palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,463
Kwa kifupi kuna mwanamke ameniulizia kama hajaridhika na matokeo ya kipimo cha DNA kinachofanyika pale Ocean Road, je kuna njia yoyote ya msaada zaidi ya kurudi palepale,,,amefanya kipimo kwa takribani mara tatu sehemu hiyohiyo lakini haridhiki na matokeo anayopewa sasa anachotaka ni msaada wa kisheria au wa kijamii ni vipi anaweza kusaidiwa kwasababu yeye anaamini mtoto aliepimwa ni wa mume wake lakini kipimo kinakataa.
La pili, je kipimo kikionyesha kutoa majibu yasiyo sahihi unaweza kudai fidia kwa wao kuja kukulipa..mfano kipimo kikisema Fulani ni mtoto wako halafu baada ya miaka kumi mkapima tena na mwanaume mwingine (kukitokea mazingira ya mtu mwingine kudai yule ni mtoto wake) ikaonekana mtoto sio wako ni wa yule mwanaume mwingine,,,je mazingira hayo unaweza kudai fidia kwasababu tangu majibu ya kwanza yaliposema mtoto ni wako ulianza kutumia gharama za kumlea..
mkuu nikutoe wasiwasi hiyo DNA (Deoxyribonucleic acid) haibahatishi hata kidogo, unachopewa ndiyo hicho ulichonacho. Yawezekana mtoto alibadilishiwa kama watu wengi hapa wanavyoongea au ni kweli yeye ni mama wa huyo mtoto lakini baba siyo huyo. wanawake wana siri sana yawezekana alichepuka lakini hajui ni linialipata mimba. Mathalani mwanamume alikuwa safarini kwa muda wa miezi 6 halafu mwanamke akawa anachepuka lakini akaacha kuchepuka miezi miwili kabla ya mume wake kurudi na mwezi mmoja kabla ya mume kurudi akapata hedhi. kwa namna hii akajiridhisha kuwa kwa vile amepata hedhi basi hakuna shida. ikumbukwe kuwa kupata hedhi siyo kwamba huna ujauzito. kuna wanawake wanapata mimba na bado wanapata hedhi. akubali alichepuka ila hajui ni lini kitu kiliingia.
Mfano hapo chini nilipozungushia nyekundu ni vinasaba vya mama na mtoto na namba zenye rangi nyekundu ni mtoto na baba.