamba furani ndiye mwizi au tapeli wako sasa badala ya kuanza kuhangaika na mwizi au tapeli wako wewe unataka jamaa akurudishie kitu chako kwanza - hapa sipati picha sababu watuhumiwa wapo mtaani tu wanakula kuku na wanajiandaa na uchanguzi mkuu majimboni kwao. kweli bongo tabararee

  Binafsi nashauri hizi pesa zielekezwe kwenye wilaya zisaidie kuboresha zahanati hasa vitengo vya uzazi - Pesa hizi wapewe NGO's ili kufanya shughuli hii kwa usahihi na uwazi.
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Mar 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  nakubaliana nawe Elnino kwa asilimia kubwa ya maelezo yako.
  nimekuwa namsikiliza Mmembe kupitia BBC London Idhaa ya Kiswahili mara kadhaa, akitoa ufafanuzi juu ya hili swala.
  jambo moja ambalo mEMBE ANAPASWA KUTUELEZA KWANIABA YA SERIKALI YA CCM kwamba wamefikia wapi katika kuwakamata kina Chenge na Idrs Rashid waliohusika na Hasara hiyo, je watendaji wa serikali waliohusika na uhuni huo wameisha fukuzwa kazi ama kufugwa....aaache kung'ang'ania pesa hizo.
  kwanza awafikishe waharifu hao mahakamani kisha mission B ndio anaweza kwa aibu kuomba hizo pesa.
  Otherwise anajipambanua kama mmoja kati ya viongozi wanaopenda tabia za kulindana.
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Zipo? Zinarudishwa?
   
 4. C

  Chief JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,488
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Serikali inataka itafuniwe, yenyewe imeze tu, basi.
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkuu pes ni lazima zirudi hazina ndipo zipangiwe bajeti kama ni kwenda wilyani au kokote kule..We ulitaka zikakae wapi?Hazina zinaenda kuhifadhiwa sio kutumiwa..
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa vizuri pesa hizi zingeenda moja kwa moja kwenye kwenye asasi za kiraia zinazoshughulikia mambo ya kijamii maana kuzipeleka pesa hizi serikalini una uhakika zinafika na zitapewa kazi muhimu?
  Kama mfano tu hebu nifafanulie pesa za EPA zilielekezwa wapi ? na je zilifanya kazi husika?
   
Loading...