Sikubaliani na mgomo wa wafanyabiashara

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
375
500
Ni siku ya 3 Leo wafanyabiashara wa maduka makubwa na madogo jijini Mwanza Wako kwny mgomo na hawafungui maduka kabisa. Halo hii pia limewahi kutokea Mbeya na Dar. Binafsi sikubaliani nao kabisa kwa sababu
1) Kulipa kodi ni lazima ili maendeleo yapatikane, bila hizi machine TRA hawawezi kujua jumla ya mauzo yako ili ulipie ile asilimia inayotakiwa kisheria. Utaratibu wa zamani wa Ku estimate au kuangalia vitabu vya risiti mlikuwa mnajua jinsi ya kuiba na pia ulikuwa unatoa mianya ya rushwa
2) Kodi ni kubwa ndio, lkn mbona wenzenu wafanyakazi wanalipa tena kwa lazima kukatwa mishahara juu kwa juu? tena kubwa mno kuliko hata hii ya kwenu? Tatizo mlizoea ujanja ujanja huko nyuma.
3) Migomo yenu haijengi Bali inaumiza wananchi na nyinyi wenyewe. He huko Dar na Mbeya walivyogoma ilikuwa ndio suluhu?
4) Mnalalamika machine ni ghali, eti tsh 850,000/- kulinganisha na China $50. Hivi hebu tuseme ukweli jamani, machine km ile ya ya Electronics ununie kwa $50 itafanya kazi kwa muda gani?? Sehemu yenyewe ni China???? Cheap is expensive....

Hebu fungueni maduka na mlipe kodi, acheni kulalamika lalamika, na mjue kwamba duniani more watu wanalipa kodi tena kubwa sana tofauti tu ni kwamba wenzetu wanazitumia kodi hizo vizuri.
 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,767
2,000
hii inashangaza sana kwa serekali kutokuwa na msimamo,wangapi hapa tumeajiriwa na tunalipa kodi zaidi ya kipato cha chini, tunabaki kulalamika kimya kimya tukipokea slips,
Leo hawa wanatunyonya na hawataki kulipa kodi.....
 

By hair

Senior Member
Sep 6, 2013
141
0
Tatizo lenu hamjui kero zilizopo kuaacha hiyo mashine,kwanza mjue walipa kodi ni wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara wadogo na wakati,wafanyabiashara wakubwa,pamoja na makampuni makubwa hawalipa kodi ipasavyo,hata nyinyi mtakapokuja kuamka mbona mtagoma tu,hakuna mtu anayekataa kulipa kodi,kwavile tunajua umuhimu wa kodi.serikali haitozi kodi kwenye madini,kwenye makampuni ya simu,na hata hizi kodi tunazolipa si tunashuhudia jinsi wanavyozila kwenye halimashauri,na manispaa zetu.kingine mashine hizo zitumiwe na wafanyabiashara wakubwa wenye mitaji mikubwa,wanoingiza mizigo kutokana nje.Na sio kwa wenye mitaji midogo,niwape mfano kidogo kuna mfanya biashara mmoja wilayani tarime,Ana duka,Sheli,na Pia anauza na magari,na Ana mabasi Pia,biashara yake ni ya mabilioni,lakini Hana mashine,na hakuna anayethubutu kumsogelea,kwa Hali Kama hiyo usawa uko wapi,tukubaliane kila mtu alipe kodi kulingana na uwezo wake,kusiwe na upendeleo ,na kodi hizo zikafanye kazi husika.sio tena wazipige na kwenda kuzificha uswisi.nyerere alisema serikali corrupt hakusanyi kodi kwenye makampuni makubwa, Bali itakusanya kodi kwa wafanyabiashara wadogowadogo.Hatuwezi kufika kwa mtindo huu.
 

brown mshani

Member
Oct 21, 2013
8
0
wewe mi nama huelewi bado kuhusv machine hizo, kusema eti walizoea ujanja wa kuiba uko nyuma c hoja, kinacholengwa hapo ni kunyonya kila kitu kinachozalishwa na wananchi(surplus). kwann hawataki wav waendelee jamani. wameshndwa kukusanya hela kutoka maliasili zinazoibwa, kuzuia mafisad bal wanataka kuchukua kwa watu wanaotja jasho. mi naona wafanyabiashara wakomae tu
 

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
375
500
Tatizo lenu hamjui kero zilizopo kuaacha hiyo mashine,kwanza mjue walipa kodi ni wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara wadogo na wakati,wafanyabiashara wakubwa,pamoja na makampuni makubwa hawalipa kodi ipasavyo,hata nyinyi mtakapokuja kuamka mbona mtagoma tu,hakuna mtu anayekataa kulipa kodi,kwavile tunajua umuhimu wa kodi.serikali haitozi kodi kwenye madini,kwenye makampuni ya simu,na hata hizi kodi tunazolipa si tunashuhudia jinsi wanavyozila kwenye halimashauri,na manispaa zetu.kingine mashine hizo zitumiwe na wafanyabiashara wakubwa wenye mitaji mikubwa,wanoingiza mizigo kutokana nje.Na sio kwa wenye mitaji midogo,niwape mfano kidogo kuna mfanya biashara mmoja wilayani tarime,Ana duka,Sheli,na Pia anauza na magari,na Ana mabasi Pia,biashara yake ni ya mabilioni,lakini Hana mashine,na hakuna anayethubutu kumsogelea,kwa Hali Kama hiyo usawa uko wapi,tukubaliane kila mtu alipe kodi kulingana na uwezo wake,kusiwe na upendeleo ,na kodi hizo zikafanye kazi husika.sio tena wazipige na kwenda kuzificha uswisi.nyerere alisema serikali corrupt hakusanyi kodi kwenye makampuni makubwa, Bali itakusanya kodi kwa wafanyabiashara wadogowadogo.Hatuwezi kufika kwa mtindo huu
.[!!]Mkuu, ikiwa ni sheria na kila biashara ikiwa na mashine, mianya hii ya Rushwa ambayo huyu jamaa uwezekano mkubwa ni kwamba anaitumia haitakuwepo tena. Na kinachotakiwa ni kwamba kila biashara either kwa udogo wake au ukubwa wake ilipe kodi accordingly
 

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
375
500
wewe mi nama huelewi bado kuhusv machine hizo, kusema eti walizoea ujanja wa kuiba uko nyuma c hoja, kinacholengwa hapo ni kunyonya kila kitu kinachozalishwa na wananchi(surplus). kwann hawataki wav waendelee jamani. wameshndwa kukusanya hela kutoka maliasili zinazoibwa, kuzuia mafisad bal wanataka kuchukua kwa watu wanaotja jasho. mi naona wafanyabiashara wakomae tu
Kisheria ni kwamba, chochote unachozalisha lazima ukilipie kodi, uwe mfanya biashara mdogo au mkubwa, ndo maana MFAGIZI aliyeajiriwa analipa kodi na MENEJA naye analipa kodi, huu ni ubinafsi tu wa wafanyabiashara hamna lolote! Hilo la Serikali kushindwa kukusanya hela toka vyanzo vingine ni sawa lakini hali'justify kwa nini mfanyabiashara asilipe kodi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom